Utajuwaje kama upungufu wako wa nguvu za kiume ni tatizo la kisaikolojia au ni tatizo la mwili wako

Last Updated on 10/02/2024 by Tabibu Fadhili Paulo

Utajuwaje kama upungufu wako wa nguvu za kiume ni tatizo la kisaikolojia au ni tatizo la mwili wako

Kama umekuwa ukijiuliza ni nini hasa ndiyo chanzo cha tatizo lako la kupungua kwa nguvu za kiume na hupati jibu, basi hatimaye leo umetua sehemu uliyokuwa ukiihitaji.

Upungufu wa nguvu za kiume unaweza kukutokea kama matokeo ya mwili wako kutokuwa na nguvu hasa kama ishara ya uwepo wa magonjwa mengine au kama matokeo ya saikolojia yako kutokuwa sawa.

Kwenye makala hii nafafanua namna ya kufahamu iwapo chanzo cha tatizo lako ni mwili (physical) au ni saikolojia (mind).

1. Upungufu wa nguvu za kiume unaweza kukutokea kama matokeo ya saikolojia pale ubongo unaposhindwa kutuma taarifa ya kukusisimua kuhusu tendo la ndoa kwenye mishipa ya damu ya uume.

Hali hii inaweza kukutokea wakati wowote hata wakati ukiwa katikati ya mchezo!

Hapa ni kwamba saikolojia yako inakuwa imevurugwa, yaani akili yako inakuwa haipo sawa na hivyo ni vigumu uume kusimama imara.

Kwa Kawaida hali hii haitokei mara kwa mara labda kama mwanaume husika anasumbuliwa na msongo wa mawazo kwa muda mrefu.

Dalili zitakazokuonyesha kwamba tatizo lako linatokana na mvurugiko wa akili ni pamoja na zifuatazo :

*Umezungumza na Daktari wako na amekupa dawa na amekupima vipimo vyote na huonekani kuwa na ugonjwa wowote maalumu unaoweza kukuletea upungufu wa nguvu za kiume.

Ukiona daktari haoni ugonjwa wowote unaojulikana wazi kusababisha upungufu wa nguvu za kiume basi ni dalili tosha tatizo lako ni la kisaikolojia zaidi.

*Kama ukijaribu kupiga punyeto unaona uume unasimama vizuri lakini ukiwa na mwanamke uume unagoma kusimama imara ni ishara kuna tatizo kichwani kwako na siyo kwenye viungo vya mwili

*Angalia ufanisi wa kazi zako nyingine ambazo hazihusiani na tendo la ndoa na huko nako ukiona ufanisi na ubora wa kazi zako unapungua tofauti na siku za nyuma ni dalili kuna kitu siyo sawa kinaendelea kichwani kwako

Hizo ni dalili chache Kati ya nyingi zinazoweza kukujulisha kwamba una tatizo la upungufu wa nguvu za kiume kama matokeo ya saikolojia yako kutokuwa sawa.

Tuangalie sasa ni nini ndiyo chanzo hasa cha saikolojia yako kutokuwa sawa.

Linapokuja suala la chanzo cha msongo wa mawazo au stress huwa ni jambo tofauti kwa kila mwanaume.

Chanzo cha stress kwa John hakiwezi kuwa sawa na cha George, kila mwanaume ana changamoto zake za pekee ambazo hazifanani na mwingine.

Hata hivyo vifuatavyo ni moja kati ya vyanzo vingi vya kuvurugika kwa saikolojia miongoni mwa wanaume wengi:

  • Ukosefu wa elimu kuhusu tendo la ndoa
  • Wasiwasi wa kutomfikisha mkeo au mchumba wako kileleni
  • Matatizo na migogoro ya kwenye mahusiano
  • Matatizo yanayohusiana na uchumi na kipato
  • Hali ndogo sana ya kujiamini
  • Mtazamo mbaya kuhusu tendo la ndoa
  • Baadhi ya magonjwa hasa UKIMWI
  • Kutokujishughulisha na chochote kinachoweza kuimarisha afya ya akili kama vile mazoezi ya viungo na kupata usingizi wa kutosha
  • Ulevi wa kupindukia (Ulevi kupita kiasi)
  • Kama matokeo ya uraibu wa kutazama picha na video za wakubwa (x)
  • Historia mbaya ya zamani katika tendo la ndoa nk

Haijalishi nini ndiyo chanzo cha tatizo la saikolojia yako kuvurugika iwe nimekitaja hapa au sijakitaja bado kuna tumaini kwako kama upo tayari kuondokana na tatizo hili.

