Last Updated on 06/07/2022 by Tabibu Fadhili Paulo
Makosa mengine matatu wafanyayo wanaume kitandani
Kumekuwa na dhana nyingi hasa ambazo ni potofu kuhusu tendo la ndoa.
Kumekuwa na mijadala mingi isiyo na mwisho kuhusu hili na wanaume wengi wanaonyesha hawana ufahamu juu ya wanawake juu ya nini hasa wanapenda au hawapendi linapokuja suala la tendo la ndoa.
Na wanaume wengi wanaishia kuchanganyikiwa juu ya nini hasa cha kufanya ili kuwaridhisha wake zao.
Na ukweli ni kuwa zaidi ya asilimia 75 ya wanawake kwenye ndoa wanaishi kwa kuvumilia tu hasa linapokuja hitaji lao la kitandani.
Maelfu ya wanawake hawajawahi kufikishwa kileleni na hata hawajuwi kufika kileleni ndiyo kupoje kupoje hasa lakini bado wanavumilia kuishi na wanaume hao miaka na miaka na kwa bahati mbaya wanalazimika kubaki kimya bila kusema lolote ili tu wasije kuonekana ni Malaya au wana tabia mbaya.
Makosa matatu wanayofanya wanaume kitandani :
1. Kudhani kwamba wanawake hawapendi tendo la ndoa
Hili ndilo kosa namba 1 wanaume wengi wanafanya kwenye ndoa zao bila kufahamu.
Wanaume wengi wanafikiri wanawake hawana hisia za kimapenzi au za kutaka kushiriki tendo la ndoa.
Ndiyo sababu inapotokea mwanamke akamtongoza au kumtaka mwanaume basi wanaume wengi hushikwa na mshangao na kuanza kumuwazia mabaya mwanamke huyo ikiwemo kumuita ni mwanamke malaya!
Sikia nikuambie mwanaume mwenzangu, wanawake nao wanapenda kushiriki tendo la ndoa mara nyingi kama vile wanaume tulivyo.
Wanawake wengi wana hisia kali za kimapenzi au hata za kushiriki tendo la ndoa kama tulivyo sisi wanaume.
Shida moja ni kuwa utamaduni na desturi za kiafrika ndizo zinamfanya mwanamke kuwa muoga kukuonyesha hizo hisia waziwazi kwa kuogopa huenda utamchukulia ndivyo sivyo.
Kwahiyo kama mke wako anaonekana anakupangia ratiba kitandani na haonekani kukukumbusha kwamba anahitaji kushiriki tendo la ndoa na wewe tambua kutakuwa na shida nyingine na pengine chanzo cha hiyo shida ni wewe mwenyewe mwanaume.
Wanawake wengi wanapenda kushiriki tendo la ndoa lakini hawapendi tendo la ndoa ambalo ni baya.
Hata hivyo kama ilivyo kwa wanaume, wapo pia wanawake wachache kwa asili hawapendi kushiriki tendo la ndoa mara kwa mara na wanaweza kukaa miezi 6 au hata mwaka bila kushiriki tendo la ndoa na bado akawa anajisikia vizuri bila shida yoyote.
Hao ni asilimia 1 kati ya 100 ya wanawake wote na mara nyingi huwa hawaoelewi na hata wakiolewa huwa hawadumu kwenye ndoa kwa sababu wanaume wengi hawawezi kuvumilia kuishi na mwanamke wa namna hiyo.
Wapo pia wanaume wachache wasiopenda tendo la ndoa, hawana habari ya kuoa wala kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi.
Lakini kwa ujumla wanawake wengi wanapenda sana kushiriki tendo la ndoa mara kwa mara kama tulivyo wanaume.
Kama mwanaume ulikuwa unadhani wanawake hawapendi sarakasi za kitandani badili mtizamo wako kuanzia sasa.
Ni mila, desturi na tamaduni ndiyo zinawazuia kueleza hisia zao waziwazi kwetu.
2. Kutumia muda mchache sana kumuandaa kabla ya tendo lenyewe.
Kosa lingine wanaume wanafanya kitandani ni kutotumia muda mwingi na wa kutosha kumuandaa mke kisaikolojia na kimwili kwa ajili ya kuwa tayari kwa tendo la ndoa.
Mwanamke anahitaji maandalizi kwa ajili ya mechi masaa 24 siku 7 za wiki (twenty four seven).
Kila unachoongea naye au kufanya naye muda wote kiwe kinamuandaa kwa namna moja au nyingine kuweka saikolojia na mwili wake tayari kwa mechi
Mwanamke anahitaji maandalizi ya kutosha kwa kiingereza wanaita ‘fore play‘ ya muda mrefu siyo nusu saa au dakika 10.
Najua kuna mtu hapa anasema kwamba huo muda utatoka wapi kwa maana anawaza pengine atakosa hata muda wa kufanya kazi zingine za kumwingizia kipato!
HAPANA, haipo hivyo.
