Last Updated on 14/09/2022 by Tabibu Fadhili Paulo
Mambo 6 ambayo huwa hawakuambii kuhusu maisha ya ndoa
1. Mahaba mazito ya mwanzo hayadumu milele
Kila mara unapoanza mahusiano mapya au kila penye ndoa mpya huwa kunakuwa na mahaba mazito.
Ni wakati huo unaweza kujihisi upo juu ya watu wote kwenye hii dunia.
Ni wakati wa kimuhemuhe, ni wakati wa hamasa, ni wakati wa shauku kubwa kwa kila mmoja kwa mwenzake.
Ni wakati wa furaha kuu.
Furaha ambayo haiwezi kuelezeka kirahisi na mtu akakuelewa.
Ni wakati huu ukisikia watu wanasema mapenzi yanaumiza na hayana maana unawaona kama watu hao ni wapumbavu na wasiojitambua kabisa.
Hapa kila mmoja anamuona mwenzake ni wa mhimu na wa thamani sana.
Hapa kila mmoja anamwambia mwenzake kamwe sitakuacha na nipo tayari hata kufa kwa ajili yako!
Lakini kadri miaka inavyoenda ndani ya miaka mitatu au mpaka miaka mitano hivi hali hii hubadilika ghafla na kila mmoja kuanza kumuona mwenzake kama kituko.
Hapa kila mmoja anaweza kwa nyakati fulani kuanza kujihoji ilikuwaje nikaoa au kuolewa na huyu?.
Kwahiyo ukiwa kwenye vikao vya harusi kabla ya kuanza kuishi na mke au mme wako hakuna mtu atakuambia jambo hili kwamba kuna wakati mtaanza kuchokana na hata kugombana.
Kila mtu hata viongozi wa dini watakuwa wanakuambia sasa utaenda kuwa na furaha tele na kwamba shida zote kwenye maisha yako zimeisha!
Ukweli ni kwamba hiyo ni furaha ya muda mfupi kabla hamjaanza kugombana na kila mmoja kuanza kumuona mwenzake kama kituko fulani hivi.
Wapo wanandoa ambao huchukua muda mrefu zaidi kufikia hatua hii ambapo inaweza kuchukua mika 10 au hata zaidi ya hapo.
Hawa ni wale ambao wanafahamu kwamba kila mmoja anawajibika kwa mwenzake na wapo tayari kufanya kila liwezekanalo ili kufanya mapenzi yao kuonekana bado ni mapya na yasiyochosha.
Kwahiyo hoja yangu hapa ni kuwa unapoingia kwenye ndoa usiwe na mawazo kwamba itakuwa ni furaha tu mwanzo mwisho.
Hapana.
Mwanzoni mtapendana sana mpaka utajiona umemaliza hii dunia lakini ukae ukijua kadri miaka inavyoenda lazima hamu hiyo ya kupendana sana itapungua na hiyo ni hali ya kawaida kwa ndoa nyingi.
Utatakiwa ulifahamu hili ili ujiandae kisaikolojia na wakati huo huo uwe tayari kuweka nguvu ili kufanya ndoa yenu iendelee kuonekana ni mpya na isiyochosha.
Hii ndiyo sababu unapoachana na huyu na kuanza mahusiano na mwingine mpya unajihisi raha sana na kuona kama ulikuwa unapoteza muda na yule mwingine, kumbe ni hali tu ya kawaida hutokea hivyo kwa kila mahusiano yoyote mapya.
2. Maisha yenu ya kitandani yatapata msukosuko baada ya kuzaa watoto
Mkishaoana na mpo wawili tu maisha yenu ya kitandani yatakuwa mazuri na yenye kupendeza sana.
Hapo mtafurahia sana tendo la ndoa mpaka kwenye nukta ya kutokurudi tena duniani.
Lakini hali hiyo huanza kupungua na kupatwa na shida za hapa na pale mara tu mtakapoanza kuzaa watoto.
