Last Updated on 01/08/2023 by Tabibu Fadhili Paulo
Sababu kuu 4 kwanini huponi tatizo lako la upungufu wa nguvu za kiume
1. Unasubiri upone ndipo uendelee kushiriki tendo la ndoa
Moja ya kosa kubwa unalolifanya linalokusababishia usipone tatizo lako la upungufu wa nguvu za kiume ni kusubiri upone ndipo uendelee na tendo la ndoa.
Ni kosa kusubiri upone hali yako ya kuwahi sana kufika kileleni kila mara, hali yako ya uume kuwa mlegevu au uume uliosinyaa sababu ya punyeto ndipo uje ushiriki tendo la ndoa.
Unaweza kujiuliza kwanini ni kosa kusubiri kupona lakini jibu lake ni jepesi tu kwamba tendo la ndoa lenyewe ni sehemu ya matibabu ya tatizo lako.
Kama una tatizo la kuwahi sana kufika kileleni na unatumia dawa kisha unasubiri umalize dawa ndipo uendelee na tendo la ndoa basi unaweza usipone kabisa.
Unatakiwa uendelee kutumia dawa kwa uaminifu wote wakati huo huo unaendelea kushiriki tendo la ndoa mara kwa mara.
Kushiriki tendo la ndoa mara kwa mara ni dawa pia ya tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.
Mhimu hapa ni kuwa na kiasi kwa sababu ukizidisha sana kushiriki tendo la ndoa nayo hiyo tabia inaweza kukuletea upungufu wa nguvu za kiume!
Walau mara 2 au 3 kwa wiki ni sawa, lakini usikae wiki 3 au mwezi mmoja bila kushiriki tendo la ndoa.
Kinachowafanya wanaume wengi wasubiri wapone ndipo washiriki tendo la ndoa ni aibu ya kuonekana si lolote mbele ya mwanamke sababu tu amewahi kufika kileleni na hawezi kurudia tena.
Unalotakiwa kufahamu ni kuwa ni bora upate hiyo aibu sasa na baadaye ufurahie maisha yako ya ndoa kuliko uipe aibu nafasi kubwa na uishi na tatizo milele.
Vile vile tambua wanawake wengi hawapo vile kama ambavyo tunadhani wapo, Ukiwa mkweli na muungwana atakuelewa tu bila shida yoyote.
Unaweza kumwambia kabisa mapema kwamba ni kweli nimetaka kushiriki tendo la ndoa na wewe lakini mwenzio nisikudanganye nina tatizo la kuwahi sana kufika kileleni, nina tatizo la kuwa na uume mlegevu na kadharika kwa hiyo usinishangae wala usishtuke!
Mwambie tu usiogope.
Mwambie lakini upo bize na matibabu na unaamini tatizo litaisha siku za hivi karibuni.
Mwanamke ukimwambia hivyo mapema atakuona una akili na unajali na pengine anaweza kukuambia ufanye nini ili na yeye afike kileleni bila kutumia uume wako.
Kwahiyo endelea kutumia dawa wakati huo huo endelea kushiriki tendo la ndoa mara kwa mara hata kama hupati matokeo mazuri kwa wakati uliopo.
Ukifanya hivi kupona tatizo la upungufu wa nguvu za kiume ni uhakika.
Ukiwa mwanaume usiwe muoga, kuwa jasiri ndiyo sifa kuu ya mwanaume.
Na kama unaona kufanya hivyo na mke wako au na mke wako mtarajiwa ni jambo la aibu sana basi jaribu mechi za kirafiki huko nje huku ukiweka tahadhari kubwa usije kuambukizwa magonjwa ya zinaa na utakapoona umepona utarudi kuendelea na maisha yako na mkeo au na mke wako mtarajiwa (mchumba).
Usijiwekee wewe mwenyewe au hata Mungu mipaka sana, maisha ni mafupi na ni haya haya.
Fanya lolote hata kama siyo la kawaida sana machoni pa wengi lakini kichwani kwako umejiwekea lengo kwamba unafanya hayo ili upone uume wako na ukipona utatubu kwa Mungu dhambi zako na kuendelea na maisha yako.
Mungu wetu ni Mungu wa neema na rehema, hatoi hukumu kwa jinsi ya kibinadamu na mara zote kabla ya kukuhukumu kwanza anatanguliza rehema.
Kwa sehemu kubwa tunaokolewa kwa neema na rehema na siyo kwa matendo yetu kwa asilimia 100.
Umeamka mzima leo siyo kwa sababu huna dhambi au wewe ni mtakatifu au kuna jambo lolote ulifanya jana kwa Mungu ndiyo akaona uamke na leo mzima!
