Jinsi ya kuacha punyeto

Jinsi ya kuacha kujichua

Last Updated on 26/10/2022 by Tabibu Fadhili Paulo

JINSI YA KUACHA PUNYETO

Punyeto ni tendo lolote la kujitafutia ashiki binafsi hasa kwa kuchochea viungo vya uzazi.

Wanaochukua hatua hiyo ili wajipatie kionjo cha kuridhisha kinachofanana na kile cha tendo la ndoa kwa kawaida wanasukumwa na msisimko uliowapata, pamoja na aibu ya kujitafutia mtu na hofu ya kuambukizwa maradhi ya zinaa.

Kufanya hivyo ni kupotosha maana ya jinsia kwa binadamu, ambayo ni kufanya wawili wawe kitu kimoja kwa nguvu ya upendo ambao huanzia rohoni na kukamilika katika muungano wa miili yao.

Upendo maana yake ni kujitoa kwa muungano na mpenzi unaoleta tunda lake katika mtoto, ambaye ni kwa pamoja wa baba na wa mama, akiwaunganisha upya ndani mwake.

Katika tendo la kujichua hakuna lolote kati ya hayo: hakuna upendo wala kujitoa kwa wengine, hakuna muungano wala uzazi, isipokuwa kujitafutia iwezekanavyo furaha ya kimwili (ashiki) iliyokusudiwa na Mungu kuwa sehemu ya furaha nzima ya muungano wa ndoa.

Katika tendo hilo la ubinafsi mtu yuko peke yake na kubaki peke yake: halengi chochote nje ya mwili wake, hivyo anazidi kuzama ndani mwake badala ya kustawi kwa kujiwekea malengo mema kama vile ndoa, haki, huduma kwa wenye shida, utume n.k.

Matokeo yake ni kupoteza nguvu za mwili na hasa kuvuruga msimamo wa nafsi kwa kujisikia mnyonge, mwenye kosa na mtumwa wa tendo ambalo analikinai mara tu baada ya kulitenda. Hatimaye anaweza kupata matatizo katika tendo la ndoa.

Kwa msingi huo punyeto inahesabika kuwa dhambi kubwa, tena upande mmoja ni kubwa kuliko uasherati (kuzini kati ya msichana na mvulana), kwa sababu linakwenda kinyume cha maumbile na kuandaa njia kwa dhambi nyingine kama vile ushoga.

Ushoga kwa asilimia fulani ni matokeo ya juu ya madhara ya kupiga punyeto.

Mtu anajiona uume wake hauinuki na hauna nguvu yoyote tena sasa mwisho wa siku anaona bora awe shoga tu.

Hata hivyo elimu nafsi inatueleza pia urahisi kwa mtu asiyekomaa kimapendo kufuata njia hiyo danganyifu, tena ngumu kuachwa baada ya kuzoeleka.

Punyeto ni uteja (Addiction) kama ulivyo uteja mwingine wa vilevi kama sigara, bangi, pombe, madawa ya kulevya na kadharika.

Uteja wowote ikiwemo na uteja wa kujichua husababishwa na kumikali mbili zilizopo kwenye ubongo zijulikanazo kama ‘Dopamine’ na ‘endorphin’.

Dopamine ni transimita nyurolojia ambayo hukusaidia kujisikia raha.

Wakati endorphins ni homoni inayotolewa ukiwa una mfadhaiko wa akili (stress) na wakati unafanya kazi yoyote inayohitaji nguvu.

Endorphin pia hukusaidia wakati unaporudi kwenye hali yako ya kawaida ya utulivu baada ya misukosuko ya maisha.

Wakati unapiga punyeto mwili wako huitoa homoni hii dopamine kemikali ambayo hukufanya ujisikie raha za kimapenzi na kisha mwili huitoa tena endorphin baada ya kuwa umemaliza tendo hilo.

Kadri unavyoendelea kuwa teja wa punyeto ndivyo na ubongo wako unavyozidi kuzalisha na kuzitoa hizi homoni kwenye mwili wako.

