Nguvu za kiume ni nini?

Last Updated on 01/11/2024 by Tabibu Fadhili Paulo

NGUVU ZA KIUME NI NINI?

Nguvu za kiume ni neno linalotumika mara nyingi kumaanisha ‘Uwezo wa mwanaume kufanya tendo la ndoa’.

Na inapokuwa tofauti na hivi, tunaita ni ‘kupungua au kukosa nguvu za kiume’.

Kupungukiwa kwa nguvu za kiume hutofautiana toka mtu mmoja hadi mwingine.

Inaweza kuwa ni hali ya kutokuwa na uwezo wa kusimamisha uume, au hali ya kutokuwa na uwezo wa kufika kileleni kwa muda mzuri wa kutosha.

Nguvu za kiume pia siyo idadi ya mabao.

Hilo ni mhimu kwanza ulielewe.

Unaweza kwenda mabao hata manne na bado ukaonekana huna nguvu za kiume.

Nguvu za kiume ni muda gani umetumia kubaki hapo mchezoni ndiyo jambo la mhimu.

Kama unafika mpaka magoli manne na kila goli unatumia dakika 3 au 4 kufika kileleni basi tunaweza kusema wewe huna nguvu za kiume.

Ila kama utaweza kwenda goli moja tu na likachukua dakika 10 au 15 au 20 hivi na kuendelea hakika tunasema wewe una nguvu za kiume.

Tunaamini muda huo umetosha kuweza kumfikisha mwenza wako kileleni.

Mwanaume pia utahitaji kujua dalili au ishara za mwanamke anapofika kileleleni.

Bila kujua dalili au ishara za mwanamke anayefika kileleni ni kazi bure.

Kama unahitaji kuzifahamu ishara na dalili za mwanamke anayefika kileleni nitafute WhatsApp +255714800175 nikuelekeze na itakugharimu 33000 (elfu 33).

Kumbuka pia tendo la ndoa siyo ugomvi.

Wapo baadhi ya wanaume wanadhani ili umfikishe mwanamke basi unatakiwa umfanye kwa nguvu au kwa fujo sana utadhani ni ugomvi fulani hivi!, mapenzi siyo hivyo.

Ndiyo hutakiwi ufanye kilegelege sana lakini pia huhitaji kufanya kwa nguvu kama vile ni ugomvi!

Tatizo ni hizo video feki mnazotazama mnadhani mapenzi ndiyo huwa hivyo jambo ambalo si kweli.

Kila mwaka wasichana na wanawake wengi hutekwa na watu wasiojulikana sehemu mbalimbali duniani na baadhi yao hufanyiwa vitendo vya kikatili ikiwemo vya kingono na hurekodiwa.

Sasa wewe unapoangalia picha kama hizo unadhani mapenzi ndiyo hufanywa hivyo kumbe si kweli.

Kuna wanaume wakianza kazi hiyo ni kama vile mashine inakoboa mahindi yaani ni ugomvi mwanamke anabaki akiumia tu na kama hajuwi naye anabaki kuumia tu. Hata siku nyingine ukimhitaji atakataa kwa visingizio vingi sababu unamuumiza bila wewe kujua.

Pole pole, kwa nguvu kidogo inapochanganya lakini siyo kwa fujo kama vile ugomvi. Umeipata hiyo?! bila shaka kazi inabaki kuwa kwako!.

Kumbuka mwanaume lazima utafika kileleni hata iweje, hivyo ni jukumu lako kuhakikisha kabla hujawa na uwezo tena wa kuendelea na tendo la ndoa uwe umeona na una uhakika mke wako naye amefika kileleleni.

Hivyo nguvu za kiume siyo idadi ya mabao, ni muda unaotumia kubaki hapo kifuani ndiyo mhimu na si idadi ya mabao.

Pamoja na hayo yote, elimu mhimu ambayo mwanaume anatakiwa kuwa nayo, ni kuwa nguvu za kiume hazipatikani kwa kutumia madawa ya kemikali au mahala pengine; bali zinatokana na vyakula tunavyokula kila siku.

Imesomwa na watu 2
Nguvu za kiume ni nini?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WhatsApp 0714800175