Last Updated on 19/01/2022 by Tabibu Fadhili Paulo
Dawa ya kuacha punyeto
Bila shaka umzima na unaendelea vizuri na mwaka mpya.
Kwa sababu hii ni makala yangu ya kwanza tangu mwaka huu uanze basi napenda kutumia nafasi hii kumshukuru Mungu kwa kutuwezesha kuvuka salama na kuuona mwaka mwingine wa 2022.
Napenda kukutia moyo na kukuombea yale yote uliyopanga kuyafanya mwaka uliopita 2021 na hayakuwezekana basi mwaka huu usipite bure Mungu akutendee muujiza na ukafanikiwe katika yote.
Kidunia huu ni mwaka wa 6 na tunapata kujua hivyo kwa kujumlisha namba zote zinaounda mwaka yaani 2+0+2+2 = 6
Hivyo huu ni mwaka wa sita kidunia (6th universal year) na ni mwaka ambao unasisitiza vitu au shughuli zifuatazo ambazo ni;
*Kupalilia
*Kukaa nyumbani
*Kujali wengine na
*Kujipenda mwenyewe
Hayo ndiyo mambo manne mhimu ya kuzingatia kwa mwaka huu 2022.
Katika hayo yote manne, Kujipenda mwenyewe ndiyo linatakiwa liwe jambo lako la kwanza la mhimu kuliko yote.
Mwaka huu 2022 kama hutachukua hatua Kujipenda mwenyewe basi mambo mengi utakayohangaika nayo hayatafanikiwa kamwe.
Huu ni mwaka wa 6 kidunia kwa watu wote, kama utahitaji kufahamu sasa ni mwaka wa ngapi kwako binafsi yaani huu ni mwaka wako wa ngapi kwako binafsi na ni vitu gani vingine mhimu utatakiwa uzingatie basi usione tabu kunitafuta WhatsApp kwa namba +255714800175 na mimi nitakusaidia hilo kwa gharama ya shilingi 55000 tu.
Dawa ya kuacha punyeto
Turudi kwenye jambo letu la leo sasa ambalo ni dawa ya kuacha punyeto!
Awali ya yote nikiri hadharani kwamba punyeto ni tatizo kubwa kwa sasa na ni jambo linaloleta mashaka juu ya mstakabali wa afya ya vijana wa kizazi hiki wote wa kiume na wa kike.
Kwa kifupi tu niseme kwa sasa hali siyo nzuri hasa tangu kushamiri kwa matumizi ya simujanja (smartphone) miongoni mwa wanafunzi na vijana.
Badala ya kutumia simu hizo kutafuta masomo mtandaoni vijana wanazitumia kuangalia picha mbaya za wakubwa na matokeo yake wamekuwa ni mateja wa kupiga punyeto na kuacha inakuwa ngumu sana kwao.
Kwa sababu hiyo nimekuwa nikikutana na watu mara kadhaa huko kwenye WhatsApp wakiniulizia juu ya dawa ya kuacha punyeto.
Lakini mimi mara nyingi nimekuwa nikiwajibu kwa kuwauliza swali lingine ambalo ni ‘Je Umewahi kuona mahali popote nimeandika nauza dawa ya kuacha punyeto’?
Huwa wanachukia nikiwajibu hivyo.
Hivi karibuni tu baba mmoja mtu mzima kabisa alinitafuta kwenye WhatsApp anatafuta dawa ya kuacha punyeto kwa mwanamke ambaye anadai ni rafiki yake walisoma pamoja lakini ana tatizo hilo kubwa la kujichua.
Ndiyo, kama ulikuwa hujuwi wadada na wamama nao wanajichua tena sana tu tofauti na ulivyokuwa unadhani sema tu madhara yake kwao hayajionyeshi kwa haraka na wazi kama ilivyo kwa wanaume.
Basi mimi nilimjibu hivyo hivyo tena huyo baba kwamba Umewahi kuona mahali popote nimeandika nina dawa ya kuacha punyeto kwa mwanamke?
Basi akakasirika kwanini nimemjibu hivyo akaamua kuni-block mazima kwenye WhatsApp, mimi nikajinyamazia kimya.
Ukweli ni kwamba HAKUNA DAWA YA KUACHA PUNYETO.
HAKUNA DAWA YA KUACHA KUJICHUA.
Kuna mbinu tu na maarifa juu ya namna ya kuacha punyeto lakini hakuna dawa ya kuacha punyeto.
Ni wewe mwenyewe ndiyo unatakiwa uamue kwamba kuanzia leo punyeto basi.
Ni wewe mwenyewe unatakiwa uichukie hiyo tabia na kuchukuwa hatua.
Kama kuna mtu yoyote anakuambia anayo dawa ya kuacha punyeto huyo ni muongo mkubwa.
Punyeto ni starehe, ni sawa na kilevi na inaweza kukuletea utegemezi yaani ukawa teja wa punyeto kama walivyo mateja wa madawa ya kulevya pasipo wewe mwenyewe kujijua kwamba umeshakuwa teja.
Uamuzi ni wako
Mimi ninayo dawa nzuri sana ya asili kwa ajili ya kuimarisha nguvu za kiume na kutibu madhara yatokanayo na punyeto lakini siyo ya kuacha punyeto.
Pamoja na kwamba naweza kukupa dawa ya kutibu madhara yatokanayo na punyeto na kuimarisha nguvu zako za kiume bado utatakiwa uache punyeto haraka ili dawa iweze kukutibu na kukupa mabadiliko mazuri yanayodumu kwa muda mrefu.
Kama nakupa dawa ya kutibu madhara yatokanayo na punyeto na bado unaendelea kujichua hiyo ni kazi bure na hutakaa upone.
Nimeshaandika mara nyingi hapa kuhusu madhara ya punyeto kwa wote mwanaume na mwanamke kama hujawahi kuziona hizo post unaweza kuuliza hapo kwenye boksi la comment na mimi nitakupa link uzisome.
Nakutakia mwaka mpya mwema wenye baraka, amani, afya njema na mafanikio tele.
SHARE POST HII NA RAFIKI ZAKO WENGINE
Nitumie link boss
Sawa, nakutumia
nitumie link