Kuna watakatifu wengi tu wamefariki jana ila kwa neema zake tu amekupendelea wewe kuwa hai mpaka leo
Unaweza kulala pia na mwanamke kwa usiku mmoja au dakika kadhaa tu bila kulazimika muwe wapenzi na ukatafuta mwingine tena siku nyingine mpaka umepona.
Mapenzi hayo ya siku 1 au ya dakika kadhaa wazungu huyaita “one night stand”.
Sitapenda kuongea sana lakini na wewe mwenyewe jiongeze na kama unahitaji msaada wa kimawazo zaidi tafuta muda tuonane mimi napatikana Kibugumo Mji Mwema Kigamboni Dar Es Salaam.
2. Unategemea nguvu za mwili peke yake
Nguvu za kiume bado ni msamiati kwa watu wengi.
Wengi hawajuwi nguvu za kiume ni nini hasa.
Wengi unapozungumzia nguvu za kiume akili yao yote inawaza uume!
Uume umeundwa kwa nyama na mishipa ya damu, hakuna mfupa wowote kwenye uume.
Nguvu za kiume hazina uhusiano wa moja kwa moja na uume wako.
Nguvu za kiume ni nguvu za mwili wako wote zikijumuisha nguvu za akili pia.
Sasa kuna wanaume mpo bize na kujenga nguvu za mwili yaani kujenga misuli na muonekano wa nje wa mwili kwa ujumla huku mkisahau kutengeneza pia nguvu za ndani ya mwili (nguvu za akili, nguvu za ubongo, utulivu wa nafsi, usingizi).
Kwahiyo kuwa bize na mazoezi peke yake, kuwa bize na vyakula peke yake bila kuwa bize na afya ya akili yako pia kutaendelea kukuzuia usipone kabisa tatizo lako la upungufu wa nguvu za kiume.
Ninaposema nguvu za akili simaanishi kuwa na akili nyingi darasani au shuleni, hapana, sizungumzii akili za namna hiyo.
Bali ninaposema afya ya akili hapa namaanisha utulivu wa nafsi yako kwa ujumla.
Una amani ya kiasi gani?
Ndiyo nguvu ya akili ninayomaanisha.
Kama huna utulivu wa nafsi basi kunyanyua kwako vyuma, kwenda mazoezini kila siku na kula vizuri hakutasaidia upone tatizo lako la upungufu wa nguvu za kiume.
Unatakiwa uwe na akili iliyotulia na amani nyingi kwenye maisha yako.
Kama una madeni sugu kila kona, watoto hawana ada ya shule, unadaiwa kodi ya nyumba, chakula chenyewe kinapatikana kwa shida, una mawazo mawazo (stress) kila siku, hupati usingizi mzuri na wa kutosha kila siku basi ni vigumu sana wewe kupona tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.
Kwahiyo huponi tatizo lako la upungufu wa nguvu za kiume kwa sababu upo bize na nguvu za mwili bila kufanya lolote kuhakikisha akili yako pia ina nguvu za kutosha.
Ni mhimu kuwa na maisha ya kawaida na ya kuridhika, ila kama una tamaa ya kuishi maisha ya kitajiri sana na uwezo huo huna basi utaendelea kudhuru afya yako ya kitandani bila hata wewe mwenyewe kujua.
Kuwa mtu wa shukrani japo kwa kidogo ulichonacho tayari, kaa karibu na Mungu na ishi vizuri na watu wengine wote bila kujali ni maskini au matajiri.
3. Unadhani kuimarisha nguvu za kiume ni kazi ya siku moja
Hapa ndipo wanaume wengi sana wanapoferi.
Shida kubwa ya tatizo la upungufu wa nguvu za kiume inaanzia hapa.
Wanaume wengi hudhani upungufu wa nguvu za kiume ni jambo linaloweza kutibika kwa wiki 2, kwa kunywa dawa mwezi mmoja halafu umepona milele!
Poleni sana.
Hata malaria tu hakuna dawa ya kunywa mara 1 kisha umepona milele.
Huwa nakutana na wanaume wanaotafuta dawa ya asili kwa ajili ya kuimarisha nguvu za kiume na kutibu madhara yatokanayo na punyeto na wengi wao huuliza kama dawa nitakayowapa itaenda kutibu tatizo lao na hawatahitaji tena dawa milele.
Tatizo la upungufu wa nguvu za kiume haliishi kwa staili hiyo.
Ni jambo endelevu la kila siku maisha yako yote.