Kama upo Dar Es Salaam au maeneo ya karibu na Dar na unahitaji msaada zaidi kuhusu tatizo hili fanya mpango tuonane tuongee zaidi ili kufikia muafaka sahihi wa kumaliza tatizo lako, weka miadi (appointment) kwenye WhatsApp +255714800175, mimi napatikana Kibugumo Mji Mwema Kigamboni.

Utajuwaje kama upungufu wako wa nguvu za kiume ni tatizo la kisaikolojia au ni tatizo la mwili wako

.

2. Upungufu wa nguvu za kiume unaweza kukutokea pia wakati kuna kitu siyo sawa kwenye mwili wako (in your physical body)

Hapa uume unashindwa kusimama vizuri na kuhimili tendo la ndoa kama matokeo ya shida fulani kwenye mwili na siyo kwenye ubongo.

Akili yako ipo salama, huna mawazo mawazo, hela ipo ya kutosha lakini mwili hauwezi kusimamia show (mchezo).

Mara nyingi tatizo hili huwakumba wanaume wanaokaribia kuzeeka na wazee, wenye magonjwa kama kisukari, vidonda vya tumbo, bawasiri, shinikizo la juu la damu, wenye kolesto na uzito uliozidi.

Hapa ubongo unatoa taarifa za msisimko lakini kitu fulani katika mwili kinazuia mtiririko huru na sahihi wa damu kwenye mishipa ya damu mwilini na kuelekea kwenye uume.

Dalili kuu zitakazokuonyesha kuwa tatizo lako la upungufu wa nguvu za kiume linatokana na mwili na siyo akili yako ni kuwa utapata shida ya uume kusimama imara katika hali zozote na tatizo linaweza kukutokea mara nyingi zaidi au hata kwa mfululizo kwa kipindi kirefu.

Pamoja na hayo yote bado hakuna sababu yoyote ya kuchanganyikiwa kwa sababu suluhisho lipo labda kama chanzo ni uzee basi hapo hakuna namna nyingine zaidi ya kukubaliana na hali yako.

Vifuatavyo ni vyanzo vya upungufu wa nguvu za kiume kama matokeo ya mwili wako kutokuwa sawa :

  • Magonjwa mbalimbali kama vile kisukari, vidonda vya tumbo, bawasiri, shinikizo la juu la damu, uzito na unene kupita kiasi nk
  • Matumizi sugu ya vilevi
  • Kutoshiriki mazoezi ya viungo
  • Matatizo kwenye Mfumo wa upumuwaji
  • Mabadiliko ya homoni mhimu kwa mwanaume
  • Kama madhara mabaya (side effects) ya baadhi ya dawa za kizungu
  • Kama madhara ya kupiga punyeto kwa kipindi kirefu
  • Uchovu sugu
  • Chakula ambacho siyo sahihi

Mpaka hapo natumaini utakuwa umepata uelewa juu ya tatizo la upungufu wa nguvu za kiume kama matokeo ya saikolojia yako kuvurugika (stress) na Matatizo yanayohusiana na mwili wako (physical).

Upungufu wa nguvu za kiume una vyanzo vingi na vipo vinavyoweza kuondoka haraka na vipo vinavyochukua muda kuondoka.

Mchawi hapa ni kupata tabibu wa kushea naye tatizo lako na siyo kukaa kimya na kukata tamaa, kama utanichagua mimi kukusaidia kuondokana na tatizo lako basi tuwasiliane WhatsApp +255714800175

Share post hii na wengine uwapendao

Imesomwa na watu 31
Utajuwaje kama upungufu wako wa nguvu za kiume ni tatizo la kisaikolojia au ni tatizo la mwili wako

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WhatsApp 0714800175