Endorphins na dopamine ni homoni zinazohusika na kupunguza au kushusha kiwango cha stress kwenye akili yako.

Kwahiyo wale wote wanaosumbuliwa sana na stress au wenye matatizo yoyote ya kuvurugika kwa akili wanakabiliwa zaidi na hamu ya kutaka kupiga punyeto kuliko watu wengine wenye utulivu wa akili zao.

Hivyo punyeto kwa sehemu kubwa ni matokeo ya kutokuwa na namna nzuri za kushughurika na mihemko yako katika maisha.

Punyeto inakufanya wewe ulikimbie tatizo kwa muda mfupi badala ya kushughulika na tatizo uso kwa uso.

Wakati punyeto ya mara 1 au 2 kwa mwezi inaweza isilete shida yoyote kwenye afya yako, ukizidisha ina madhara makubwa kiafya kuliko hata sigara. Wapo baadhi hufanya punyeto karibu kila siku.

Shida hii miaka ya sasa ni kubwa sana kwa vijana wa miaka 15 mpaka 25 na wengi wao wanakuwa bado wapo shule na vyuoni na wengi hawajuwi kama baadaye inaweza kuwaletea madhara.

Wazazi wanawanunulia watoto wao simu janja (smartphone) ili waweze kupata masomo kirahisi mtandaoni na mawasiliano kati yao na wazazi lakini vijana hao kwa ujinga wao wanajaza picha na video za ngono na huzitazama kila mara na kama matokeo yake hujikuta watumwa wa punyeto na mwisho wa yote ni kufeli masomo yao.

Wakati mwili unatoa hizi homoni mbili mwili wako unajisikia kuwa na hisia au stimu sawa sawa na za yule aliyetumia dawa ya kulevya ijulikanayo kama ‘heroin’.

Kuacha punyeto siyo jambo rahisi kama mtu anavyoweza kukuaminisha.

Hili ni swali ninalokutana nalo karibu kila siku niwasilianapo na watu hasa wanaume.

Ni ngumu kuacha punyeto kuliko hata sigara.

Hata hivyo penye nia pana njia na hakuna lisilowezekana kama umeamua.

Inaweza kuchukua muda lakini ukiwa na malengo na afya yako mwishowe utafanikiwa kuacha.

Kama ilivyo kwa tabia zingine zozote mbaya, kuacha punyeto kunahitaji mikakati na kuepuka chochote kinachoweza kukupelekea kuwaza kujichua.

Kitu pekee kinachoharibu afya, nguvu na ubunifu kwa mwanaume ni punyeto.

Siwezi kukueleza kwa namna inayoeleweka madhara ya punyeto hata ukaamini.

Ni somo zito na wengi wanalichukulia juu juu tu.

Kama wewe ni mwanaume na unataka kuepukana na ujinga, unataka kuepukana na hali ya kukosa hamasa ya kuwa mbunifu au kufanya kazi kwa bidii basi acha punyeto.

Kuna uwezekano kuna baadhi ya watu pengine hata wataalamu kabisa wamewahi kukuambia kuwa punyeto ni ngono salama na ni jambo la kawaida na ukaamini.

Ukweli ni kuwa punyeto ni mbaya kiwango ambacho siwezi kukueleza ukaamini.

Nguvu ya mwanaume ipo kwenye mbegu zake (semen).

Kila mara mbegu zake zinapotoka nguvu zake hupungua pia.

Sasa unapofanya punyeto maana yake unapoteza nguvu bila sababu na bila uumbaji wowote kutokea tofauti na vile ungeshiriki na mwanamke.

Mara tu unapoacha kujichua utaona nguvu zako za mwili na ubongo zinaongezeka kiwango ambacho hukuwahi kufikiri.

Kama unajiona ni mnyonge, huna nguvu, mjinga au unajiona ni mpumbavu hivi mara nyingi ujuwe ni matokeo ya kuzoea kujichua.

Mwanaume aliyezoea kujichua hata kutongoza kwake huwa ni shida sana kwani amejawa na aibu zisizoelezeka na wengi wao hupenda mambo ya bahati nasibu na ya mikato mikato (shortcut).

