Last Updated on 06/08/2021 by Tabibu Fadhili Paulo
Katika makala hii nitakueleza Vyakula ambavyo mwanaume hatakiwi kula ili kubaki na afya bora wakati wote. Kuna vingine unaweza kuwa unavitumia kila siku bila mwenyewe kujuwa.
Awali ya yote elewa tu kuwa hii ni orodha ndogo sana katika vyakula ambavyo mwanaume hatakiwi kula. Ni sehemu ndogo na kwa hakika vinazidi zaidi ya vyakula 20 ambavyo hutakiwi kula.
Jina langu naitwa Fadhili Paulo.
Endelea kusoma ….
Ukiacha sigara ambayo imeandikwa wazi ni hatari kwa afya yako, vitu vingi tunavyokula na kunywa havifai kwa afya zetu.
Kuna vyakula vingine kwenye orodha hii vinashtua sana watu wengi wanapovisoma kwa mara ya kwanza kwani ni tofauti na walivyoelezwa na kuamini kwa muda mrefu na vingine vinatishia maslahi ya wengine.
Kwa sasa vyakula vingi si salama na bado sisi waafrika tuna nafuu kidogo ukilinganisha na wenzetu wazungu kwani sisi ardhi yetu kwa sehemu kubwa bado haihitaji mbolea za viwandani ili kukuza mazao mbalimbali.
Shida zaidi inaonekana kwa watu wanaoishi mijini kuliko wale wa vijijini.
Dar Es Salaam kwa mfano karibu asilimia 90 watu wanakula nyama ya kuku wa kisasa, ni kuku ambao wanafugwa kwa muda wa siku 30 tu!
Kuku wa kisasa ndio wanaotumika sana kwenye masherehe mbalimbali hapa mjini na kila kona kila mgahawa na vibanda vya chakula hawa ndio kuku wanaoliwa zaidi.
Ni vigumu kukuta mgahawa au hoteli wanauza kuku wa kienyeji.
Sasa kuku anafugwa na kuwa tayari ndani ya siku 30 kuna usalama gani hapa kiafya!
Ukiacha kuku uje kwenye samaki nako hakuna usalama.
Wajasirimali wengi sasa wanafuga samaki kwenye mabwawa na samaki hao hulishwa vyakula mbalimbali ili waweze kukua kwa haraka.
Vyakula hivi wanavyopewa samaki hawa bado si salama kwa afya zetu.
Kuna samaki pia wanaingizwa kutoka nchi zingine ambao nao namna wanavyofugwa na kuhifadhiwa si salama kwa afya zetu na hili tumeshaliona siku za nyuma kuna kontena kadhaa zimewahi kukamatwa na serikali zikihusishwa kuwa na samaki ambao hawafai kwa matumizi ya binadamu.
Tukija kwenye mboga za majani nako hali si shwari.
Mboga nyingi za majani zinazolimwa mijini zinalimwa kwa kutumia mbolea za viwandani zisizofaa kwa afya ya binadamu.
Kama haitoshi mboga hizi zinamwagiliwa kwa kutumia maji machafu na kupuliziwa madawa ambayo nayo si salama kwa afya zetu.
Hivi karibuni tulimsikia waziri mmoja akisema hata ugali wa dona nao si salama kwani mahindi yanayotumika kutengeneza unga huo yanahifadhiwa na dawa zisizofaa kwa afya zetu.
Tukija kwenye matunda nako hakuna usalama kwa asilimia 100.
Matikiti maji kwa mfano naambiwa hata ile rangi yake ya ndani ili iwe nyekundu kabisa na ya kuvutia kuna dawa yanapuliziwa yakiwa shambani.
Kuna mapapai ya kisasa pia huko sokoni na mitaani, nimeona maparachichi ya kisasa pia na nikiuliza yanatoka wapi wengi wanajibu yanatoka Burundi ukiyaona utaona ni makubwa kweli kweli kwa umbile tofauti na mengine ya kawaida tuliyoyazoea!
Kwahiyo utaona wazi ni vigumu sana kukwepa kula vyakula visivyofaa kwa afya kwa nyakati za sasa na hasa kwa watu waishio mijini.
Pengine chakula pekee chenye usalama kwa asilimia 99 kwa sasa ni maji ya kunywa hasa maji ya bombani kwako nyumbani au ya kwenye kisima.
Soma hii pia > Vyakula vinavyoongeza nguvu za kiume kwa haraka zaidi
Vyakula 6 ambavyo mwanaume hutakiwi kula;
1. Punguza kula vyakula feki kuzuia kupoteza nywele
Moja ya matatizo makubwa upande wa urembo kwa wanaume ni kupoteza nywele (upala).
Lakini kama unatafuta kitu cha kukilaumu dhidi ya tatizo lako la kunyonyoka nywele basi ni hiyo sahani yako ya chipsi unayokula kila siku.
Vyakula feki (junk foods) ni hivyo vinapatikana kwenye fast foods na takeaway centers nyingi hasa mijini kadharika vyakula vile vyote vya kwenye maboksi.
