Kitu kingine kinachoharibu nguvu za kiume ambacho hujawahi kukifikiria

Vinavyoharibu nguvu za kiume

Last Updated on 24/09/2020 by Tabibu Fadhili Paulo

Pengine tayari unafahamu kuwa kutokujishughulisha na mazoezi ya viungo mara kwa mara ni hatari kwa afya yako ya nguvu za kiume. Ndiyo hilo ni jambo ambalo kila mtu analijuwa (common sense).

Jina langu naitwa Fadhili Paulo. Endelea kusoma …

Mara nyingi tunapozungumzia vitu vinavyoharibu au kushusha nguvu za kiume huwa tunakimbia kutaja vilevi, vyakula feki, kutokujishughulisha na mazoezi ya viungo na mfadhaiko wa akili.

Hivyo ni vitu vinavyojulikana wazi kwa watu wengi kwamba ndiyo vinahusika na kushusha nguvu za kiume, Lakini kuna jambo unalifanya kila siku, kila wiki na kila mwaka tena kwa miaka sasa na hujuwi kama linahusika na kushusha nguvu zako za kiume moja kwa moja.

Inawezekana unakula vizuri kila siku, upo bize na mazoezi na unaepuka vilevi na msongo wa mawazo lakini bado unakosa nguvu za kutosha kitandani kwa sababu tu kuna jambo unalifanya na hakuna mtu amewahi kukuambia kama linaharibu vibaya sana nguvu za kiume na uwezo wa mwanaume kuhimili tendo la ndoa.

Ndiyo wewe unadhani kwakuwa unaenda kufanya mazoezi kila siku basi hiyo inatosha, si ndiyo?.

Je ni kitu gani hicho kinachoharibu nguvu zako za kiume kila siku bila wewe kufikiri wala kudhani? Jibu ni Kukaa masaa mengi kwenye kiti ndicho kitu kinachoharibu nguvu zako za kiume kimya kimya bila wewe kujuwa na hakuna mtu amewahi kukuambia hilo mpaka sasa.

Ukweli ni kuwa hata kama wewe ni mtu wa kutembeatembea hapa na hapa lakini kama masaa mengine mengi yanatumika ukiwa umekaa kwenye kiti, mwili wako hautaweza kuwa na nguvu za kuweza kuhimili tendo la ndoa.

Hizi ni sababu 7 kwanini kukaa masaa mengi kwenye kiti au chini kila siku kunavyochangia kuharibu nguvu zako za kiume bila wewe kujua:

1. Kunakosesha kupata oksijeni ya kutosha

Mara nyingi ukiwa umekaa unapenda kuegemea mgongo na siyo kukaa wima umenyooka, matokeo ya mkao huu ni kuzuia oksijeni kutembea kwa uhuru wote ndani ya mwili na mapafuni kwa ujumla.

Kisayansi tunapumua kwa uhuru wote tukiwa tumesimama na siyo tukiwa tumekaa.

Ukiwa umesimamaa ndipo mapafu hupata uwezo wa kujitanua mpaka mwisho na hivyo kuweza kutoa hewa chafu na kuingiza hewa safi ndani kiurahisi zaidi.

Hali hii ya kukosa oksijeni ya kutosha mwilini hujulikana kwa kitaalamu kama ‘hypoxia’. Wanasema kukaa kwenye kiti masaa matatu tu ni sawa na mtu aliyevuta sigara 6.

Bila kupata oksijeni ya kutosha mwilini mwako ni vigumu uwe na nguvu za kuweza kuhimili tendo la ndoa.

Kwahiyo inajulikana wazi kuwa sigara huharibu nguvu za kiume kwakuwa zinafanya oksijeni kutopatikana kirahisi mwilini. Inawezekana kweli wewe huvuti sigara ila kama unatumia muda mwingi kukaa kwenye kiti huna tofauti na anayevuta sigara moja kwa moja.

Kama ukikaa masaa matatu ni sawa na kuvuta sigara 6 kuna uwezekano unavuta sigara 12 mpaka 18 kila siku bila wewe mwenyewe kujua!

2. Unapata kirahisi kansa ya titi na kansa ya tumbo

Kansa ya titi na kansa ya utumbo mpana mara nyingi imeonekana kujitokeza kwa watu wa kula kulala yaani wale wasiopenda kujishughulisha na mazoezi ya viungo. Kituo cha kudhibiti magonjwa cha Marekani (CDC) kimesema maisha ya kula kulala yanaweza kukuweka kuwa karibu karibu na kansa kwa zaidi ya asilimia 40.

Hii ndiyo sababu wanawake wengi wanapatwa na kansa ya matiti miaka hivi karibuni sababu wengi wao ni watu wa kukaa tu nyumbani masaa mengi tofauti na wanaume ambao hutembea huku na huko kutafuta riziki ya kila siku.