Punyeto ikikuzoea unakuwa huna tofauti sana na teja wa madawa yoyote ya kulevya.

Hata kama huvuti sigara, huvuti bangi, hutumii dawa za kulevya au hunywi pombe kupitiliza lakini ukiwa tu ni mtumwa wa punyeto mwili wako na ubongo hauna tofauti na hao wanaoutumia hivyo vilevi kila siku.

Kila wakati unapopiga punyeto unajiuwa mwenyewe pole pole kimya kimya bila hata kujuwa.

Siri ya mafanikio kama mwanaume au kama wewe ni mwanaume na unataka kuwa mtu mwenye mafanikio kwenye maisha yako, nakuonya leo kwa upole, acha kujichua na hutakaa unisahau maishani mwako.

Kuna mambo mengi yataanza kutokea kwenye ubongo wako na kwenye mwili wako mara tu unapoanza kuacha tabia hii ya kujichua.

Uwezo wako wa kujiamini na kujitambua utaongezeka kwa haraka sana na wala hutaamini kama kumbe ni punyeto tu ndiyo ilikuwa inachelewesha maisha yako namna hiyo hata ukawa unajiona hufai, siyo mzuri, ukawa hujiamini hata kuzungumza mbele ya watu.

Soma pia hii > Madhara 21 ya punyeto kwa wanaume

Jinsi ya kuacha kujichua

Jinsi ya kuacha punyeto

1. Tafuta Daktari na uongee naye juu ya tatizo lako

Wakati unapokuwa tayari kuacha tabia yako mbaya ya kujichua hatua ya kwanza ni kumtafuta daktari na ikiwezekana uonane naye uso kwa uso siyo kwenye simu kwa msaada na maelekezo zaidi.

Usitafute msaada mtandaoni kwani unaweza kukutana na habari za kukukatisha tama au kukuhamasisha kuendelea kushiriki zaidi punyeto.

Daktari au Tabibu amefundishwa namna ya kushughulika na matatizo ya kitabia ya kiakili na namna ya kukupa mbinu nzuri za kuachana na tatizo hilo kutokana na umri wako na mazingira unayoishi.

Siyo gharama sana wapo matabibu unaweza kuonana nao bure na wengine hawachaji pesa nyingi kama unavyoweza kudhani.

2. KUWA BIZE

Akili isiyojishughulisha na lolote ni makao makuu ya shetani na kila aina ya ujinga.

Kuwa bize na kazi, mazoezi, masomo kutakusaidia kupunguza hamu yako ya kutaka kujichua kirahisi zaidi kuliko ukiwa ni mtu wa kula na kulala.

Tembelea ndugu jamaa na marafiki kila mara unapokuwa huna kazi yoyote ya kufanya. Tafuta kitu kingine tofauti na punyeto unachopenda kukifanya mara kwa mara na uwe bize na hicho.

Ukiwa bize na kazi au mazoezi ya viungo au hata masomo kutakusaidia kuichosha akili yako na mwili kwa ujumla na hivyo hutapata tena nguvu za kutaka kujichua.

Kuna namna nyingi za kukufanya uwe bize. Nenda hata shambani kulima kama huna shughuli yoyote maalumu ya kufanya.

Kuwa bize, endelea kufanya kazi, endelea na mazoezi ya viungo kila siku.

3. KUWA NA MKE AU MCHUMBA

Namna pekee nay a uhakika ya kuacha punyeto ni kuoa au kuwa na mchumba. Hii ndiyo njia pekee yenye uhakika wa asilimia 100 ya kuacha punyeto.

Tofauti na hii ni kuomba tu neema ya Mungu.

Mungu siyo mjinga hata akatuumba watu wa jinsia mbili tofauti. Ingawa bado nimekutana mara kadhaa na wanaume ambao tayari wameoa lakini bado wanajihusisha na kupiga punyeto.

Ukimuuliza inakuwaje unapiga punyeto na una mke majibu ni kuwa ameshazoea mchezo huo anashindwa kuacha!