Kila siku ukiamka lazima ujue utaishi vipi siku hiyo ili kuendelea kuongeza na kuimarisha nguvu zako za kiume.
Ni sawa na kinga ya mwili.
Hata kuimarisha Kinga ya mwili siyo kazi ya siku 1 au ya dawa 1, ni maisha yako ya kila siku siku zote za uhai wako.
Unapotumia dawa ili kuondokana na tatizo lako la kuwahi sana kufika kileleni au kuwa na uume mlegevu haina maana ni jambo utakalolifanya mara 1 kisha umepona milele!
Hata baada ya kupona bado utahitaji dawa tena huko mbeleni baada ya miezi kadhaa au miaka kadhaa bado utatakiwa kutumia dawa tena ili kuendelea kujiimarisha.
Utatakiwa kuendelea kufanya mazoezi ya viungo mara kwa mara hata kama huna tatizo lolote la upungufu wa nguvu za kiume, utatakiwa uendelee kula vizuri na kuwa na utulivu wa nafsi wakati wote ukiendelea kuishi.
Mhimu ni kuhakikisha unatumia dawa rafiki hasa za asili zisizo na madhara mengine kiafya hata kama utatumia mara nyingi.
Kwahiyo moja ya sababu kwanini tatizo la upungufu wa nguvu za kiume haliishi kwako ni kudhani matibabu yake ni jambo la wakati mmoja kisha umepona milele!
4. Umeweka imani yako yote kwenye dawa na hela unayotoa unaponunua dawa
Siyo jambo baya kuweka matumaini yako kwenye dawa, lakini siyo sawa kuweka imani yako yote kwenye dawa peke yake.
Hili ni kosa kubwa ambalo matabibu tunaliona siyo kwa upande wa nguvu za kiume tu bali karibu kwa magonjwa mengine yote.
Watanzania wengi wanaamini sana kwenye bidhaa kuliko kwenye ushauri na elimu.
Kwa nchi kama Marekani au Ulaya ishu siyo dawa, ishu ni daktari au Tabibu uliyeamua kumtumia kukutibu tatizo lako.
Watu wengi wanatamani kupona na shida yao kubwa ni kupona tu.
Lakini kutegemea dawa peke yake na hela zako bila kuwa karibu na daktari ni kosa kubwa litakaloendelea kukugharimu miaka na miaka mpaka utakapobadilika.
Ndiyo maana mimi huwa napenda tuwasiliane kupitia WhatsApp na siyo kwa simu ya kawaida.
Kwanini?
Ni kwa sababu kwenye WhatsApp tunaweza kuendelea kuchat na kuchat, kuchat na kuchat kila siku na kila mara utakapokuwa na jambo lolote.
Kwenye WhatsApp pia naweza kukutumia hii makala yote unayosoma hapa na ukabaki nayo milele kwenye simu yako.
Siwezi kukutumia makala hii kwa njia ya simu au kwa sms ya kawaida!
Lakini wengi wanapenda kupiga simu na wapewe dawa haraka.
Katika hali tu ya kawaida huwezi kumpigia mtu simu mara 10 kwa siku, lakini unaweza kuchat na mtu WhatsApp hata mara 50 kwa siku.
Kwenye WhatsApp naweza kukutumia picha, naweza kukutumia video, lakini siwezi kufanya hivyo kwa simu ya kawaida au kwa sms ya kawaida.
Lakini sababu watu wanapenda vitu vya haraka haraka bila kuzingatia elimu na ushauri mwingine basi hawaponi na kupata suluhisho la kudumu kwa matatizo yao.
Kwahiyo kama umekuwa ukijiuliza kwanini huponi tatizo lako la upungufu wa nguvu za kiume hata baada ya kunywa dawa kadhaa na kutumia hela nyingi ni kwa sababu umeweka imani yako yote kwenye dawa peke yake bila kuwa karibu na daktari anayekupa dawa.
Kuna mambo mengine mengi ambayo hayahusiani na dawa moja kwa moja na ni ya mhimu ili upone na mambo hayo utayapata tu kwa kuwa karibu na Tabibu aliyekupa hiyo dawa.
Naitwa Fadhili Paulo, ni Tabibu wa Tiba asili, nipo Kibugumo Mji Mwema Kigamboni Dar Es Salaam.
WhatsApp napatikana kwa namba hii +255714800175 na unaweza kuchat na mimi toka popote ulipo hata kama ni chumbani kwako na utajibizana na mimi mwenyewe moja kwa moja na siyo na wasaidizi wangu.
Tafadhali SHARE post hii kwa ajili ya wengine uwapendao.