Faida 15 za kushiriki tendo la ndoa mara kwa mara

faida za kushiriki tendo la ndoa

Last Updated on 24/10/2021 by Tabibu Fadhili Paulo

Faida 15 za kushiriki tendo la ndoa mara kwa mara

Utafiti mmoja wa mwaka 2015 ulihitimisha kwamba kushiriki tendo la ndoa mara kwa mara kuna uhusiano mkubwa na wa moja kwa moja wa ubora wa afya yako na maisha yako kwa ujumla.

Kuridhika katika mahusiano kunaweza kuongezeka sana kutokana na watu waliopo kwenye mahusiano kushiriki tendo la ndoa.

Kadri tendo bora la ndoa linavyokosekana baina ya wanandoa wawili ndivyo kiwango chao cha kuridhika kwenye uhusiano huo kinavyopungua pia.

Kwa sababu ya kuongezeka kwa shughuli za kimaisha na ubize sana kwenye maisha yetu kumekuwa na kupungua kwa kushiriki tendo la ndoa.

Mpaka mwaka 2010 idadi ya kushiriki tendo la ndoa imepungua mara 9 zaidi ukilinganisha na ilivyokuwa mwaka 1990.

Tunaposema kushiriki tendo la ndoa mara kwa mara tunamaanisha walau mara 1 kwa wiki.

Kadri unavyozidi kuwa mtu mzima ndivyo na uwezo wako wa kushiriki tendo la ndoa mara kwa mara unavyopungua.

Kwa kawaida ukiwa na miaka kati ya 20 mpaka 40 unaweza kushiriki tendo la ndoa mpaka mara 80 kwa mwaka.

Ukiwa na miaka 40 mpaka miaka 59 unaweza kushiriki tendo la ndoa mpaka mara 54 kwa mwaka.

Wakati ukiwa na miaka 60 na kuendelea unaweza kushiriki tendo la ndoa mpaka mara 20 kwa mwaka.

Ingawa idadi ya kushiriki tendo la ndoa inapungua kadri unavyozidi kuwa mtu mzima bado tendo la ndoa linabaki kuwa ni kitu mhimu hata kwa watu wazima na wazee.

Kuna faida nyingi za kisaikolojia na za kimaumbile zinazopatikana kwa kushiriki tendo la ndoa mara kwa mara.

Tendo la ndoa mara nyingi lina uhusiano wa karibu na maisha mazuri na yenye furaha.

Ndiyo, ukweli ni kuwa huwezi kuwa na furaha 100 kwa 100 kama hushiriki tendo la ndoa na hasa kama huna sababu zozote za msingi za kiafya zinazokuzuia kushiriki.

Soma hii pia > Madhara 10 ya punyeto kwa wanawake

Faida 15 za kushiriki tendo la ndoa mara kwa mara:

1. Huongeza hali ya kujiamini

Kushiriki tendo la ndoa mara kwa mara kunaweza kukusaidia kukuongezea hali na uwezo wako binafsi wa kujiamini.

Tendo la ndoa la mara kwa mara husaidia kukuondolea hali ya kuwa na wasiwasi na woga usio na sababu na hivyo kusaidia mtu kuongeza hali ya kujipenda zaidi.

2. Huongeza hali ya kuwa na furaha zaidi

Kwa mjibu wa utafiti uliofanywa nchini China mwaka 2015 ilihitimishwa kwamba kuna uhusiano wa karibu wa kiasi cha furaha alichonacho mtu na kushiriki kwake tendo la ndoa.

Tendo la ndoa ni moja kati ya vitu vinavyoweza kukusaidia kuongeza furaha yako.

3. Huongeza ukaribu na ushirikiano

Kuna kemikali mbili za ubongo hutolewa wakati wa kushiriki tendo la ndoa ambazo husaidia kuongeza ukaribu na ushirikiano baina ya watu wawili.

Endorphin ni kemikali inayotolewa na ubongo wakati wa tendo la ndoa na husaidia kupunguza msongo wa mawazo na maumivu au kujisikia vibaya.

Wakati kemikali au homoni nyingine ijulikanayo kama ‘oxytocin’ ambayo huongezeka kwa kuzichezea chuchu za mwanamke yenyewe husaidia kuongeza katika mwili hali ya utulivu, furaha na kuridhika.