Vyakula hivi feki vina kiasi kingi mno cha lehemu (cholesterol) na lehemu hii hupelekea kile huitwa kwa kitaalamu kama ‘pregnenolone’ na kupelekea kiasi kikubwa cha ‘dihydrotestosterone’ (DHT) na hatimaye kupotea kwa nywele kichwani a.k.a upara.
Kunyonyoka kwa nywele kunaweza kuwa ni jambo la kurithi (genetics) lakini vile vile aina ya chakula unachokula kinaweza kuwa kinahusika moja kwa moja.
2. Punguza kunywa pombe au acha kabisa kuzuia kuota matiti
Wanaume wengi wanaokunywa bia kupita kiasi huwa na uwezekano mkubwa wa kupatwa na tatizo la kuota matiti kama wamama tatizo lijulikanalo kwa kitaalamu kama ‘gynecomastia’.
Kwenye bia au pombe mara nyingi hakuna lishe ya moja kwa moja na hivyo hukufanya ujisikie njaa au hata kuongzeka kwa njaa zaidi na ndiyo sababu unaambiwa kama huna uhakika utakula wapi ni bora usinywe pombe ili kulinda afya yako.
Kwenye bia kuna kitu kama homoni ya oestrogen ya kupandikizwa na hivyo unywaji pombe kupita kiasi kuna uhusiano wa moja kwa moja na matokeo ya wanaume kuwa na matiti kama wanawake.
Soma pia hii > Dawa ya kuongeza nguvu za kiume
3. Acha kutumia baadhi ya mafuta ya mboga mboga kuepuka saratani ya tezi dume
Mafuta yatokanayo na mboga mboga au mimea yamekuwa yakipigiwa debe kwa miaka mingi na watu wanaojihusisha na lishe, wajasiriamali wa mafuta hasa ya alizeti na wale wanaharakati wenye hasira sana na mafuta yatokanayo na wanyama.
Kama kuna orodha inayoshtua watu wengi basi ni hili la mafuta ya mimea au mboga mboga.
Watu wengi wanaona haiwezekani na wengine wanafikia hatua ya kuhoji maswali ambayo yanakatisha tamaa na hasa wajasiriamali wa alizeti.
Mpendwa napenda tu kukujulishwa kuwa elimu haina mwisho na pale maslahi yako yanapoguswa usiwe mtu wa kupaniki.
Usiwaze kwamba labda biashara yako ya mafuta ya alizeti itashuka, hapana.
Miaka yote watu wa afya wamekuwa wakisema sigara ni mbaya kwa afya lakini hujawahi kuona sigara zimeachwa kutengenezwa au watumiaji wake wamepungua, la hasha hata sigara zipande bei vipi bado watu watanunua na sigara na pombe ndiyo vitu vinatuingiza kodi nyingi kuliko hata madini hapa nchini.
Hivyo tulia, relax na uwe tayari kujifunza vipya usivyovijuwa na hata vinavyotishia biashara na maslahi yako.
Hata hivyo leo nakujulisha baadhi ya mafuta hayo ya mimea na mboga mboga si salama sana kutumika na mwanaume kila siku.
Hili limekuja hasa kutokana na kuongezeka kwa magonjwa ya moyo na lehemu (cholesterol) na watu wakahimizwa kutumia mafuta ya namna hiyo.
Lakini baadhi ya mafuta haya ya mboga mboga ndiyo kitu kibovu kabisa unatakiwa kukiepuka ili usipatwe na saratani ya tezi dume.
Saratani ya tezi dume ni ugonjwa unaoendelea kujipatia umaarufu miaka ya karibuni na idadi kubwa ya wanaume wanaendela kuugua ugonjwa huu hasa wale wenye miaka 40 na kuendelea.
Linapokuja suala la kujilinda na saratani ya tezi dume basi mafuta yenye omega 3 ndiyo suluhisho la kudumu na siyo mafuta yenye omega 6 kama ilivyo kwenye vyakula vingi vya kwenye makopo, mafuta ya alizeti, maharage ya soya, mafuta ya canola na mafuta ya corn na mengine yote yenye omega 6.
Mwili wako bado unahitaji mafuta yenye omega 6 lakini kwa kiasi kidogo sana tofauti na ambavyo umekuwa unakula kila siku.
Matumizi ya kuzidi ya mafuta yenye omega 6 zaidi kuliko omega 3 yanahusihwa moja kwa moja na kuongezeka kwa magonjwa kwenye mfumo wa upumuwaji, saratani mbalimbali, kisukari, uzito kupita kiasi, uvimbe na maumivu katika mishipa.
Mafuta gani sasa tutumie kama hata ya alizeti hayafai? swali zuri.
Nimesema baadhi ya mafuta haya ya mimea si salama hasa yakitumika kila siku na kwa wingi. Hivyo mara moja moja unaweza kutumia lakini yasiwe ndiyo mafuta makuu kwa kila unachopika.
Kwa vyakula unavyohitaji mafuta mengi kama vile ukipika chipsi au maandazi unaweza kutumia mafuta haya ili kuepuka gharama kubwa za mafuta mengine ambayo ni salama kwa afya.
