Last Updated on 17/01/2024 by Tabibu Fadhili Paulo
Mwanamke akikupenda sana anaweza kuchepuka
Mkeo akikupenda SANA anaweza kuchepuka!!!
Huenda ulikuwa bado hujuwi kuhusu hili lakini moja kati ya sababu nyingi zinazoweza kumshawishi mkeo achepuke inaweza kuwa ametokea kukupenda sana kupita kiasi.
Hiyo ni ngumu kuielewa lakini nitajaribu kukusaidia uweze kuelewa kwanini hilo linaweza kutokea.
Kinachotokea ni kitu ambacho kwa lugha ya kiingereza hujulikana kama ‘BACKUP’.
Backup (bakiapu) ni kama kopi ya kitu kingine.
Ni kuwa na mbadala wa kitu kingine endapo kwa bahati mbaya kile ulichonacho sasa kitapotea.
Inaweza kuwa ni kitu kingine au kitu kile kile kama ulichonacho sasa.
Unaepuka hasara mapema.
Una biashara ya kuuza vitunguu swaumu kwa mfano na wakati huo huo una biashara nyingine pembeni ya kuuza nguo.
Unajipa moyo kwamba endapo hii biashara ya vitunguu swaumu itazingua au itashuka soko lake au msimu fulani unaona wazi havina wateja, basi unawekeza kwenye kuuza nguo ili kufidia kipato chako kinachoweza kupotea wakati soko la vitunguu swaumu linasumbua.
Au kama una data (mafaili) labda kwenye mtandao, kwenye computer au kwenye simu na unataka data hizo zisikupotee kirahisi unafanya backup sehemu nyingine labda kwenye flash, au kwenye memory card au sehemu nyingine huko huko mtandaoni kwamba zikipotea zile data orijino basi unazo nyingine pembeni unazoweza kuzirudishia na ukaendelea na kazi.
Usiache pia kusoma na hii
Madhara 10 ya kupiga punyeto kwa wanawake
Kama unataka kutunza chat zako za WhatsApp kwa mfano unabonyeza vile vidoti vitatu vya kushuka pembeni juu kulia, kisha unabonyeza settings, kisha chats, kisha shuka chini bonyeza chat backup na backkup itaanza hiyo shughuli ambapo itatunza data zako kwenye internal memory pia kwenye cloud based google drive storage.
Sasa ikitokea ukaibiwa simu kwa bahati mbaya, au simu imekufa ghafla, basi unanunua tu simu nyingine unaingiza email yako ya gmail kwenye hiyo simu utaingia playstore utafunga WhatsApp kisha fanya restoration na chat zako zote zitarudi tena kama mwanzo neno hadi neno, picha hadi picha na mengine yote kulingana na settings zako wakati unafanya backup WhatsApp yako ikiendelea kutumika kila siku.
Unakuwa hujapoteza kitu na maisha yanaendelea.
Kwa hiyo na mwanamke akikupenda sana anapatwa na mawazo kwamba ikitokea lolote la kutokea na ukamuacha anaweza kuumia sana kwenye maisha yake.
Anaona kama vile dunia yote itakuwa imeisha.
Anaona itakuwa ngumu sana kuendelea na shughuli zake za kila siku endapo tu utatokea ukamuacha.
Ili kujikinga na hayo yote basi anaamua kujiandaa mapema kwa kujiwekea bega mapema la kuegemea endapo ndoa yenu itavunjika au litatokea lolote la kutokea na ukamuacha.
Anakuwa na backup yake pembeni mapema.
Anaamua kuchepuka na kuwa na mwanaume mwingine kama ulinzi tu wa moyo wake pindi wewe mmewe wa sasa akupendaye sana na ametokea kukufia utakapoamua kumuacha au kumtelekeza kwa sababu nyingine nyingi zilizo nje ya uwezo wake.
Umeona?
Siyo kila mara mkeo akichepuka maana yake hakupendi kama wanavyoamini wanaume wengi.
Kuna wakati mwingine mwanamke anaweza kuchepuka ili kuilinda ndoa yenu.
Kumbuka sababu za mwanamke kuchepuka ni nyingi na hakuna namna wewe kama mwanaume unaweza kufanya ili kumzuia mkeo asichepuke.
Haijalishi wewe mwanaume ni nani na una nini.
Mkeo akiamua kuchepuka atachepuka tu, huwezi kumzuia.
Kuna vitu unaweza kufanya kama mme ili kuzuia uwezekano wa mkeo kuchepuka na vinaweza kusaidia hilo, lakini mwisho wa siku ni uamuzi wake BINAFSI yeye mwenyewe mkeo kuamua kwamba hataki kuchepuka kwa sababu yoyote ili kukuheshimu wewe na ndoa yenu.
Ushauri : Mwanamke uliyepo kwenye ndoa tulia na mmeo.
Jambo mhimu kwenye mahusiano ni kupenda na siyo kupendwa.
Kama tayari moyo wako umemfia huyo mmeo basi mwambie tu ukweli juu ya hilo na umweleze wazi kwamba siku akikuacha utapata tabu sana lakini utakuwa tayari kwa lolote na utamuachia Mungu NA KURUHUSU MAISHA MENGINE YAENDELEE LAKINI haupo tayari kuchepuka ili tu kujiweka tayari kwa maumivu ya kuachwa.
Subiri kwanza mpaka uachwe ndiyo uendelee na mipango mingine.
Wakati mwingine ni hofu yako tu na wasiwasi wako kichwani kwani mmeo huenda hana wazo lolote la kukuacha kwa sasa au hata baadaye.
Jiamini na ujikubali.
Amini baada ya hili, au baada ya hiki kutakuwa na kingine na maisha yataendelea.
Lakini usijipe presha sasa isiyo na sababu na inayoweza kuhatarisha zaidi maisha yako.
Share post hii na RAFIKI zako wengine kwenye Twitter ?
Mwanamke akikupenda sana anaweza kuchepuka Share on XMHIMU SANA : Ukiwa na swali lingine lolote kuhusu makala hii uliza hapa hapa chini kwenye sanduku la comment na utajibiwa tena hapa hapa BURE.