Last Updated on 16/12/2024 by Tabibu Fadhili Paulo
Kwenye makala hii naeleza kwa kirefu juu ya dalili anazozionyesha mwanaume asiyejiamini.
Kama unapenda kufahamu ikiwa una tatizo la kutokujiamini au huna fuatilia makala hii mpaka mwisho.
Kumbuka naeleza juu ya mwanaume asiyejiamini kwenye ndoa yake au kwa mke wake.
Makala hii haielezi juu ya mwanaume asiyejiamini sehemu nyingine labda kazini au kwenye maisha mengine, hii inajadili juu ya mwanaume asiyejiamini kwenye ndoa yake.
Kama una tatizo la kutokujiamini sehemu nyingine tofauti na kwenye uhusiano wa ndoa basi jaribu kupata msaada sehemu nyingine.
Kutokujiamini kunatajwa kama moja ya sababu inayoweza kusababisha mke kuchepuka kirahisi na hata ndoa kutodumu.
Watafiti wa masuala ya jinsia na mahusiano wanasema mara tu mke anapogundua mmewe ana tabia ya kutokujiamini basi huwa ni ishara tosha kwa mwanamke huyo kwamba anaweza kumuendesha mme atakavyo hata kuchepuka au kumvunjia mme heshima za hapa na pale.
Nisikuchoshe sana na maneno mengi, hapa chini nimekuandikia dalili 8 zitakazokusaidia kujiona ikiwa unajiamini au la
1. Furaha yako yote inategemea mkeo
Katika uhusiano, ni muhimu kuzingatia mahitaji ya mwenza wako.
Lakini kuweka furaha yako yote kwa mkeo siyo jambo sahihi.
Kama inakutokea kwamba furaha yako yote inategemea na mke basi ni dalili haujiamini.
Ni mhimu kuwa na vitu vingine zaidi ya mke vinavyoweza kukupa furaha.
Kwa sababu kuna nyakati utalazimika kuwa mbali na mkeo labda kwa sababu za kuumwa au kusoma au katika shida yoyote inayoweza kukulazimisha kuwa mbali na mkeo kwa muda fulani.
Kumbuka siyo jambo baya kuona mkeo ni furaha yako, siyo jambo baya.
Ubaya ni pale kunapokuwa hakuna kitu kingine zaidi kinachoweza kukupa furaha zaidi ya mkeo kwani hiyo ni dalili haujiamini.
2. Hupendi kukosolewa
Hii ni dalili nyingine ya mwanaume asiyejiamini kwenye ndoa yake.
Kama inakutokea unapata shida sana pale unapokosolewa au pale unapoambiwa udhaifu wako basi ujue unasumbuliwa na tatizo la kutokujiamini.
Mwanaume anayejiamini haogopi kukosolewa, anafahamu kwamba kama binadamu atakuwa na upungufu fulani.
Hivyo siyo jambo baya mkeo akikukosoa au kukueleza kwamba sehemu fulani haupo sawa.
Ukiona unapoambiwa makosa yako unapaniki na kuwa mkali sana basi ujue unasumbuliwa na tatizo la kutokujiamini.
Mtu anayejiamini hata umtolee kashifa gani, kama ni ya kweli utaona anacheka tu na atakuambia ahsante kwa kuchukua muda wako na kunirekebisha.
3. Muda wote unataka kuwa na mkeo
Bila shaka, kila mtu anapenda kujisikia anahitajika, lakini kuna kikomo cha busara kwa hili.
Kama hujiamini, muda mwingi utataka kuwa na mkeo.
Kuna uwezekano ukatamani hata kuacha kazi ili muda wote ubaki na mkeo!
Kuwa karibu na mkeo ni jambo zuri sana na mara nyingi tunahimiza jambo hili lakini bado lazima kuwe na kiasi na mipaka.
Najua wapo wengine kazi zao hufanyia nyumbani na hawalazimiki kwenda mbali na nyumbani kila siku, pamoja na hilo bado usitumie masaa yote 24 kubaki na mke wako tu, nyakati fulani nenda mbali kapige stori na rafiki na jamaa zako wengine.
4. Unatoa zawadi na pongezi mara nyingi sana
Siyo jambo baya pia kutoa zawadi na kumsifia mke mara kwa mara.
Lakini kama unatoa zawadi kupita kiasi ni dalili haujiamini.
Kama kila ukienda nje ukirudi nyumbani ni lazima urudi na zawadi ya mkeo hiyo ni ishara haujiamini.
Kuwe na muda fulani umepita tangu umetoa zawadi moja hadi nyingine lakini siyo kila siku unaleta zawadi.
