Utafiti : wanaume maskini wana nguvu nyingi kitandani kuliko matajiri

Last Updated on 14/01/2021 by Tabibu Fadhili Paulo

UTAFITI : Wanaume maskini wana nguvu nyingi kitandani kuliko wanaume matajiri

Tofauti na watu wengi tunavyojuwa na kufahamu na kuamini kuwa watu wenye hela watakuwa na nguvu za kiume za kutosha kitandani, utafiti wa hivi karibuni unatoa majibu tofauti na wengine wengi wanavyoamini

Watu wengi hudhani mwanaume akiwa hana hela basi anakuwa mtu wa mawazo mawazo au stress nyingi kiasi cha kushindwa kuhimili tendo la ndoa, kumbe siyo kweli!!

Kinachoonekana hapa ni kuwa wanaume wengi mwanzoni wanapoanza kupata hela ni kweli huwa wanakuwa na afya nzuri na wanaweza kweli kuhimili tendo la ndoa kwa usahihi kabisa na wanakuwa na nguvu za kiume za kutosha kitandani, lakini kadri hela zao zinavyozidi kuongezeka ndivyo na wao wanavyozidi kuishiwa nguvu za kiume na kukosa hamu ya kushiriki tendo la ndoa

Utagundua sasa kumbe hela siyo kila kitu na kuwa ni mhimu sana kumuomba Mungu akupe hekima kabla ya kukupa hela

Usipokuwa na hekima hela yako mwenyewe uliyoitafuta kwa tabu usiku na mchana ukiipata inaweza kukudhuru badala ya kukupa faida na mapumziko

Zifuatazo ni sababu kuu 5 kwanini wanaume wengi matajiri hawana nguvu kitandani tofauti na wale maskini au wenye kipato cha kati

Sababu kuu 5 kwanini wanaume wengi matajiri hawana nguvu kitandani tofauti na wale maskini au wenye kipato cha kati :

  1. Ubize na kazi

Mapenzi yanahitaji nguvu, muda na hela.

Mara nyingi matajiri wengi wana hela lakini hawana nguvu wala muda.

Hawana nguvu za mwili kwa ujumla sababu muda mwingi wapo bize na kazi za kuingiza hela kwenye biashara na kazini kwao

Kumbe wanaume wengi maskini hawawajibiki kwenye kazi wala biashara yoyote hivyo wana muda mwingi wa BURE kitu ambacho wanawake wengi wanakipenda sana kwenye mahusiano pia wana nguvu nyingi sababu wanapata muda wa mazoezi na akili zimekaa BURE tu muda mwingi bila kuhangaika na chochote

  1. Stress na mawazo juu ya biashara

Stress au msongo wa mawazo ndiyo kitu namba moja kinachopunguza na kushusha nguvu za kiume kwa haraka sana

Ukiwa na mawazo mawazo kuwa na nguvu za kiume ni jambo lisilowezekana. Huwezi kuwa na stress na wakati huo huo uwe na ufanisi mzuri kitandani, haiwezekani.

Unapoanza kuwa na hela stress yako hupungua sana lakini kadri hela zinavyozidi kuongezeka ndivyo na stress inavyofumuka na kujijenga kwa upya

Hii ndiyo sababu matajiri wengi pia ndiyo hao hao walevi sana na wengi wao hutumia pia madawa mabaya ya kulevya

Ili kuhakikisha hela haipungui na kuwa inazidi kuongezeka, matajiri wengi hujikuta katikati ya majaribu na mambo mengi yanayosababisha stress na mawazo mawazo kuongezeka

Kupata hela siyo kazi ngumu kabisa kama watu wengi wanavyoamini, kilicho kigumu ni kuitunza hela, kuifanya iongezeke na kuilinda

Katika mambo yote hayo ukilinganisha na mazingira ya biashara yasiyotabirika, mambo ya kodi, mambo yanayohusu ushindani katika biashara huwalazimisha matajiri wengi kuingia kwenye mazingira ya kuishi kwa wasiwasi, kukosa usingizi, kufanya kazi muda mrefu na kupita kiasi nk

Tajiri kwa kawaida hata kutembea peke yake kwa uhuru mitaani hawezi, muda mwingi anahisi atakabwa au kujeruhiwa na watu anaohisi wanamuonea wivu kwa mali zake nk

Kumbe kwa wenzangu wanaume maskini au wenye kipato cha kati hawana shida hizi zote. Hawana biashara kubwa na wanaishi kwa furaha na muda mwingi utawaona wapo bize kuangalia na kufuatilia mpira kwenye TV

  1. Nguvu ya hela

Hela ni aina mojawapo ya nguvu ila siyo nguvu za kiume

Tajiri sababu ya nguvu ya hela yake anaweza kumpata mwanamke yoyote wakati wowote

Simu moja tu ya tajiri mwanamke ameshafika mahali alipo boss

Kwa sababu hiyo wanaume wengi matajiri hawana muda wa kuwa bize wakati wa tendo la ndoa ili kumfikisha mkewe kileleni

Hana shida hana uhaba wa wanawake na mbaya zaidi kuna orodha ndefu ya wanawake kwenye foleni ya wanaomtaka wengine wanamtongoza kabisa!