Kama kukaa kwenye kiti masaa mengi kunaweza kukuletea saratani ya tumbo kunashindwa vipi kukupunguzia pia nguvu zako za kiume?

Soma pia hii > Dawa ya saratani ya tezidume

3. Una uwezekano mara 147 zaidi wa kupatwa na maradhi ya moyo

Matatizo katika mfumo wa upumuwaji ndiyo moja ya matokeo makubwa unaweza kuyapata ukiwa ni mtu wa kupenda kukaa kwenye kiti masaa mengi.

Ni matokeo ya kutokupata oksijeni ya kutosha kama matokeo ya kukaa kwenye kiti masaa mengi.

Tunafanya mazoezi ili kuongeza uwezo wa kupumua na nguvu za kiume zinategemea ubora wa afya ya mwanaume hasa kwenye mfumo wake wa upumuwaji.

Kukaa masaa mengi kwenye kiti kunaharibu afya yako ya moyo na kukuletea ugonjwa wa moyo. Ni vigumu yaani ni sawa na haiwezekani kwa mwanaume kuwa na nguvu za kiume ikiwa moyo wake hauna afya nzuri. Na ndiyo sababu unaona madaktari wanasisitiza kupunguza vyakula vya mafuta ili kuwa na nguvu kitandani kwakuwa mafuta huharibu mtiiririko mzuri wa damu mwilini na kwenye viungo vya uzazi vya mwanaume.

Kwenye utafiti mmoja uliohusisha watu 800,000, wale waliokuwa wakikaa kwenye kiti masaa 10 kila siku walikuwa na uwezekano mara 147 zaidi wa kupatwa na magonjwa ya moyo kuliko wale waliokaa kwenye kiti masaa machache au mara moja moja.

Kuna tafiti nyingi zinazokubaliana na nadharia hii na inatokana na ukweli kwamba ukiwa umekaa ni rahisi mafuta mengi kujilundika mwilini mwako kuliko ukiwa umesimama.

Kadri unavyokaa masaa mengi kwenye kiti ndivyo vimeng’enya vinavyofanya kazi ya kuchoma mafuta mwilini vinavyokuwa na nguvu chache kuchoma hayo mafuta.

Na tatizo la unene au uzito kupita kiasi lina uhusiano wa moja kwa moja na matatizo mbalimbali ya moyo.

Kukaa muda mrefu kunaleta magonjwa ya moyo na magonjwa ya moyo yanaleta upungufu wa nguvu za kiume moja kwa moja.

4. Itakuwa vigumu kitambi na uzito kukuisha

Umewahi kujaribu kufanya mazoezi, kubadili chakula au hata kufunga na bado ukawa unasumbuliwa na kitambi au uzito kuwa mkubwa? Basi jibu la tatizo lako ni kukaa kwenye kiti masaa mengi.

Utafiti unaonyesha kukaa tu kwenye kiti hata kama hauli chakula kingi bado utaendelea kuongezeka uzito.

Kwahiyo kama unataka kuondoa kitambi au tumbo au kupungua uzito kwa haraka acha kukaa masaa mengi kwenye kiti, hata kama kazi yako ni ya ofisini jaribu namna unaweza kupata meza ya kusimama huku unaendelea na kazi yako.

Kama una kitambi nguvu za kiume zitatoka wapi? inawezekana kabisa hupendi kitambi na umeshatumia dawa kadhaa ili kukiondoa lakini hakitaki kuondoka na hata huelewi shida ipo wapi. Jibu nimekupa leo nalo ni kiti chako ndiyo sababu ya shida hii kwako! Badilika kuanzia leo na hutakawia kuona mabadiliko

Soma pia hii > Dawa ya kuongeza nguvu za kiume

5. Ni rahisi kupatwa na ugonjwa wa Kisukari

Unataka kupona au kuepukana na Kisukari aina ya pili? Basi acha kukaa kwenye kiti muda mrefu.

Ni vigumu sana kama unaumwa kisukari halafu uwe na nguvu za kiume. Hakuna hilo ni ndoto.

Inajulikana wazi kwa wagonjwa wengi wa kisukari moja ya matatizo wanayoyapata ni kuishiwa hamu na nguvu ya kushiriki tendo la ndoa.

Moja ya hatari zaidi za kukaa kwenye kiti masaa mengi ni kuwa mwili unakuwa hauitiki vema kwa insulin jambo ambalo ni matokeo ya kukaa masaa mengi kwenye kiti na hii ni matokeo ya kuzalishwa kwa wingi kwa kongosho kupita inavyohitajika kama matokeo ya kukaa muda mrefu.

Wakati ukiwa umekaa tu kwenye kiti kongosho linaendelea kutengeneza insulin lakini katika mwili huo uliokaa tu, insulin inakuwa haitumiki vema na mwili jambo linalomaanisha kuwa damu sukari (glucose) haiondolewi kwenye mzunguko wa damu kwa haraka.