Sina maana uache kazi zako zote kutwa nzima ubaki unatizamana na mkeo ili kumuandaa.
Hata ukiwa kazini unaweza kumpigia simu kwa dakika 2, unaweza kumtumia sms ya kawaida, unaweza kumtumia video kwenye WhatsApp na kadharika na kadharika.
Mhimu ni kuwa maongezi yenu na majadiliano yenu mengi yawe yanamuandaa tayari kwa kushiriki tendo la ndoa.
Hata mnapokuwa tayari wawili kitandani tumia muda mwingi kuongea naye na kumshikashika huko na huko ili kumwamsha kwa muda mrefu labda dakika 40 ndiyo umwingie tayari kwa tendo.
Kuna baadhi ya wanaume lugha yenu, matamshi yenu, matendo yenu, tabia zenu, sauti zenu vyote kwa pamoja ni kama vinamkimbiza au kumuondolea hamu mwanamke ya kutaka kushiriki na wewe.
Tubadilike kwenye kipengele hiki na tutumie muda mwingi sana na wa kutosha kwenye maandalizi.
Kama mkeo amechoka na ana uchovu mwingi sababu ya kazi za kutwa nzima basi mwandalie maji ya moto ya kuoga na umuogeshe, pikia watoto chakula na uhakikishe wamelala salama, hapo hutasikia tena kauli toka kwa mkeo kwamba amechoka au hajisikii.
Kuwa karibu na kumsikiliza mkeo ni dawa rahisi ya bure ya kumpa mkuyati wa kukuhitaji kitandani mara nyingi tena na tena.
Kuwa mpenzi wake, rafiki yako wa karibu na utaona atakavyokuwa na ushirikiano mzuri kwako muwapo uwanjani.
3. Kutaka kushiriki tendo la ndoa kwa jinsi unavyofahamu wewe.
Hili ndilo kosa wanaume wengi sana wanafanya kwa wake zao bila hata kujua madhara yake.
Wanaume wengi hupenda kuwa viongozi wawapo kitandani na kulazimisha wake zao washiriki nao tendo la ndoa kwa namna na mitindo fulani ambayo wao wanaume wanataka.
Hilo ni kosa kubwa sana.
Na hata pale mwanamke anapojitoa uoga na kutaka kukushauri tushiriki hivi mwanaume anakuwa mkali na haelewi kitu.
Wanaume mtambue wanawake nao ni binadamu na wana hisia tofauti tofauti kila mmoja na wanaitika tofauti.
Kama umezoea kufanya tendo la ndoa kwa namna fulani na anafurahia basi usifikiri unaweza kufanya hivyo hivyo kwa kila mwanamke na akaridhika.
Siyo kila mwanamke anaweza kufika kileleni kwa kuwekewa tu uume ukeni na kumkoboa hapo masaa mawili!
Kuna wanawake wanahitaji mambo mengine zaidi na wanapenda ushiriki nao tendo Ia ndoa kwa namna fulani ambayo ni nzuri kwao.
Namna nzuri ya kufanikiwa katika hili ni kumpa uhuru mkeo muwapo kitandani.
Siku nyingine mpe uongozi yeye ndiyo aongoze tamasha.
Utagundua huwa anapenda tendo la namna gani.
Au unaweza kumuuliza moja kwa moja kwamba unatakaje?
Unapenda vipi?
Kitu gani au staili gani inakuvutia na kukuamsha zaidi?
Muulize pole pole mara kwa mara na kama kweli umemfanya kuwa rafiki yako wa karibu na siyo mama wa kukulelea tu watoto basi atafunguka kwako.
Jambo la mhimu hapa ni kuwa chochote atakachokuambia anapendelea unawajibika kumpa au kumfanyia bila kuhoji hoji au kuanza kumshangaa tena wakati uliuliza mwenyewe na amekupa jibu la kweli toka moyoni mwake.
Wanawake wanapenda sana mwanaume mwenye kifua na mwenye siri.
Hawapendi mwanaume mlopokaji anayeongea na kila mtu kuhusu mahusiano yake na mkewe hata yale ya kitandani.
Kuna namna fulani ya tendo la ndoa mkeo anapenda na wewe hujawahi kumuuliza wala kumpa ruhusa ya kuwa kiongozi wa mechi japo mara moja moja.
Kama uliona mwanamke akilia kwa namna fulani kwenye video za wakubwa basi unataka na mkeo naye awe anafanya hivyo, huo ni upumbavu.
Wanawake hawapendi mwanaume anayeigiza kila alichokiona kwenye video.
Kila mwanamke ana namna yake ya kuitika na siyo lazima iwe sawa na yule uliyemuona kwenye video.
Mpe ruhusa akuambie anatakaje na anapendaje.
Kama wewe ni mwanaume na unahitaji dawa ya asili kwa ajili ya kuondoa madhara yatokanayo na punyeto na kuimarisha nguvu za kiume niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175
SHARE POST HII NA WENGINE uwapendao