Kitu kimoja ambacho karibu wanandoa wote hugombana kwa sababu yake

Last Updated on 04/01/2023 by Tabibu Fadhili Paulo

Kitu kimoja ambacho karibu wanandoa wote hugombana kwa sababu yake

Kila ndoa unayoiona au kila wanandoa unaowaona hata kama kuna nyakati wanaonekana kuwa na furaha sana machoni pa watu, bado kuna nyakati huwa wanagombana!

Bila kujali dini yao, umri wao, elimu zao, kipato chao, rangi zao, yaani bila kujali chochote kuwahusu wanandoa husika bado kuna nyakati huwa wanapishana na kuzozana na hata kupigana.

Hiyo ni hali ya kawaida kwa watu wawili wanaoishi pamoja na hali ya kawaida kwenye mahusiano yoyote hata yale ambayo siyo ya mapenzi.

Kwahiyo kama bado hujaoa au hujaolewa tambua mapema kwamba utakapoingia kwenye maisha ya ndoa haitakuwa ni raha na furaha tu kila siku.

Kuna siku mtanuniana, hamtaongea kabisa na wakati mwingine mmoja anaweza hata kuhama kulala chumbani na akahamia kulala sebuleni au kulala chumba cha watoto.

Sababu za ugomvi kwenye kila ndoa ni tofauti na kila wanandoa wana namna yao ya kutatua migogoro kwenye ndoa zao.

Hata hivyo ipo sababu 1 ambayo ni chanzo cha ugomvi karibu katika kila ndoa unayoiona chini ya jua.

Kuna ndoa chanzo cha ugomvi wao kila mara ni kuchelewa kurudi nyumbani na ulevi uliozidi wa baba, ndoa zingine chanzo cha ugomvi wao ni usaliti na kukosa uaminifu, wengine ni kudharauliana na kuchukuliana poa na kadharika na kadharika.

Lakini katika ndoa zote lipo jambo moja ambalo ni chanzo cha ugomvi wa mara kwa mara ndani ya nyumba.

Je ni jambo gani hilo?

Jibu ni PESA.

Chanzo cha ugomvi kwenye ndoa nyingi

Pesa au hela au money ndicho chanzo kikuu cha ugomvi kwenye ndoa zote popote duniani bila kujali wanandoa husika ni kina nani na wana nini.

Hata kama wanandoa husika tayari ni matajiri na wana kila kitu bado kuna siku tu ipo watazozana huku chanzo cha ugomvi huo kikiwa ni hela!

Wanaume karibu wote wanapenda kuoa mwanamke mwenye matumizi mazuri ya pesa.

Wanaume hawapendi kuishi na mwanamke asiyeweza kutunza hela.

Wanaume wanaposema wanataka mke mwema moja ya huo wema ni pamoja na mwanamke mchungu na pesa na siyo anayefuja na kutumia hela kwa kila kinachoonekana machoni pake hata kama hakina ulazima wa kuwa nacho kwa wakati huo.

Pesa ndiyo chanzo cha migogoro kwenye ndoa nyingi sana hapa duniani.

Utafiti wa hivi karibuni unasema miaka ya hivi karibuni wanawake wengi wamepoteza mvuto machoni pa waume zao huku chanzo kikitajwa kuwa ni vicoba!

Mwanamke akiwa kwenye ndoa na akawa na kwenye kikoba basi akili yake masaa mengi inawaza madeni ya vicoba tu na wakati mwingine anapoteza hadi hamu ya tendo la ndoa kisa vicoba.

Kuna wakati kwenye ndoa mnaweza kuwa mnaweka hela kidogo kidogo kwa ajili ya kununua kiwanja lakini akapita mtu anauza vitenge mkeo anaweza kutumia hela ya kiwanja itatumika kununua vitenge bila wasiwasi wowote.

Wapo wanaume pia wenye matumizi mabaya ya pesa, mwanaume akipata tu hela anawaza kulewa na umalaya na kuoa wanawake wengine zaidi!

Kwenye ndoa nyingi iwe ni Afrika, iwe ni ulaya, Asia au Amerika chanzo kikuu cha ugomvi ndani ya ndoa ni hela.

Mizozo mingi kwenye ndoa nyingi chanzo chake ni hela.