Ukiwa maskini nani atakutafuta? Nani atakutaka? Mwanamke gani atajitoa ufahamu kukutongoza mwanaume maskini?

Hakuna

Kwa sababu kama hii matajiri wengi hawana hata heshima kwa wake zao, hawawaogopi, hawanyenyekei na kuwa wapole kwa wake zao

Matajiri wengi wasio na hekima anaweza kufanya umalaya ndani ya mtaa huo huo mmoja anaoishi, anaweza kutembea na wanawake kadhaa hadi mke wake akaona lakini yeye hashtuki anaona ni jambo la kawaida sababu tu ana hela

  1. Kutokujua jinsi ya kupata furaha kupitia hela

Watu wengi wanaamini ukiwa na hela tayari unakuwa na furaha

Baadhi ya watu hudhani hela inaleta furaha

Tumeaminishwa hivyo na tukaamini hivyo

Ukweli ni kuwa hela ni kitu cha mhimu sana hakuna mtu asiyejuwa hilo, Isipokuwa tu hela siyo kila kitu

Money is important, but isn’t everything

Unapoanzaanza kupata hela utaona furaha, utajisikia vizuri na afya yako inaweza kuimarika

Kadri hela zinavyozidi kuongezeka ndivyo na furaha yako kuhusu hela inatoweka pole pole

Badala ya furaha sasa ni huzuni

Muda mwingi upo kazini, uchovu mwingi, majukumu mengi, upo bize sana kiasi unaweza kusahau kula chakula

Sasa ili upate furaha ukiwa na hela ni lazima hela hizo zikusaidie kuokoa muda na siyo kupoteza muda.

Matajiri wenye akili na wenye hekima huwa hawafanyi kazi ili kupata hela, bali wanazituma hela zao kwenda kuleta hela nyingine nyingi huku yeye tajiri akiwa amelala kabisa au yupo bize kucheza na watoto wake au yupo mbuga fulani ya wanyama na familia yake wanatalii

The rich don’t work for money

Kama wewe kila siku kuanzia jumatatu mpaka jumapili lazima uamke kwenda kazini au kwenye biashara yako ndiyo uingize hela hata kama unaingiza milioni moja kwa siku wewe bado ni maskini ila hujitambui

Matajiri wasiojitambua wapo bize masaa 24 na kazi ili kuendelea kulinda hela na mali zao

Kwa kutokutambua namna gani ya kupata furaha kupitia hela matajiri wengi wameingia matatani kwenye maisha yao ya ndoa

Wengi walilazimika kutoa au kupewa talaka kama matokeo ya kutumia muda mwingi kutafuta hela badala ya kuwa bize na familia na marafiki

  1. Vitambi

Matajiri wengi wanakula hovyo

Mwingine sababu tu ana hela basi kila siku anakula nyama, kila siku anakunywa pombe, anakula machipsi na mavyakula mengi ya hovyo ya kwenye masupamaketi na maduka mengine ya kifahari

Walapo vyakula kama hivyo sababu wana hela na kusahau kula mboga za majani na ugali wa dona matajiri wengi wamelazimika kuwa na vitambi

Kwa sababu muda mwingi wanakuwa wamekaa kwenye viti huko makazini na kwenye maofisi yao inakuwa ni rahisi kwao kupata vitambi

Ndiyo, kama muda mwingi katika siku unautumia ukiwa umekaa tu chini au kwenye kiti ni rahisi sana wewe kupata tatizo la kitambi

Ukiwa na kitambi ni vigumu wewe kuwa na nguvu za kiume

Maskini wengi ni vigumu sana kupatwa na kitambi

Matajiri wengi pia wanasumbuliwa na magonjwa mengine kama ya shinikizo la juu la damu (BP), kisukari, uzito kupita kiasi na kolesto

Kitambi na magonjwa hayo mengine ni sababu nyingine inayowafanya matajiri wengi kutokuwa na nguvu za kiume za kutosha kitandani tofauti na wale maskini au wenye kipato cha kati

Naitwa Fadhili Paulo, ni Tabibu wa tiba asili na ni mtanzania, WhatsApp Napatikana kwa namba hii +255714800175

Pia kama unatafuta dawa ya asili kwa ajili ya kuimarisha nguvu za kiume na kutibu madhara yatokanayo na punyeto niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175

Tafadhali SHARE kwa ajili ya wengine uwapendao

Imesomwa na watu 295
Utafiti : wanaume maskini wana nguvu nyingi kitandani kuliko matajiri

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WhatsApp 0714800175