Kwanini mazoezi ya viungo ni mhimu sana kwa nguvu za kiume

Last Updated on 15/01/2024 by Tabibu Fadhili Paulo

Kupitia makala hii nitakueleza kwanini mazoezi ya viungo ni mhimu sana kwa nguvu za kiume. Pia utapata kuona mazoezi manne maalumu kabisa kwa kazi hii.

Zingatia sana umhimu wa mazoezi ya viungo. Bila kujishughulisha na mazoezi ya viungo kila siku itakuwa ni vigumu sana kwako kupona tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.

Kutengeneza mishipa na kupunguza uzito isiwe ndiyo sababu pekee ya kwenda gym.

Kama unahitaji nguvu za kiume na uume wenye afya, unahitaji kujishughulisha na mazoezi ya viungo mara kwa mara ili kusafisha mishipa ya damu na hivyo kuongeza kiasi cha utiririkaji wa damu kwenda kwenye uume.

Kama uzito wako upo juu sana na ni mnene fanya mazoezi ya kukimbia (jogging) kila siku kwa mwezi mmoja mpaka miwili. Kama uzito wako upo sahihi tu kwa mjibu wa urefu wako fanya mazoezi ya kuchuchumaa na kusimama.

Kwanini mazoezi ya viungo ni mhimu sana kwa nguvu za kiume?

Jina langu naitwa fadhili paulo.

Endelea kusoma ….

Wanaume napenda mfahamu tunapozungumzia nguvu za kiume hatuzungumzii nguvu za uume, bali tunazungumzia nguvu za mwili na siyo nguvu za uume kama uume.

Mwili una vyanzo vikuu vitatu vya nguvu ambavyo ni;

1. Chanzo kikuu cha kwanza cha nguvu cha mwili ni SUKARI. Hapa ni sukari yenyewe kama ilivyo sukari au vyakula kama vya wanga na protini hubadilishwa na kuwa glukozi au sukari ambayo ndiyo nguvu ya mwili

2. Chanzo cha pili cha nguvu ya mwili ni MAFUTA. Na hiki ndiyo chanzo pekee cha nguvu cha mwili chenye uwezo wa kukupa nguvu nyingi kuliko chanzo kingine chochote cha nguvu cha mwili.

Hivyo ukikutana na mtu anakuambia usile mafuta ili upate nguvu za kiume atakuwa amekupoteza sababu mafuta yenyewe ni chanzo cha nguvu chenye uwezo wa kukupa nguvu nyingi kuliko vyanzo vingine viwili vya nguvu vya mwili.

3. Chanzo cha tatu cha nguvu za mwili ni MAJI NA CHUMVI. 

Hivi karibuni imegundurika kuwa, mwili unao uwezo wa kutengeneza nguvu kwa kutumia maji (hydroelectric energy), wakati maji peke yake yanapoingia kupitia kuta za seli na kuwasha pampu maalumu za majenereta ya kuzarishia nguvu yaitwayo kwa kitaalamu, ‘cation pumps’, ni kama vile bwawa la umeme linapojengwa karibu na mto mkubwa.

Inajionyesha wazi sasa kwamba ubongo unategemea zaidi nguvu zitokanazo na umeme wa maji hasa katika mifumo yake ya usafirishaji kwenye neva zake kwenda sehemu mbalimbali za mwili.

Ili kuhimili mahitaji ya ubongo, mwili umekuza mfumo maalumu ili kutunza kiasi cha kawaida cha sukari katika mzunguko wa damu.

Hufanya hivyo kwa njia mbili, ya kwanza ni ile ya kusisimua ulaji wa vyakula vyenye protini na wanga ambavyo vitabadilishwa kuwa sukari ikijumuisha pia sukari yenyewe katika mlo, njia ya pili ni ya kubadili wanga na protini toka katika hifadhi ya mwili na kuwa sukari.

Njia hii ya pili huitwa kwa kitaalamu kama ‘Gluconeogenesis’, yaani utengenezwaji wa sukari toka katika malighafi zilizohifadhiwa. Utengenezaji wa aina hii ya sukari hufanyika katika Ini.

Hivyo ni vigumu mtu kuishi bila mafuta, wanga au sukari

Soma pia hii > Mazoezi maalumu yanayoongeza nguvu za kiume

Kwanini mafuta ni mhimu katika kutengeneza nguvu za mwili?

Kila gramu 1 ya mafuta hutoa kalori 9 za nishati(nguvu), kila gramu 1 ya protini au sukari hutoa kalori 4 za nishati(nguvu).

Hii ndiyo sababu mafuta yanapotumika kuzarisha nguvu, mtu hajisikii sana njaa na anakuwa na nguvu nyingi zaidi kuliko kama maji/chumvi au sukari/wanga/protini vikitumika kuzalisha nguvu

Kwahiyo utaona mafuta yana uwezo wa kukuletea nguvu za mwili mara 2 zaidi kuliko vyanzo vingine viwili vya nguvu vya mwili

Sasa shida ipo hapa. Mwili kamwe hauchagui mafuta kama chanzo chake cha nguvu isipokuwa tu umefanya mazoezi ya viungo au umefunga kula chakula masaa kadhaa. 