Hivyo uwezekano wa kupata Kisukari unaongezeka kwa zaidi ya asilimia 14 kwa Yule mwenye tabia ya kukaa masaa mengi kwenye kiti kuliko mtu mwingine yoyote na kisukari na upungufu wa nguvu za kiume ni mtu na mjomba wake, huwezi kuwatenganisha.

6. Utapatwa na maumivu ya nyuma ya mgongo

Kama una maumivu ya mgongo kwanza hata hiyo habari yenyewe ya kushiriki tendo la ndoa hutataka hata kuisikia. Utawezaje kuingia kwenye mechi hii ngumu na mgongo unauma? jibu ni hapana.

Hivyo utaona ni kwa jinsi gani mazoea haya ya kupenda kukaa kwenye kiti masaa mengi yanavyoharibu afya yako ya nguvu za kiume kimya kimya pasipo wewe mwenyewe kuwaza wala kudhani.

Ukiwa ni mtu wa kupenda kukaa kwenye kiti masaa mengi kuna uwezekano ukawa haukai hata mkao mzuri kiasi cha kuwa karibu na maumivu ya mgongo kila mara.

Watu wa namna hii pia huwa na maumivu ya kwenye uti wa mgongo kila mara. Kwa mjibu wa utafiti wa Taasisi ya ‘DNA India’ wagonjwa wengi wenye matatizo ya uti wa mgongo ni wale wenye miaka 20 na 30 na wengi wao ni wale hufanya kazi wakiwa wamekaa kwenye kiti masaa mengi.

Miaka ya sasa ni rahisi kukutana na watu wanaolalamika kupatwa na maumivu ya mgongo na wengi wao ukiwachunguza ni wale wanaotumia masaa mengi kukaa kwenye kiti.

7. Utakufa ukiwa bado kijana

Shirika la afya duniani limesema mtindo wa kukaa masaa mengi kwenye kiti ndiyo unaohusika na kuongezeka kwa uzito na unene kupita kiasi katika nchi nyingi zilizoendelea.

Na uzito kupita kiasi ni moja ya tatizo kubwa la afya kwa mtu mzima yoyote kuwa nalo ingawa wengi hawaelewi hilo, wengi hasa waAfrika wakiwa wanene au wenye uzito mkubwa ndiyo hudhani hiyo ni afya.

Uzito na unene kupita kiasi huja na matatizo mengine makubwa ikiwa ni pamoja na matatizo katika mfumo wa upumuwaji, kisukari, stroke, kukosa usingizi nk na haya yote yanaweza kupelekea wewe kufa ukiwa bado kijana.

Utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha Harvard mwaka 2014 ulitoa hitimisho kwamba kukaa kwenye kiti masaa mengi ni moja ya sababu ya vifo vya mapema kwa watu wengi.

Mtandao wa Huffington ulienda mbali zaidi na kusema kukaa kwenye kiti masaa matatu tu kwa siku ni sawa na mtu aliyevuta sigara 6 na kuwa kukaa kwenye kiti masaa mengi kunaua watu wengi zaidi duniani kote kuliko hata UKIMWI.

Pamoja na kuwa kusimama ni bora zaidi kuliko kukaa, bado unatakiwa utumie muda fulani kukaa pia, usisimame masaa yote kutwa nzima, ukisimama masaa matatu tumia nusu saa nyingine kukaa hivyo hivyo mpaka siku yako inaisha.

TUFANYAJE SASA SISI TUNAOFANYA KAZI MAOFISINI?

Zipo meza maalumu za kukusaidia kufanya kazi ukiwa umesimama

.

Na kama wewe ni dereva wa masafa marefu au ni kwamba ni ngumu kwako kufanya kazi zako ukiwa umesimama basi hakikisha unafanya zoezi la kusimama na kuchuchumaa kila siku. Tazama video ya hilo zoezi hapa chini;

.

Nini maoni yako? umekaa muda mrefu kwenye kiti na unapata mojawapo ya madhara yaliyoandikwa hapa? nipe uzoefu wako.

Soma pia hii > Mazoezi maalumu yanayoongeza nguvu za kiume

Tafadhali SHARE post hii kwa ajili ya wengine.

Kama una swali uliza hapo chini sasa hivi.

Imesomwa na watu 9,166
Kitu kingine kinachoharibu nguvu za kiume ambacho hujawahi kukifikiria

5 thoughts on “Kitu kingine kinachoharibu nguvu za kiume ambacho hujawahi kukifikiria

    1. Unatakiwa utumie muda mwingi mchana kulala. Na wakati huo huo uwe na mipango ya siku 1 kuja kuachana na kazi hiyo. Usifanye kazi hiyo maisha yako yote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WhatsApp 0714800175