Je Punyeto ni dhambi kwa mjibu wa Biblia?

Je Punyeto ni dhambi kwa mjibu wa Biblia

Last Updated on 23/05/2024 by Tabibu Fadhili Paulo

Swali: Je Punyeto ni dhambi kwa mjibu wa Biblia?

JIBU: Biblia haisemi moja kwa moja wala kutaja punyeto kama ni dhambi.

Aya ya kwenye Biblia ambayo mara nyingi huwa inanukuliwa ikihusishwa na punyeto ni habari ya Onan kwenye kitabu cha mwanzo 38 : 9 – 10. Wengine huutafsiri mstari huu kwa maana ya kwamba kumwaga mbegu zako nje ya uke ni punyeto.

Hata hivyo hicho sicho huo mstari ulimaanisha.

Mungu alimlaumu Onan siyo kwa kumwaga nje mbegu zake bali ni kwa sababu Onan alikuwa ni muasi.

Onan alikataa kutimiza majukumu yake na kutoa urithi kwa ndugu zake.

Hiyo aya kwahiyo haihusu punyeto au kujichua bali ni katika kutimiza majukumu ya familia.

Je Punyeto ni dhambi kwa mjibu wa Biblia

Aya ya pili kwenye Biblia ambayo hutumika kama ushahidi wa dhambi ya kujichua ni katika Mathayo 5 : 27 – 30.

Hapa Yesu alikuwa akizungumzia juu ya kuwa na mawazo mabaya yanayopelekea dhambi na anasema, ‘Ikiwa mkono wako wa kulia unakusababishia wewe kufanya dhambi basi ukate na uutupe’.

Ingawa kuna uhusiano juu ya mawazo mabaya na punyeto bado sina uhakika kama Yesu alikuwa akizungumzia kuhusu punyeto kwenye hii aya.

Biblia yote kwa ujumla haina aya au ukurasa unaozungumzia moja kwa moja kwamba punyeto ni dhambi.

Punyeto kwa sehemu kubwa ni matokeo ya mawazo mabaya yaliyomo kichwani na nafsini mwa mtu, kuangalia picha chafu na mazungumzo mabaya.

Ni matatizo hayo ndiyo yanayopaswa kushughulikiwa kwanza kabla hujaifikiri punyeto yenyewe.

Ikiwa dhambi ya mawazo mabaya, mazungumzo mabaya, tamaa mbaya na kuangalia picha chafu itakoma basi moja kwa moja hakutakuwa na punyeto.

Watu wengi wapo bize na kuhoji juu ya punyeto wakati katika hali ya kawaida wanatakiwa wahoji na kutubu juu ya yale yanayompelekea mtu kupiga punyeto kwanza.

Kwa sababu kama hizo swali hili la je punyeto ni dhambi kwa mjibu wa Biblia linahitaji mjadala mpana kwanza.

Soma na hii > Dawa ya kuongeza nguvu za kiume

Wakati Biblia haisemi moja kwa moja ikiwa kujichua ni dhambi au la kuna kanuni kadhaa za kiBiblia tunazoweza kuzitumia ili kupata jibu lenye muafaka zaidi.

(1) 1 Wakorintho 10 : 31

31. Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lo lote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu.

Kama katika chochote ufanyacho hakimpi Mungu utukufu ni vizuri usikifanye hicho kitu.

(2) Warumi 14 : 23

23 Lakini aliye na shaka, kama akila, amehukumiwa kuwa ana hatia, kwa maana hakula kwa imani.

Na kila tendo lisilotoka katika imani ni dhambi.

Ikiwa tuna uhakika kabisa jambo hili nifanyalo halimpi Mungu utukufu, basi jambo hilo ni dhambi.

(3) 1 Wakorintho 6 : 19 – 20

19. Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;

20 maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu.

Miili yetu imeokolewa na inamilikiwa na Mungu, ni hekalu lake hivyo chochote kibaya tufanyacho juu ya miili yetu ikiwemo kujichua ni dhambi.

(4) Wagalatia 5 : 22 – 23

22 Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,

23 upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.

Kujichua au kupiga punyeto ni matokeo ya moja kwa moja ya mtu kukosa kiasi na kushindwa kujidhibiti nafsi.

Kweli hizo kadhaa zilizomo katika Biblia lazima ziwe na ujumbe mzito juu ya yale tufanyayo na miili yetu.

Kwa mjibu wa aya hizi, wengi wanahitimisha kwamba punyeto ni dhambi.

Punyeto kama punyeto haiwezi kuwa inampa Mungu utukufu ambaye ndiye mmiliki halali wa miili yetu na haiwezi kufanywa hadharani na kwa kujiamini kabisa.

Kama umekuwa ukijiuliza ikiwa punyeto ni dhambi au siyo dhambi basi jibu unalo.

Hata hivyo jambo la mhimu si kuwa punyeto ni dhambi bali jambo la mhimu ni kuwa unayafahamu madhara ya punyeto kwa afya yako ya mwili na akili?

Soma hii pia > Madhara ya punyeto kwa wanaume

Kama unatafuta dawa ya asili ili kujitibu madhara yatokanayo na punyeto au kujichua niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175, ninayo pia dawa kwa anayewahi sana kufika kileleni na ya kuondoa kitambi pia.

Naitwa Fadhili Paulo, ni Tabibu wa Tiba Asili na ni mTanzania.

Ofisi yangu inaitwa Tumaini Herbal Life ipo Kibugumo Mji Mwema Kigamboni Dar Es Salaam.

SHARE kwa ajili ya wengine uwapendao

Imesomwa na watu 3,124
Je Punyeto ni dhambi kwa mjibu wa Biblia?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WhatsApp 0714800175