Mkishakuwa na mtoto mmoja au wawili tu tayari nafasi yenu ya kushiriki tendo la ndoa inaweza kushuka au kupungua kwa zaidi ya nusu yake.
Kama kabla ya kuzaa mlikuwa mnashiriki mara 4 kwa wiki basi mkishakuwa na watoto wawili inaweza kushuka mpaka mkaanza kushiriki mara 2 tu kwa wiki au hata mara 1.
Hiyo ni hali ya kawaida kabisa kwenye ndoa nyingi na wala lisikushangaze litakapokutokea.
Hili nalo ni jambo ambalo hakuna mtu atakuambia wakati wowote wa maandalizi ya ndoa yenu, si wazazi, si wakubwa wenu wala viongozi wa dini watawaambia jambo hili.
Lakini ni jambo linalotokea kwa ndoa karibu zote.
Na kadri mnavyozidi kuzaa watoto wengi mara kwa mara bila kusubiri muda mwingi upite baada ya kuzaa mmoja ndivyo tatizo linavyozidi kuwa kubwa.
Kuepuka hali hii isitokee haraka unashauriwa usiwe na haraka sana ya kuzaa mara baada tu ya kuoana na kuanza kuishi pamoja.
Walau mwaka mmoja au hata miwili ipite baada ya kuoana ndipo muanze kuwaza kuzaa mtoto.
Msisikilize ndugu, jamaa au marafiki wanaowashawishi kuzaa haraka, dhumuni hasa la kuoana siyo kuzaa na wala siyo lazima kwamba mkioana lazima mzae watoto kama jamii inavyojaribu kuwaaminisha hilo.
Tatizo la watu wengi wapo bize sana kuishi kama vile jamii au watu wengine wanavyotaka badala ya kuishi maisha yao wenyewe kama wanavyotaka.
Vile vile nakushauri ukishapata mtoto mmoja basi walau ipite miaka mitano ndipo uzae mwingine na siyo unazaa kila baada ya mwaka mmoja au miaka miwili.
3. Talaka inaweza kuwa ni jambo la kuambukizwa
Hili nalo ni jipya na wengi huwa hawaambiwi kuhusu hili.
Ingawa sipendi kuharibu kirahisi hivyo ndoa yako ya sasa lakini ukweli ni kuwa watu wako wa karibu wana uhusiano fulani na ubora wa maisha yako.
Kama una marafiki watano wazuri kwako na wa karibu yako sana au hata ndugu zako labda dada yako au shangazi yako na hao wote ndoa zao hazikudumu basi kuna uwezekano mkubwa hata yako pia haitadumu.
Inaweza kukushangaza sana hii.
Kama katika rafiki zako watano wa karibu sana, wanne kati yao ndoa zao hazikudumu basi hata ndoa yako kuna uwezekano mkubwa itavunjika pia.
Jambo hili hakuna kiongozi wa dini, ndugu yako wa karibu au wakubwa zako wengine watakuambia unapokuwa kwenye maandalizi yako ya kuoa au kuolewa.
Ila kuna msemo ambao kila mtu anaufahamu unasema ; NIONYESHE RAFIKI ZAKO NIJUE TABIA YAKO.
Kwenye utafiti mmoja wa mwaka 2013 uliowahi kufanywa na jarida moja liitwalo ‘SOCIAL FORCE JOURNAL’ ulibaini kuwa talaka inaweza kuwa kama ugonjwa wa kuambukiza ukisambaa baina ya marafiki, ndugu na jamaa.
Kama mkeo ana marafiki wengi ambao ndoa zao hazikudumu kuna uwezekano wa mpaka asilimia 75 wa ndoa yenu kuisha kwa njia ya talaka pia.