Bila kufanya MAZOEZI AU KUFUNGA KULA mwili utaendelea kuchagua SUKARI kama chanzo chake cha nguvu na mafuta yataendelea kujirundika mwilini bila kuwa na faida yoyote na hivyo kukuletea kitambi, manyama uzembe na mwisho kukuletea tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.

Kwahiyo ukikutana na mtu anakuambia usitumie mafuta ili kuwa na nguvu za kiume anakudanganya.

Mafuta ni mhimu kwako kama ilivyo mhimu pia vyakula vya wanga na protini lakini ni lazima uwe bize na mazoezi ya viungo kila siku ili kupata faida hii adimu ya mazoezi ya viungo kwa nguvu za mwili na kiume kwa ujumla.

Soma pia hii > Dawa ya kuongeza nguvu za kiume

Mafuta nayo yamegawanyika mara mbili. Kuna mafuta mazuri na mafuta mabaya.

Kwa mfano mafuta yanayotumika kupikia chipsi au maandazi au mafuta mengi tunayotumia kupikia majumbani si mafuta mazuri.

Hata nafuta ya alizeti si mafuta mazuri kwa afya ingawa hili wajasiriamali wengi wa mafuta ya alizeti hawataki kulisikia ukilisema kwani wanaona unawaharibia biashara yao. 

Mafuta mazuri kabisa ni yale yenye OMEGA 3 ambayo ni pamoja na mafuta ya nazi, mafuta ya mawese, mafuta ya mbegu za maboga, mafuta ya ufuta, mafuta ya parachichi, mafuta ya zeituni na mafuta ya samaki.

Kama mwanaume yupo bize na mazoezi ya viungo kila siku anaweza kula mafuta yoyote yawe mazuri au mabaya na bado akabaki na afya njema.

Mhimu ni mazoezi bila mazoezi hata hayo mafuta mazuri ukiyatumia bado hutaona faida yoyote.

Na hata wanga upo wanga wa aina mbili. Wanga mzuri na wanga mbaya.

Wanga mzuri ni ule ambao haujakobolewa, mfano wanga uliomo kwenye ugali wa sembe ni tofauti na wanga uliomo kwenye ugali wa dona.

Kadharika wanga uliopo kwenye mkate mweupe ni tofauti na wanga uliopo kwenye mkate wa ngano ambayo haijakobolewa (brown bread).

Wanga uliomo kwenye mchele mweupe ni tofauti na wanga uliomo kwenye mchele wa brown.

Kwahiyo ukikutana na mtu anakuambia usile vyakula vyenye wanga ili kuwa na nguvu za kiume anakuwa amekudanganya pakubwa sana na mhimu muombe afafanue ni wanga upi hasa anamaanisha na siyo akataze tu wanga wote kwa ujumla.

Soma hii pia > Vyakula ambavyo mwanaume hatakiwi kula

Mkate wa Brown

Kwahiyo ili kuwa na nguvu za kiume ni mhimu na lazima mwanaume ajishughulishe na mazoezi ya viungo kila siku au mara nyingi.

Tofauti na hapo hata ule nini hata utumie dawa gani sahau wewe kuwa na nguvu za kiume za kudumu.

Kwa mwanaume mazoezi ni lazima iwe una upungufu wa nguvu za kiume au upo vizuri kitandani bado unatakiwa uwe bize na mazoezi kila mara ikibidi kila siku.

Kwahiyo umhimu wa kwanza wa maoezi ya viungo kwa nguvu za kiume ni kuwa kwanza maoezi yanakuwezesha kuchoma mafuta mwilini ambayo bila mazoezi yangeendelea kujirundika mwilini na kukuletea mwili wenye uchovu na legelege.

Pili mazoezi yanauwezesha mwili kutumia mafuta kama chanzo chake cha nguvu na siyo nguvu tu bali nguvu mara 2 zaidi tofauti na kama mwili ungetumia sukari au maji na chumvi kutengeneza nguvu.

Mazoezi pia ni mhimu sana kwa mwili katika kuzuia na kutibu tatizo la msongo wa mawazo (stress).

Msongo wa mawazo ndicho chanzo kikuu cha kushuka kwa nguvu za kiume kwa wanaume wengi lakini ni tatizo linaloweza kuepukika kirahisi kama mtu atakuwa bize na mazoezi ya viungo kila siku.

Shida iliyopo wanaume wengi linapokuja suala la mazoezi hawakosi visingizio na kisingizio chao kikuu ni kukosa muda wa kufanya mazoezi!.

Ni hatari sana kuwa na wanaume wa namna hii kwenye nchi yetu.