Wakati mwingine wazawadie hata wazazi wako, ndugu zako hata rafiki zako wengine.
Yaani kuna wakati unatoa zawadi mpaka mke mwenyewe anabaki kujiuliza ikiwa ni salama kweli kichwani kwako au kuna tatizo lingine?.
5. Unataka kujua mkeo anazungumza na nani na nini
Dalili nyingine ya mwanaume asiyejiamini ni kupenda kujua mkeo anazungumza na nani na huwa wanazungumza nini.
Mkeo akipigiwa simu si ajabu ukakimbia kuangalia simu yake ni nani hasa amempigia na wanazungumza nini hasa?
Ukiona una tabia hii kila wakati kwa mkeo ujue haujiamini.
Mtu asiyejiamini huwa na tabia ya kutowaamini na wengine pia.
Kutaka kujua kila kitu kuhusu mkeo kwamba anawasiliana na nani na wanaongea nini ni dalili ya moja kwa moja ya mwanaume asiyejiamini.
Kama unamfuatilia mkeo kwenye mitandao ya kijamii yaani kila akiweka picha au ujumbe wowote iwe ni Facebook au Instagram au mtandao mwingine na wewe lazima utoe maoni (comment) au unapenda (like) ujue una tatizo kubwa la kutokujiamini.
6. Unalalamika mara kwa mara kuhusu rafiki zako wa kike wa zamani
Kama wewe ni mme halafu kila ukimhadithia mkeo kuhusu wachumba zako wa zamani na wakati wote unasema walikuwa ni wabaya, wasaliti na hawafai basi ujue hujiamini.
Haiwezekani wachumba zako wote wa zamani wawe ni wabaya, lazima mmoja au wawili walikuwa wazuri ila wewe ndiyo ulifanya makosa wakakuacha.
Lakini kwa kuwa hujiamini na hivyo huamini wengine basi utataka kuhitimisha kwamba X wako wote walikuwa wabaya.
7. Unamuuliza mara kwa mara mkeo ikiwa anakupenda
Kwa kuwa hujiamini basi ni kawaida kwako kila mara kumuuliza mkeo ikiwa anakupenda.
Kama unajiamini huhitaji kuuliza swali hili kila mara.
Tabia hii ya kuuliza mara kwa mara ikiwa mkeo anakupenda huenda sambamba na kumwambia kila mara asikusaliti
Ukiona haipiti mwezi lazima umkumbushe mkeo kwamba asikusaliti ujue una tatizo la kutokujiamini.
Siyo vibaya kumkumbusha mkeo asikusaliti lakini hutakiwi kumkumbusha hilo kila wakati kwani ni dalili mbaya ya mtu mwenye tatizo sugu la kutokujiamini.
Hizo ni dalili za mwanaume asiyejiamini kwenye ndoa yake na kama kuna nyingine unazifahamu na sijaandika naomba uziandike hapo kwenye boksi la comment.
Ni mhimu pia kama mwanaume umejigundua una tatizo hili la kutokujiamini kujipeleleza na kujichunguza ili kubaini ni nini hasa ndiyo chanzo cha tatizo lako.
Kila mwanaume ana sababu yake inayomfanya apoteze uwezo wa kujiamini kwenye ndoa yake na ndiyo sababu ni mhimu kujichunguza binafsi kuona ni nini hasa kilipelekea mpaka ukaanza kuwa na tabia ya kutokujiamini.
Kama utahitaji maongezi zaidi binafsi tukiwa wawili na upo Dar Es Salaam au karibu na Dar Es Salaam weka miadi (appointment) tuonane tuzungumze juu ya tatizo lako na namna nzuri ya kulitatua kwa upande wako, niachie ujumbe kwenye WhatsApp.
Kabla sijaondoka lazima nikupe na angalizo kuhusu hili nililokufundisha hapa leo;
Ingawa nimesema ni mhimu sana kwa mme kujiamini kwenye ndoa yake au kwa mke wake, ni mhimu kufahamu pia kwamba ukijiamini sana kupita kiasi ni rahisi kuonekana ni mjinga (arrogant).
Ni vizuri kabisa kujizoesha tabia ya kujiamini lakini usisahau kuwa na kiasi kwani kujiamini kukizidi ni rahisi sana watu wengine kukuchukulia kama mjinga na usiyejielewa.
Kama wewe ni mwanaume na unatafuta dawa nzuri ya asili kwa ajili ya kuimarisha nguvu za kiume na kukusaidia usiwahi kufika kileleni, niachie ujumbe WhatsApp +255714800175
*****