Unachoweza kufanya kuzuia ugonjwa huu usifike kwenye ndoa yenu ni kujitahidi kuwa mbali na marafiki au ndugu wa namna hiyo na kujitahidi sana kuishi kwa mjibu wa akili yako binafsi na siyo kwa kusikiliza maneno ya wengine kuhusu mambo ya ndoa.
Jitahidini kukaa mbali na watu ambao ndoa zao zilivunjika na muishi kwa kanuni zenu binafsi na msiwe watu wa kueleza sana shida zenu kwa marafiki na ndugu.
Kama ni marafiki ni rahisi kuwatenga na kutafuta wengine lakini kama ni ndugu itakuwa vigumu kuwatenga lakini jitahidi usiwasimulie sana kuhusu ndoa yenu au shida zenu zingine.
Kuna wanawake au hata wanaume wengine wakigombana kidogo tu, tayari anakimbilia kumsimulia ndugu yake au rafiki yake ambaye na yeye huyo rafiki au ndugu ndoa yake haikudumu na mwisho wa haya yote hata wewe utashauriwa; ‘Achana naye tu kwani kuna nini, mbona hata mimi niliachana na fulani na ninaishi tu bila shida’.
Tumeshashuhudia haya kwenye jamii yetu, ni mhimu kwako wewe uyafahamu haya usije kusema hukuambiwa.
4. Vigezo na mashariti ya kuoa na kuolewa vimekuwa vikiongezeka siku hadi siku
Kabla ya mwaka 1850 ili mwanaume uweze kuoa ulihitajika tu uonyeshe unalo shamba la kulima na una afya ya kukimbizana na simba au wanyama wengine wakali wakisogea kwenye nyumba yenu!
Baada ya mapinduzi ya viwanda mwanzoni mwa miaka ya 1900 kigezo kikuu kikawa ni mwanaume uwe una kazi ya kukuingizia kipato, umeenda shule, na una hofu ya Mungu.
Baada ya kuja kwa facebook vigezo vimekuwa vingi sana kiasi kwamba kuoa sasa ni kama anasa na ni jambo wanaloliweza matajiri tu.
Baada ya kuja facebook sasa ili uoe lazima uwe na nyumba yako binafsi, umeenda shule, kazi nzuri, gari, una hela ya kutosha na uwe na uwezo wa kumpeleka mkeo nje (out) kula au kunywa kwenye hotel na migahawa ya gharama japo mara 2 kwa mwezi.
Hayo nimetolea kama mifano tu na unaweza kucheka kama una nafasi.
Ninachotaka kujaribu kukueleza hapa ni kuwa kwa sasa kama unataka kuoa na uwe na amani hasa kwa sisi tunaoishi mijini ni bora ujenge kwanza uwe na nyumba yako binafsi ndipo uoe.
Hata sheria ya ndoa tu iliyopo sasa kama wewe ni mwanaume na unataka uishi vizuri na huyo mkeo mtarajiwa ni bora ujipange kwanza vya kutosha mkeo akija awe na hitaji moja tu labda la nguo au kwenda out lakini mengine yote yawepo tayari.
Hili nalo hakuna mtu atakuambia kabla ya kuingia kwenye ndoa yako lakini mimi leo tayari nimekuambia na ikiwa unahitaji kunipa zawadi yoyote nijulishe tu kwanza kwenye WhatsApp +255714800175.
Kama unapanga kuoa halafu muanze kuhangaika kutafuta mali pamoja na huyo mkeo hata kama yeye anakaa tu nyumbani kuosha vyombo wewe unagombana kwenye daladala huko unahangaika kutafuta mjenge au mnunue gari basi siku mkiachana mtagawana 50 kwa 50 tofauti na kama angekukuta navyo vyote tayari unavyo.
Kwahiyo vigezo na masharti ya kuoa na kuolewa vimekuwa vikiongezeka mwaka hadi mwaka.