Tendo la ndoa husaidia sana kuongeza ukaribu na ushirikiano.

3. Huondoa msongo wa mawazo (stress)

Msongo sugu wa mawazo (stress) unaweza kutokea kama matokeo ya kutoshiriki tendo la ndoa mara kwa mara.

Hata hivyo kushiriki tendo la ndoa mara kwa mara kunaweza kuwa ni mbinu rahisi ya kushughulikia tatizo lako la msongo wa mawazo.

Tendo la ndoa husaidia kuzidhibiti na kuzituliza homoni zinazoleta msongo wa mawazo ambazo ni ‘cortisol’ na ‘adrenaline’.

Ukishiriki leo tendo la ndoa kuna uwezekano wa kuzituliza homoni hizo zisilete mawazo mawazo kichwani kwa siku nzima inayofuata.

5. Uhakika wa kupata usingizi mzuri

Hakuna kitu cha mhimu kwenye afya ya binadamu kama usingizi.

Hakuna.

Yaani siwezi nikakueleza ni namna gani usingizi ulivyo ni wa mhimu kwa afya bora na ukanielewa.

Hata ule vizuri vipi, hata uwe na nini kama hupati usingizi mzuri na wa kutosha kila siku ni vigumu wewe kuwa na afya bora.

Lakini ni jambo linalojulikana wazi na watu wote kwamba tendo la ndoa husaidia sana kuleta usingizi mzuri.

6. Husaidia kuongeza kinga ya mwili

Ndiyo tendo la ndoa ni moja ya vitu mhimu katika kuongeza na kuimarisha kinga ya mwili.

Kama ulikuwa hujuwi hili sasa umejuwa.

Tendo la ndoa husaidia kukupa usingizi mzuri na usingizi mzuri ni mhimu sana linapokuja suala la ubora wa kinga yako ya mwili.

Kinga yako ya mwili haiwezi kufanya kazi zake vizuri kama hupati usingizi mzuri na wa kutosha.

Kinga yako ya mwili haiwezi kufanya kazi zake vizuri kama muda wote upo peke yako mpweke na mwenye huzuni huzuni.

Kushiriki tendo la ndoa mara kwa mara husaidia kukukinga na homa za mara kwa mara, aleji na mafua.

7. Husaidia kudhibiti baadhi ya magonjwa

Tendo la ndoa ni aina mojawapo ya mazoezi.

Hivyo basi magonjwa kama shinikizo la juu la damu, shambulio la moyo, kolesto, magonjwa kwenye mfumo wa upumuaji na yale yanayohusiana na matatizo ya akili yanaweza kudhibitiwa kwa kushiriki tu tendo la ndoa mara kwa mara.

8. Huongeza uwezo wa ubongo

Baadhi ya tafiti kwa wanyama zimethibitisha pasipo na shaka kwamba kushiriki tendo la ndoa mara kwa mara kuna uhusiano na kuwa na akili nzuri na yenye utulivu.

Tendo la ndoa linasemwa ni moja ya vitu vinavyosaidia kuzalishwa kwa seli mpya ndani ya ubongo.

Hata kwa binadamu tafiti baada ya tafiti zimehitimisha kuwa tendo la ndoa (siyo punyeto au kujichua) husaidia kuongeza uwezo wa ubongo kufanya kazi.

Utafiti mmoja wa mwaka 2018 ulihitimisha kuwa tendo la ndoa husaidia kuongeza uwezo wa ubongo kutunza kumbukumbu kwa watu wazima hata wenye miaka 50 na kuendelea.

Soma hii pia > Jinsi ya kuacha punyeto

9. Husaidia kupunguza maumivu mbalimbali mwilini

Kemikali iitwayo ‘endorphin’ ambayo mwili huitoa wakati wa tendo la ndoa husaidia kukuletea hali ya utulivu na kujisikia vizuri.

Kemikali hiyo hiyo husaidia pia kupunguza maumivu ya kichwa na maumivu ya mgongo.

Tendo la ndoa husaida pia kupunguza maumivu kwa wanawake wakati wa siku zao za hedhi.