Kumbe mafuta mazuri zaidi kwa mwanaume ambayo unaweza kuyatumia hata kila siku ni pamoja na mafuta ya Nazi, mafuta ya mbegu za maboga, mafuta ya mawese, mafuta ya zeituni, mafuta ya ufuta na mafuta ya mbegu za mlonge.
Utaona mafuta haya kwanza hayapatikani kirahisi na ni gharama sana ukilinganisha na hayo mengine uliyozoea kuyatumia.
Hii ni fursa kwa watu wenye mtizamo chanya (people with positive mindset) kuamua sasa kuwekeza nguvu kwenye kutengeneza mafuta haya mengine mazuri kwa afya kama mafuta ya nazi kwani tuna utajiri mkubwa wa nazi hapa nchini.
Soma pia hii > Dawa ya saratani ya tezidume
4. Popcorn
Popcorn au bisi ni chakula kingine mwanaume hatakiwi kula, hupikwa kwa kutumia mafuta yasiyo na afya, sodiamu nyingi na ni chanzo cha baadhi ya kansa.
Kuna kitu kinaitwa ‘Diacetyl’ kinachopatikana kwenye popcorn ambacho kinahusika na kusababisha kansa na kuna kingine kiitwacho ‘Perfluorochemicals’ ambacho huathiri tezi ya thyroid na ugonjwa wakati huo huo husababisha ugonjwa wa kupungukiwa umakini ujulikanao kwa kiingereza kama ‘Attention-deficit/hyperactivity disorder (ADHD)‘.
Ni vizuri kuacha kula popcorn
Soma pia hii > Dawa ya asili ya kuzuia mimba kuharibika
5. Mkate mweupe
Mkate mweupe una wanga mwingi zaidi usio na faida. Kwenye hatua za kutengeneza mkate mweupe vitamini zote za kundi B hupotea, hupotea pia nyuzinyuzi (fiber).
Siyo hivyo tu mkate mweupe umesemekana kuwa ni sababu ya ugonjwa wa kisukari na kuongeza uzito zaidi mwilini wakati huo huo ukisababisha tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu sana.
Vingine vinavyofanana na na hilo ni ugali wa sembe, tambi nyeupe, chai ya rangi na kahawa.
Kula mkate ambao ngano yake haikukobolewa (brown bread), kula ugali wa dona na chai unaweza kutumia tangawizi au mdalasini badala ya majani ya chai.
Soma pia hii > Dawa ya asili ya kupata mimba haraka
6. Chumvi ya mezani
Chumvi ya mezani ile ya unga nyeupe haifai kwa mwanaume.
Kila mmoja amesikia chumvi hii husababisha shinikizo la juu la damu na pamoja na hayo bado sehemu kubwa ya watu wanatumia chumvi hii.
Chumvi ya mezani husafishwa kwa kuondoa madini madini na hupitishwa katika joto la nyuzi joto 1093.
Kwa hiyo uliyonayo sasa ni asilimia 40 ya sodiamu na asilimia 60 ya kloridi, na kisha kemikali kama vile ‘aluminium silicate’ huongezwa ili kuifanya isishikane na hivyo kubaki katika hali ya unga.
Aluminium silicate inatajwa kuwa ni miongoni mwa sababu zinazosababisha ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu (Alzheimer).
Chumvi ya mawe ya baharini ile ambayo haijapita kiwandani (unrefined sea salt) ndiyo nzuri zaidi kwa afya ya mwanaume
Nini kifanyike sasa ili kuepukana na haya yote?
Bila shaka utakuwa una swali kama hili.
Bado nasisitiza vyakula safi, vizuri na vya asili bado vinapatikana.
Tujitahidi kuvitafuta kokote vilipo na tuvitumie.
Vingine kama mboga za majani unaweza kuamua mwenyewe kuchukua jukumu la kulima bustani yako ndogo hapo nyumbani kwako ambayo utakuwa na uhakika na usafi wa maji unayotumia kumwagilia na hautaweka mbolea au madawa yasiyofaa kwa afya yako.
Wakati huo huo mazoezi ya viungo yanabaki kuwa ndiyo mwokozi wetu mkubwa kwa afya zetu nyakati za sasa.
Inapokuwa ni vigumu kuepuka mojawapo ya vyakula hivi basi tunaweza kuzikinga afya zetu na madhara ya vyakula hivi kwa kuwa bize na mazoezi ya viungo kila siku.
Soma pia hii > Madhara ya punyeto kwa wanaume
Kama una swali au unahitaji ushauri wowote uliza hapo kwenye comment ni faraja kwangu kuona nimekujibu vizuri.
Barikiwaaa
Amina
Naomba kujua sehemu nayoishi kwa sasa kuna tendency ya wafanyabiashara wanatukatia matunda katika mchanganyiko mbalimbali mfano anaweka parachichi,tango,ndizi,chungwa,tikitimaji, na nanasi je hakuna ubaya wowote katika mchanganyiko huo?
Hakuna ubaya wowote ndugu ALLAN GEORGE