Last Updated on 01/11/2024 by Tabibu Fadhili Paulo
Sababu za uume kushindwa kusimama
Kushindwa kwa uume kusimama pia hutambulika kama kuishiwa nguvu za kiume. Ni kitendo cha mtu kushindwa kusimamisha uume au kudumisha usimamaji wa uume kwa muda wa kutosha kufanya tendo la tendo na mwenza wake.
Pamoja na ukweli kuwa mara zote Mwanaume lazima atafika kileleni, hali huweza kuwa tofauti kwa upande wa pili kwani mwanamke anahitaji mwanaume akawie zaidi ili na yeye (mwanamke) aweze kutosheka.
Mkeo hupendelea ukawie na ikiwezekana ukawie zaidi. Kama utakuwa unawahi kumaliza, basi mkeo anakuwa hapati raha kamili.
Hata hivyo tambua pia kuchelewa sana kufika kileleni inaweza kuwa kero kwa mwenza wako. Kwa kawaida wanawake wengi wanaweza kufika kileleni kuanzia dakika ya 8 kwenda juu tangu tendo la ndoa lianze.
Muda mzuri wa kutumia katika kushiriki tendo la ndoa bila kuleta kero zingine ni kati ya dakika 15 mpaka dakika 30 hivi. Ikiwa mwanaume ataendelea bila kufika kileleni hata baada ya dakika 35 au 40 na zaidi basi hiyo sasa ni kero na si tendo la ndoa tena.
Ingawa, kama una tatizo la kuwahi kufika kileleni hauko peke yako. Asilimia 30 hadi 40 ya wanaume wa rika zote wanakabiliwa na tatizo la kuwahi kufika kileleni au kupungukiwa kwa nguvu za kiume.
Hata hivyo kutambuwa tu kwamba wanaume wengine pia wana tatizo kama lako siyo sababu ya wewe kukaa tu bila kutafuta suluhisho la tatizo lako.
Habari njema ni kuwa zipo njia zinazoweza kuleta matokeo mazuri na hatimaye kulimaliza tatizo hili bila madhara mabaya hapo baadaye.
Wakati mwingine uume kushindwa kusimama inaweza kuwa si tatizo, lakiini jambo hilo linapojitokeza kila mara na kwa kipindi kirefu inaweza kuleta msongo wa mawazo kwa mume na hata kwa mke.
Sababu nyingine ambazo zinaweza kupelekea uume usisimame vizuri ni pamoja na matatizo ya mhemko kama;
1. Wasiwasi
2. Hasira
3. Msongo wa mawazo (Stress)
4. Huzuni
5. Hofu na mashaka
6. Kukosa hamu ya tendo la ndoa n.k
Ili uume usimame vizuri ni lazima:
1. Mfumo wako wa neva uwe na afya nzuri inayopelekea mpwito neva (nerve impulses) katika ubongo, uti wa mgongo na uume.
2. Mishipa ya ateri iliyo na afya ya ndani na iliyo karibu na corpora cavernosa
3. Kiwango sahihi cha oksidi nitriki (nitric oxide) ndani ya uume.
Uume kushindwa kusimama vizuri kunaweza kusababishwa pia kama kipengele kimojawapo hapo juu hakifanyi kazi vizuri.
Mambo mengine yanayopelekea kupunguwa kwa nguvu za kiume, uume kushindwa kusimama vizuri na kuwahi kufika kileleni ni pamoja na:
1. Uzee
2. Kisukari
3. Kujichua/Punyeto
4. Uzinzi
5. Kukosa Elimu ya vyakula
6. Kutokujishughulisha na mazoezi
7. Shinikizo la juu la damu
8. Ugonjwa wa moyo
9. Uvutaji sigara/tumbaku
10. Utumiaji uliozidi wa kafeina
11. Kudhurika kwa neva au uti wa mgongo
12. Madawa ya kulevya
13. Kupungua kwa homoni ya testerone
14. Athari kutoka kwa baadhi ya dawa
15. Pombe
16. Kutazama picha za X mara kwa mara
17. Kukaa muda mrefu kwenye kiti