Mwanamke anayeshiriki tendo la ndoa mara kwa mara na akawa anafikishwa vizuri kileleni mara nyingi hata wakati wake wa hedhi huwa hasikii maumivu yoyote makali.

Kushiriki tendo la ndoa mara kwa mara humsaidia pia mwanamke kuwa na uke mzuri, humsaidia kuondokana na tatizo la uke mkavu na humuongezea hamu zaidi ya kutaka kushiriki zaidi tendo la ndoa siku zingine.

Pia mwanamke mjamzito anayeshiriki tendo la ndoa mara kwa mara na akawa anafikishwa kileleni humsaidia kujifungua salama na kumuondolea hatari ya kujifungua kwa upasuaji.

Tendo la ndoa husaidia kuondoa harufu mbaya mdomoni, huongeza afya ya meno, husaidia mmeng’enyo mzuri wa chakula na husaidia pia kukupa ngozi nzuri na isiyoonyesha kuzeeka.

Tendo la ndoa hasa la asubuhi linaleta ngozi nzuri na nyororo.

Kama wewe ni mwanamke na unaishiwa au huna kabisa hamu au hisia za kutaka kushiriki tendo la ndoa niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175 ninayo dawa nzuri sana ya asili kwa ajili yako.

10. Husaidia kupunguza uzito

Tendo la ndoa ni aina mojawapo ya mazoezi.

Ukiwa bize na tendo la ndoa kwa dakika 20 au 30 unaweza kuchoma mpaka gram 200 za mafuta mwilini na hivyo kukusaidia kupungua uzito.

Vile vile tendo la ndoa husaidia kupunguza hali ya kusikia njaa na hali ya kupenda kula mara kwa mara na hivyo kukuwezesha wewe kuwa na uzito sahihi.

11. Husaidia kudhibiti saratani ya tezidume

Saratani ya tezidume imefahamika na kugundulika kuwa inawapata zaidi wanaume ambao hawashiriki tendo la ndoa mara kwa mara.

Kushiriki tendo la ndoa mara kwa mara mpaka mara 21 kwa mwezi kunaweza kukusaidia kukukinga na saratani ya tezidume baadaye uzeeni.

Saratani ya tezidume ni ugonjwa wa pili kwa kusababisha vifo vitokanavyo na saratani kwa wanaume wengi watu wazima kuanzia miaka 50 na kuendelea.

Kuna aina nyingi za saratani zaidi ya 100 lakini saratani ya tezidume ndiyo ya pili kwa kusababisha vifo kwa wanaume kati ya hizo saratani zingine zote zaidi ya 100.

Kwa leo nimekuandikia hizo faida 11 siku nyingine tena nikipata muda nitakuongezea faida nyingine 4 zaidi.

Hata hivyo siyo kushiriki tu kama kushiriki tendo la ndoa ndiyo kutakupa faida hizi, ni lazima kuwepo na maelewano, masikilizano na hisia baina yako na mwenza wako.

Ni lazima liwe ni tendo bora la ndoa siyo tendo kama tendo tu.

Wote wawili lazima hisia zenu ziwepo hapo siyo mmoja anawaza tendo la ndoa na mwingine anawaza madeni yake ya VICOBA hapo ni vigumu kupata hizi faida.

Mawasiliano na maelewano baina yenu wawili ni mhimu sana ili kuwa na afya nzuri ya kitandani na kuwa na tendo bora la ndoa.

Mara nyingi wanandoa wanaoishi kama mtu na rafiki yake ndiyo wanao uwezo wa kuwa na afya nzuri ya kitandani na kuwa na tendo bora la ndoa.

Ugomvi wa mara kwa mara, hasira zisizoisha na kukosekana kwa maelewano ni moja ya vitu vitakavyokuzuia kuwa na tendo bora la ndoa kati yako na mwenza wako.

Kama wewe ni mwanaume na unatafuta dawa ya asili ya uhakika na isiyo na madhara ya kuimarisha nguvu za kiume na kutibu madhara yatokanayo na punyeto niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175

Share makala hii na wengine uwapendao.

Faida 15 za kushiriki tendo la ndoa mara kwa mara Share on X
Imesomwa na watu 1,798
Faida 15 za kushiriki tendo la ndoa mara kwa mara

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WhatsApp 0714800175