Kwa wenzetu wazungu kuanzia shule ya msingi kijana wa kiume hata binti wa kike anaweza kuwa na mchumba na akampeleka mpaka nyumbani kwa wazazi na isilete shida yoyote.

Shida ni huku kwetu Afrika ambako kijana huruhusiwi kuwa na mchumba wala mpenzi mpaka umalize shule au chuo na siyo kumaliza tu shule labda mpaka upate kazi inayoeleweka ndiyo unaweza kuwa na mchumba na ukampeleka mpaka kwa wazazi na wasipige sana kelele.

Kwahiyo kwa vijana waliopo shule ya msingi, sekondari na hata vyuo wengi wao sababu ya maadili yetu ya kiafrika wanajikuta hawana namna zaidi ya kupiga punyeto.

Hivi karibuni tulisikia huko Kenya wabunge walitaka kupitishwa mswaada wa sheria kuruhusu vijana waweze kuanza kushiriki tendo la ndoa wakiwa na miaka 16 na siyo mpaka 18, sijajuwa wameishia wapi kama wamefanikiwa au la

Kama husomi shule au chuo na umeshakuwa mkubwa namna pekee ya kuacha punyeto ni kuoa au kuwa na mchumba karibu.

Kwa mwanaume tendo la ndoa ni moja ya mahitaji yake ya lazima kama ilivyo kwa chakula au malazi ingawa hili wengi hawajuwi na wanaweza kupinga ila ukweli unabaki pale pale mwanaume ili awe na akili yenye utulivu na iliyotulia lazima awe anashiriki tendo la ndoa na siyo kupiga punyeto.

Ni kweli mapenzi yana madhara yake hasa kama unasoma na upo bize masaa yote na mapenzi.

Mapenzi pia yanahitaji muda, nguvu na hela, kama bado hali yako kiuchumi haieleweki au huna muda wa kumhudumia mwenza wako basi tumia mbinu zingine za kuacha punyeto kwa sasa mpaka utakapokuwa tayari kwa mahusiano.

Wanaoathirika zaidi na punyeto kati ya wanawake na wanaume ni wanaume.

Hivyo wanaume tuache kuwadharau wanawake na tutambuwe bila wao sisi hatujakamilika.

4. ACHA KUTAZAMA PICHA ZA X

Kama kuna kitu kimehamasisha tabia hii ya kujichua kwa kasi sana miaka ya sasa basi kitu hicho si kingine zaidi ya picha za X.

Yaani picha hizo na punyeto ni kulwa na doto, huwezi kuvitenganisha.

Ni ngumu sana sawa sawa na haiwezekani kwamba uangalie picha za x halafu usiishie kwenda kujichua kama huna mke wala mchumba.

Hizi nazo zina uteja wake (addiction) kama ilivyo kwa punyeto yenyewe. Ukishazoea kuziangalia nazo kuziacha inahitaji neema ya Mungu.

Ni kama madawa ya kulevya hivi.

Sasa kama unataka kuacha kujichua au kupiga punyeto, hakikisha unasahau kuziangalia hizi picha kuanzia sasa.

Popote ulipozihifadhi iwe kwenye simu au kwenye computer hatua ya kwanza zifute kabisa kote zisionekane.

Kama huwa unaziangalia kwenye mtandao futa anuani ya blog au tovuti ambazo huwa unazitembelea kuangalia uchafu huo futa na historia yake kwenye browser yako ya simu au computer.

Kama upo kwenye magroup labda huko facebook au WhatsApp na kuna wenzako wanaweka picha za namna hiyo jitowe kwenye hayo magroup haraka dakika hii hii.

Ukiweza kukaa mbali na hizi picha una uwezekano wa kuacha punyeto kwa zaidi ya asilimia 98.

Tofauti na hapo sahau wewe kuacha punyeto na utaendelea kuwa mtumwa wa wa punyeto mpaka utakapokufa.

Na hizi picha za X ni mpango mkakati wa kishetani wa kukizubaisha na kukiangamiza hiki kizazi cha sasa pasipo wao kujitambua.