Unakosaje muda wa mazoezi ndugu?

je muda wa kulala unapata?

je muda wa kula chakula unapata?

je muda wa kwenda bafuni kuoga unapata?

je muda wa kukaa bar au kijiweni unapiga stori na washikaji unapata?

Unashindwaje sasa kupata muda wa mazoezi dakika 30 au 40 kwa siku?

jibu ni moja tu, wewe ni mvivu na huoni umhimu wowote wa afya yako.

Mazoezi gani sasa ya viungo nifanye ili kuongeza nguvu za kiume? hilo lazima utauliza.

Jibu fupi ni mazoezi yoyote yanaweza kukusaidia kuongeza nguvu za kiume ila mazoezi ya kukimbia (jogging), kuchuchumaa na kusimama (squatting), pushup, na mazoezi ya kutembea ni mazoezi ya uhakika zaidi kwa kuongeza nguvu za kiume. 

Makala inaendelea hapo chini.

Endelea kusoma …

Faida 50 za Jumla za mazoezi mwilini:

Moja ya mahitaji matano (5) mhimu ili kuishi baada ya oksijeni, maji, chumvi, na potasiamu; ni Mazoezi.

Mazoezi ni mhimu kwa ajili ya afya zaidi ya kuwa na maumbile ya kuvutia (sex body), burudani au kitu kingine chochote.

Watu wengi hufuatilia kuhusu chakula tu, hata kama utakula vizuri vipi bila mazoezi mlo haujakamilika, kwa hiyo mazoezi ni mhimu kwa yeyote kama ilivyo kwa maji au chakula.

Faida 50 za mazoezi

Zifuatazo ni moja ya sababu 50 mhimu za kufanya mazoezi kwa afya bora na maisha marefu bila maumivu:

1. Hukufanya ujisikie vizuri
2. Huongeza uwezo wa kujifunza
3. Hujenga uwezo wa kujistahi
4. Huongeza nguvu ya ubongo kufanya kazi
5. Huuweka mwili wako kuwa unaofaa (fit) na wenye uwezo
6. Huongeza afya ya akili yako
7. Huongeza kinga ya mwili
8. Hupunguza mfadhaiko/stress
9. Hukufanya ujisikie vizuri/mwenye furaha
10. Hukufanya usizeeke mapema
11. Huweka ngozi yenye mng’aro na yenye afya
12. Husaidia kupata usingizi mtulivu
13. Husaidia kuzuia ugonjwa wa kiharusi/strokes
14. Huongeza ufanisi katika makutano/joints ya mwili
15. Huongeza nguvu za mishipa
16. Huondoa wasiwasi
17. Huongeza kumbukumbu
18. Husaidia kudhibiti ulevi/uteja
19. Huongeza uzarishaji
20. Huongeza uwezo wa ubunifu
21. Hupendezesha muonekano wa mwili
22. Huongeza uwezo wa kujiamini
23. Husaidia kuongeza nguvu juu ya malengo yako maishani
24. Huondoa tatizo la kukinaishwa na chakula
25. Huongeza miaka ya kuishi
26. Hukomaza mifupa
27. Huongeza afya ya moyo
28. Huongeza hali ya kuwa na msimamo
29. Huondoa homa ndogo ndogo mwilini
30. Huongeza hamu ya kula
31. Hudhibiti usawa wa lehemu/kolesteroli
32. Hupunguza uwezekano wa kupatwa na baadhi ya kansa
33. Hushusha shinikizo la juu la damu/BP
34. Hupunguza uwezekano wa kupatwa na kisukari
35. Huzuia kupatwa na ukichaa/uwendawazimu
36. Hupunguza au huzuia maumivu ya mgongo
37. Hupunguza uwezekano wa kupatwa na ugonjwa wa mifupa
38. Hupunguza hisia/fikra za kujisikia vibaya au huzuni
39. Huzuia kupotea kwa mishipa
40. Huongeza nguvu na ustahimilivu
41. Huongeza ufanisi katika michezo
42. Huongeza uwezo wa kuvumilia maumivu
43. Huongeza usawa na ushirikiano wa mwili
44. Huongeza usambazaji wa oksijeni katika seli za mwili
45. Huongeza hali ya ufuatiliaji/concentration
46. Huongeza uwezo wa kujitawala na kujidhibiti nafsi
47. Huondoa uchovu
48. Huongeza nguvu katika tendo la ndoa
49. Hufanya maisha ni yenye kuvutia zaidi
50. Huongeza ubora wa maisha

Ikiwa unatafuta dawa nzuri ya uhakika ya asili kwa ajili ya kuimarisha nguvu za kiume na kutibu madhara yatokanayo na punyeto niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175 

Tafadhali SHARE post hii kwa ajili ya wengine.

 

Imesomwa na watu 1,516
Kwanini mazoezi ya viungo ni mhimu sana kwa nguvu za kiume

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WhatsApp 0714800175