Na hapa nimezungumzia zaidi kwa upande wa mwanaume tu lakini wanaume nao wamekuwa na vigezo vyao vingi wanapotaka kumuoa mwanamke husika tofauti na ilivyokuwa zamani na hakuna mtu atakuambia hili mapema.
5. Siyo jukumu la mwanamke kumpenda mwanaume
Hili siyo jambo jipya au jambo geni hasa kwa wale wanaosoma na kuielewa Biblia vizuri.
Kwa mjibu wa Biblia mwanamke hawajibiki kumpenda mmewe.
Hili linaweza kukushangaza sana lakini ni jambo ambalo watu wengi hawafahamu.
Kama wewe ni mwanamke na unampenda mmeo basi ujuwe hicho ni kiherehere chako tu, huwajibiki wala hutakiwi kumpenda mmeo.
Wala kitu kikubwa mwanaume anachokihitaji toka kwa mkewe siyo kupendwa au kushiriki naye tendo la ndoa kama watu wengi mnavyodhani.
Jukumu kuu la mke ni KUTII na siyo KUPENDA.
Ni mwanaume ndiye anayewajibika kumpenda mkewe lakini mwanamke hahitajiki kumpenda mmewe zaidi ya KUMTII.
Mwanamke kazi yake kuu ndani ya ndoa ni kumtii mmewe, basi, na siyo kumpenda.
Kama mwanamke anampenda mmewe na hana dalili zozote za kumtii mme huyo ndoa hiyo haitafika popote.
Sasa hakuna ndugu, kiongozi wa dini au wakubwa zako wengine watakaokuambia siri hii.
Na hii ni siri nzito ambayo kama kila mwanamke angeifahamu basi ndoa nyingi sana zingekuwa ni sehemu ya mbinguni hapa hapa duniani.
Hakuna kitu unaweza kumchanganya mwanaume kiasi cha kukupa chochote unachotaka hasa kama ana uwezo huo pale anapoona mkewe una utii kwake.
Sasa nitoe angalizo hapa kabla sijaendelea.
Ninaposema utii simaanishi utii kwa kila kitu hata kwa yale yanayoweza kuharibu utu na haki zako kama binadamu.
Kuna mengine unaruhusiwa kusema hapana hasa kama yanaenda kinyume na utu na ubinadamu.
Wanaume wote wanatamani sana sana kuishi na mwanamke mwenye chembe chembe za utii ndani yake.
Ukiwa mkaidi hakuna mwanaume ataendelea kuvumilia kuishi na wewe hata uwe mrembo kiasi gani.
Kwahiyo ni jukumu la mme kumpenda mkewe na ni jukumu la mke kumtii mmewe na siyo kumpenda.
Kama utahitaji ufafanuzi zaidi nitafute tuonane uso kwa uso nitakusaidia zaidi.
6. Ahsante ni neno dogo lakini linadumisha ndoa
Ndoa nyingi sana hazifiki popote sababu ya kukosekana neno AHSANTE kwenye maisha ya wanandoa hao.
Neno Ahsante ni neno dogo lakini kama mke au mme analitumia mara nyingi kwa mwenzake basi ndoa yao lazima itafika mbali.
Wanandoa wengi baada ya kuishi miaka mingi huanza kusahau umhimu wa neno hili na kuanza kuona kila jambo zuri analotendewa na mwenzake basi ni haki yake na hivyo haoni sababu ya kusema ahsante.
Mmeo au mkeo amekununulia pipi mwambie ahsante, amekufulia nguo mwambie ahsante, amekubali kukupa haki yako ya kitandani bila kinyongo na kwa furaha zote mwambie ahsante na kadharika na kadharika.
Naomba niishie hapa kwa leo na kama kuna mtu anatafuta dawa ya asili ya kumsaidia kupata watoto mapacha basi niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175 na dawa inagharimu 210,000/- (laki 2 na elfu 10) kwa sasa na bei inaweza kupanda zaidi siku za mbeleni.
Tafadhari share post hii na wengine uwapendao.