Picha hizi zinaharibu afya yako ya ubongo, zinasababisha wewe kuwa teja wa punyeto, zinakuletea tatizo la kukosa hamu ya tendo la ndoa, zinaharibu utu wako wa ndani na uhusiano wako na Mungu.

Baada ya njia ya kuacha punyeto ya kuwa na mke au mchumba, njia nyingine ya uhakika ya kukuwezesha wewe kuacha punyeto ni hii ya kuacha kutazama picha za X.

Huo muda unaotazama hizo picha au hizo video kwanini usiingie youtube au google ukatafuta notisi za masomo ya ujasiriamali au ubunifu wowote na ukaboresha afya yako ya akili badala ya kuharibu akili yako kwa kutazama ujinga huo wa picha za X?.

Kingine ni kuondoa chumbani kwako vifaa vyote vinavyotumika wakati wa kujichua au kupiga punyeto.

Hivi vinajulikana kama ‘sex toys’, ni kama mamidoli ambayo watu waume kwa wake wamekuwa wakiitumia wakati wa kujichua.

Uamuzi unabaki kuwa kwako.

Ikiwa unatafuta dawa ya kutibu madhara yatokanayo na punyeto, niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175

Soma pia hii > Dawa ya kuongeza nguvu za kiume

Hizi ni baadhi tu ya faida chache zitakazokutokea mwilini unapoanza kuacha punyeto:

1. Hofu zitakuisha – Wakati unapoacha uteja wa kujichua mara moja utaanza kuona uwezo wako wa kujiamini unaanza kuongezeka.

Itakuwa ngumu sana wewe kupatwa na wasiwasi au kutetemeka hata mbele ya vitu ulivyokuwa ukitishika kirahisi hapo kabla.

Kwenye hali za hatari utakuwa unaelewa matokeo ya hatari hizo lakini utakuwa na uwezo wa kushughurika nazo kwa umakini na uangalifu mkubwa mpaka unazishinda tofauti na kabla ulipokuwa mtu wa kupaniki hata kwa vitu vidogo tu

Utaanza kuona wazi nini maana hasa ya kuwa mwanaume kwenye maisha yako.

2. Macho yataongezeka uwezo wa kuona – Uwezo wa macho kuona huongezeka mara dufu mara tu unapoacha tabia hii ya kujichua.

Na siyo uwezo wa macho tu kuona ndiyo unaoongezeka bali hata uwezo wake wa uvumulivu wa kufanya kazi masaa mengi utaongezeka.

Utaona unaweza kufanya kazi kwenye computer yako au simu yako masaa mengi bila kuhisi kuchoka haraka tofauti na mwanzo ulipokuwa teja wa punyeto.

Punyeto inasababisha upofu kama ikizidi.

3. Utaanza kujisikia vizuri – Utaanza kujisikia vizuri, utaanza kujiona ni mwenye furaha. Utajiona unafaa sana pengine ukaanza hata kuwasahau na watu wengine karibu yako.

4. Uwezo wa kukukumbuka vitu utaongezeka – Utaona ni rahisi kwako kukumbuka vitu na pia utakumbuka kumbukizi za nyuma ambazo ulikuwa umezisahau siku nyingi.

Usijali sana kuhusu kukumbuka mambo ya zamani, utaanza pia kukumbuka ndoto zako ulizokuwa umejipangia maishani miaka mingi iliyopita.

Akili yako itakuwa ni nyepesi na yenye nguvu zaidi.

5. Kinga ya mwili wako itaongezeka –  Mwili wako sasa utakuwa na akiba ya kutosha ya nguvu hivyo kuwa rahisi kuyashughulikia magonjwa.

Inawezekana mwanzoni wakati unaacha kujichua kukajitokeza magonjwa au maradhi mengine kwa sababu mwili unakuwa upo bize kujitibu wenyewe lakini pole pole mwili wote utakaa sawa hivyo usivunjike moyo mapema.