Pia zipo ndoa nyingi zilizovunjika mara tu wanandoa walipoanza kuwa na hela na utajiri, yaani hapo kabla walipokuwa maskini waliweza kuishi kwa furaha na amani lakini mara tu hela zilipoanza kuwatembelea ndoa zao ziliishia hapo!

TUFANYAJE SASA kama hali ndiyo hiyo?

Kwanza kabisa napenda kukujulisha kwamba kugombana kwenye ndoa siyo jambo baya na haimaanishi kila mnapogombana basi ndiyo mwisho wa ndoa yenu au ndiyo mtaachana.

Hapana!

Kugombana siyo dalili ya kuachana na wala siyo chanzo cha ndoa kuvunjika.

Ni jambo la kawaida kabisa na ni ishara kwamba mnapendana na kila mmoja anamjali mwenzake.

Ikiwa mnaishi miaka yote bila kugombana ni dalili mmoja wenu kati yenu ameshakufa tayari ingawa bado anaonekana yupo hai.

Hata hivyo katika kugombana kwenu muepuke vitu vifuatavyo :

1. Msiishi mkigombana kila siku

Pamoja na kwamba kugombana kwenye ndoa ni jambo la kawaida, bado msiishi kwa kugombana kila siku.

Walau zipite wiki kadhaa au miezi kadhaa au hata miaka ndipo mgombane, lakini kamwe isiwe kila siku nyinyi ni watu wa kugombana tu.

2. Hakuna sababu yoyote ya msingi ya kuwajulisha ndugu, wazazi, majirani au marafiki kila mara mnapogombana

Kama ikitokea ugomvi kidogo tu basi umeshakimbilia kuwajulisha wazazi au jamaa zako wengine huo ni wendawazimu na ndiyo unatengeneza mazingira mazuri ya ndoa yenu kuvunjika.

Kama ugomvi ni mkubwa na ulikuwa na viashiria fulani vya uvunjifu wa amani hapo ni sahihi kuwajulisha wengine

Siyo ugomvi mdogo tu tayari umeshaenda kupost Facebook! Huo ni wendawazimu.

3. Kuwe na akaunti 3 tofauti za pesa zenu.

Akaunti 1 yenu wote wawili, akaunti nyingine ya baba peke yake na akaunti nyingine ya mama peke yake

4. Hata kama ni kweli kwamba majukumu ya kulea familia ni ya baba, bado hakuna ubaya wowote na wewe mama kuchangia kuhudumia familia pale unapobahatika kupata pesa iwe ni kwenye biashara zako au kwenye mshahara wako kama umeajiriwa.

Kuna baadhi ya wanawake wanafahamu sana kuhusu haki sawa kwenye mambo mengine lakini siyo kwenye kulea familia.

Unakuta mama anaingiza milioni 2 kwa mwezi na baba anaingiza laki 8 kwa mwezi lakini bado huyo mwanamke hawezi kununua hata mboga tu kwa ajili ya familia na atamwachia majukumu yote baba huku yeye hela yake akiitumia kwenye kusukia nywele na kununua nguo na viatu kila siku.

Naomba kwa leo niishie hapa.

Kwenye makala hii nimeeleza juu ya chanzo kikuu cha ugomvi ndani ya familia zote popote duniani na nimetaja kwamba chanzo hicho ni hela au pesa au money.

Ikiwa ndoa yako inaishi kwa ugomvi kila siku na unahitaji msaada wangu zaidi na upo Dar Es Salaam au karibu na Dar Es Salaam na ungependa kuja kuniona na kupata ushauri zaidi kutoka kwangu niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175 naweza kukusaidia hilo kwa gharama ya shilingi 33000/=(elfu 33).

Vile vile ikiwa wewe ni mke na unaishiwa au unakosa hamu ya tendo la ndoa mara kwa mara na unahitaji dawa nzuri ya asili kwa ajili hiyo isiyo na madhara yoyote mabaya basi niachie tu ujumbe WhatsApp 0714800175

Share post hii na wengine uwapendao

Imesomwa na watu 138
Kitu kimoja ambacho karibu wanandoa wote hugombana kwa sababu yake

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WhatsApp 0714800175