Last Updated on 14/01/2023 by Tabibu Fadhili Paulo
Dalili 17 za homoni kutokuwa sawa kwa mwanaume
Hali ya homoni kutokuwa sawa kwa mwanaume hutokea wakati mwili wako unapozalisha sana au wakati mwili wako unazalisha kidogo sana homoni mhimu kwenye mwili wako.
Hali ya homoni imbalance kwa maisha ya sasa ya mbio na haraka ni jambo la kawaida sana kwa wanaume wengi.
Kila mwanaume atakutana na hali ya kupungua au kuongezeka kwa homoni zake mara kadhaa katika safari yake ya kuishi.
Mfumo wa tezi mwilini (endocrine glands system) ndio unaohusika na kuzalisha, kutunza na kuzitoa homoni ziende kwenye mzunguko wako wa damu mwilini.
Homoni ya testosterone ndiyo hutambulika kama homoni kuu kwa mwanaume sambamba na homoni zingine ambazo ni cortisol, insulin na thyroid.
Hata hivyo hali ya homoni kutokuwa sawa (homoni imbalance) ya kipindi kifupi haiwezi kuwa na madhara yoyote mabaya.
Homoni huuzunguka mwili wako kupitia kwenye mzunguko wako wa damu na kuzifikia ogani na tishu mbalimbali na kufanya kazi zifuatazo ;
1. Kudhibiti hamu ya chakula na mmeng’enyo wake
2. Kudhibiti matendo ya kulala na usingizi
3. Mapigo ya moyo
4. Kudhibiti hitajio la tendo la ndoa na afya ya via vya uzazi
5. Kukua na kuendelea kwa mwili kwa ujumla
6. Hali ya utulivu wa akili kwa ujumla
7. Joto la mwili
Kwa kawaida mwanaume anaweza kuanza kupata hali ya homoni kutokuwa sawa kuanzia umri wa miaka 20 kwenda juu na kadri anavyozidi kuwa na umri mkubwa ndivyo na tatizo linavyoweza kutokea kirahisi zaidi.
Sababu za homoni kutokuwa sawa kwa wanaume
Tatizo la homoni kutokuwa sawa linaweza kutokea kutokana na sababu nyingi zikiwemo ;
1. Matumizi ya muda mrefu ya baadhi ya dawa za hospitali
2. Msongo wa mawazo (stress) wa muda mrefu
3. Kutokula chakula sahihi
4. Uvimbe sehemu mbalimbali kwenye mwili
5. Kutokujishughulisha na mazoezi ya viungo
6. Ugonjwa wa kisukari
7. Uzito mkubwa
8. Dawa za uzazi wa mpango
9. Saratani
10. Upungufu wa madini chuma
11. Matatizo kwenye mfumo wa tezi
Dalili za homoni kutokuwa sawa kwa mwanaume
1. Kupata choo kigumu mara kwa mara
2. Msongo wa mawazo
3. Maziwa kuongezeka na kuwa kama ya msichana mdogo
4. Kukosa umakini
5. Ngozi kuwa kavu
6. Kupungukiwa nguvu za kiume kwa muda mrefu
7. Kuishiwa hamu ya tendo la ndoa
8. Uchovu sugu na udhaifu wa mwili kwa ujumla
9. Kushindwa kutungisha mimba
10. Kupungua kwa wingi na ujazo wa misuli
11. Kukosa usingizi mara kwa mara
12. Kuwa na mifupa dhaifu na matatizo mengine yanayohusiana na mifupa
13. Kupungua kwa uzito ghafla
14. Kuongezeka kwa kiu cha maji na kukojoa mara kwa mara
15. Kuathirika kirahisi na hali ya hewa ikiwa ni baridi au joto
16. Mabadiliko ya mapigo ya moyo na kupata kirahisi shinikizo la juu la damu
17. Hasira za mara kwa mara hata kwa maudhi madogo madogo
Kama wewe ni mwanaume na unahitaji dawa ya asili kwa ajili ya kuweka sawa homoni zako niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175.
Share post hii na wengine uwapendao