6. Woga wako utaisha – Kiasi chako cha kuwa muoga kitapungua kwa asilimia kubwa sana mara uachapo kujichua.

Utaanza kujisikia vibaya kuwa mtu muoga au mwenye wasiwasi kwani utakuwa unajiona unakaribia kuwa ni mtu mkamilifu.

Hii itakupa hali ya kuona una ulinzi wa kutosha na hivyo kuweza kushughulika na hali ngumu bila kuwa na wasiwasi wowote.

7. Uelewa kuhusu vitu na watu utaongezeka – Uwezo wako wa akili utaongezeka mara dufu.

Kama ni mwanafunzi hata uwezo wako darasani unaweza kuanza kuwashangaza walimu, wazazi hata rafiki zako.

Utaanza kuvielewa vitu bila kutumia nguvu nyingi na majibu yatakuwa yanakuja kwako kirahisi zaidi kuliko wakati ule ulipokuwa teja wa punyeto.

8. Mwili utakuwa mnyumbufu – Yaani mwili wako utakuwa mwepesi, utaweza kufanya kazi au hata mazoezi muda mrefu bila kuhisi kuchoka sana.

Ni kama unavyowaona watoto na vijana wadogo miili yao ilivyo shapu sababu bado hawajaipoteza hiyo nguvu mhimu zaidi kwa mwili wa mwanaume, ndivyo mwili wako utakavyoanza kuwa.

Utaonekana ni kijana zaidi tofauti na umri wako.

9. Utulivu utakuongezeka – Utakuwa na amani na utulivu usioelezeka kirahisi rahisi.

Utakuwa na uwezo mkubwa wa asili wa kuvumilia mambo na changamoto mbalimbali maishani mwako.

10. Utajiamini zaidi  – Utakuwa hodari zaidi, aibu zako zote zitakuisha. Utakuwa na uwezo wa kuongea na yoyote, utaweza kumtongoza hata yule mdada ulihisi haiwezekani hata kusalimiana naye tu siku za huko nyuma ulipokuwa teja wa punyeto.

Faida za kuacha punyeto ni nyingi na siwezi kuandika zote hapa maana muda nao ni mali. Bali faida zingine kwa uchache ni pamoja na zifuatazo;

  • Utakuwa na nidhamu
  • Utaacha kuwa mtu wa kupaniki
  • Unaweza kuacha uteja au ulevi mwingine wowote kirahisi
  • Ngozi yako itakuwa nzuri na ya kupendeza
  • Afya yako ya uzazi itarudi
  • Utakuwa msafi
  • Utakuwa unapangilia mambo yako
  • Uwezo wako na nia zako vitaongezeka
  • Msongo wa mawazo (stress) utaisha
  • Utakuwa na mwili unaovutia
  • Utakuwa huru, mwenye afya na mwenye furaha utadhani ni mtoto
  • Uwezo wako wa kufanya kazi na kutengeneza pesa utaongezeka
  • Hutakuwa mtu aliyetawaliwa na mihemko
  • Utakuwa ni mtu wa kuaminiwa na wengine
  • Utajiheshimu

Bado utaendelea kupiga punyeto au utaamua kuacha sasa na kuwa na afya bora na mpya ya mwili na akili kuanzia leo au utaendelea kuwa teja wa kujichua?

Uamuzi unabaki kuwa kwako.

Ikiwa unatafuta dawa ya kutibu madhara yatokanayo na punyeto, niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175

Ofisi yangu inaitwa *Tumaini Herbal Life* ipo Kibugumo Mji Mwema Kigamboni Dar Es Salaam. 

SHARE post hii na wengine uwapendao

Imesomwa na watu 10,945
Jinsi ya kuacha punyeto

16 thoughts on “Jinsi ya kuacha punyeto

  1. ubarikiwe sana kwa somo zuri na lenye afya ya mwili na akili kiujumla hatuna ya kukulipa kulingana na hili fundisho lakini itoshe tu kusema Mwenyezi Mungu azidi kukubariki katka kufikiria na kuelimisha zaidi.
    Aksante sana mwana wa Adamu.

  2. thank you very much for you subjeck i think we understand you god bless you big brother

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WhatsApp 0714800175