Last Updated on 15/03/2023 by Tabibu Fadhili Paulo
Dalili 17 za mwanamke anayechepuka
1. Kujipenda sana kunaongezeka
Dalili mojawapo kukuonyesha kwamba huenda mkeo anachepuka ni ile hali ya kuongeza Kujipenda na kujipamba sana tofauti na siku au miezi kadhaa ya kabla.
Kama ameanza kuwa msafi zaidi na kupenda kuvaa vizuri zaidi tofauti na alivyokuwa kabla basi hiyo ni dalili mambo yameanza kuwa mazuri huko nje.
2. Hatoi jibu ukimwambia NAKUPENDA
Zamani ulikuwa ukimwambia nakupenda na yeye anakuitikia nakupenda pia tena kwa haraka na tabasamu.
Ukiona ukimwambia nakupenda hakuitikii kwa haraka na kwa furaha basi ujue tayari mambo ni moto huko nje.
3. Hakutazami usoni
Zamani alipokuwa na wewe tu alikuwa anapenda kukuangalia usoni.
Jaribu sasa kumuuliza swali lolote huku ukimtazama usoni na ukiona anakwepesha macho na kupenda kuangalia chini au pembeni badala ya kuangaliana na wewe uso kwa uso basi ni dalili ameanza kuwa na bwana mwingine huko nje.
4. Amekuwa msiri ghafla
Ukiona mkeo ameanza kuwa mtu wa siri siri nyingi, hataki ujue mambo mengi kuhusu yeye, ukikaribia simu yake au computer yake anaanza kuhamaki, ujue tayari manyoya!
Hii ni moja kati ya dalili za wazi wazi za mwanamke aliyeanza kuchepuka.
5. Anaanza kukukosoa na kuongelea madhaifu yako
Kawaida mwanamke akikupenda na akiwa yupo na wewe tu haoni kasoro au udhaifu wako kirahisi.
Unaweza kuwa ulimuoa ukiwa ni mtu unayekunywa pombe na yeye hanywi lakini bado alikuwa haoni shida yoyote ila mara tu alipopata bwana mwingine huko nje anaanza kuona tabia yako ya kunywa pombe ni jambo baya na linalokera.
Hapa nimetolea mfano wa pombe lakini kuna mengine zaidi ambayo alikuwa anakuvumilia na kuona ni ya kawaida lakini sasa ataanza kukusema kwamba ulivyo hivi mimi sipendi ingawa mwanzo wala hakuona shida yoyote kwenye hayo.
Uonapo haya basi ujue tayari amepata mtu huko anayemshika masikio.
6. Anaanza kukataa kuonekana kwenye vikao au matukio ya kifamilia
Dalili nyingine ya mwanamke anayechepuka ni kuanza kukataa kuonekana kwenye matukio au mikutano ya kifamilia.
Kama mlikuwa na kawaida ya kutoka kila jumamosi familia nzima kwenda baharini au mtoni kuogelea kwa pamoja basi sasa ataanza kuleta visingizio ili tu msiwe karibu na yeye apate muda wa kufanya yake.
7. Anaweza kuhamia kulala chumba kingine tofauti na chumbani
Ukiona mkeo anapenda kulala chumba kingine tofauti na chumbani kwenu au anahamia chumba cha watoto hiyo ni ishara anakusaliti na hivyo ile hamu ya kuwa na wewe tena masaa mengi imeanza kupungua
Mwingine anaweza kuanzisha ugomvi kila inapofika muda wa kulala ili tu mzozane apate nafasi ya kwenda kulala chumba kingine mbali na wewe.
8. Muda mwingi ana hasira na wewe
Yaani ghafla tu hana amani kuwa karibu na wewe.
Utani mdogo tu ukimtania atakukasirikia sana tofauti na siku za nyuma.
Jambo dogo tu la kawaida ambalo zamani mliishia kucheka tu sasa linageuka kuwa kubwa na kuzua ugomvi na maneno mengi.
Hacheki kirahisi tena awapo na wewe, basi ujue tayari manyoya!!
9. Nafsi yako inaanza kuwa na mashaka
Ingawa wengi wetu siyo wazuri kwenye kuzisikiliza nafsi zetu zinapojaribu kutuambia jambo fulani lakini safari hii wewe mwenyewe utaanza kuhisi na kuona kuna kitu siyo sawa kwenye ndoa yenu.
Ukiona hali hii inakujia mara kadhaa nafsini mwako basi ujue ni kweli kuna uwezekano mkeo ameanza kupoteza uaminifu.
Jambo la mhimu hapa ni kwamba bado huwezi kufanya uamuzi wowote kwa hisia tu bila kuwa na uthibitisho kamili.
Lakini ukiona umeanza kuingiwa na mawazo haya ni mhimu kufanya uchunguzi zaidi.
10. Matumizi ya hela yanaongezeka
Moja ya dalili nyingine itakayokuonyesha kuwa mkeo anachepuka ni kuona kuongezeka kwa matumizi ya hela.
Mbaya zaidi hela hizi anazotumia hujampa wewe na hazijulikani zinatoka wapi.
Wapo wanawake unaweza kukuta ameshanunua kiwanja na mwingine hadi kujenga tayari amejenga na hajawahi kukujulisha chochote!
Unashangaa mara tu ana simu kali ya bei kubwa ukimuuliza anakuambia nimeuza ile nilikuwa nayo nikaongeza kahela kidogo nikanunua hii nyingine.
Ukichunguza simu uliyomnunulia kabla ni ya laki 2 lakini sasa anayo ya laki 8 na anakuambia hii inagharimu laki 2 na elfu 50 tu.
Ukiona mambo kama haya ujue tayari manyoya!
11. Kugombana na mizozo haviishi
Ukiona sasa kugombana na mizozo ya hapa na pale haipungui kwenye nyumba yenu ujue tayari mambo mazuri huko nje.
Zamani mlikuwa mnakaa hata miezi mitatu hamjanuniana hata mara moja lakini sasa wiki haipiti lazima mgombane na kuzozana, ujue tayari.
Ni ishara uvumilivu juu yako hakuna tena na kuna mtu huko nje anampa kiburi na kujiamini.
12. Sherehe hazipungui upande wake
Sherehe zimeongezeka sana upande wake na mara nyingi hatoki na wewe.
Wiki hii atakuambia kuna kitchen party ya rafiki yake, wiki inayofuata kuna sherehe ya kuzaliwa ya rafiki yake, wiki inayofuata kuna sherehe ya wana vikoba wenzake nk nk yaani kila wiki kuna sherehe sehemu fulani na ni lazima ahudhurie na anatoka akiwa kapendeza kweli kweli!
Basi ujue tayari!
13. Kujitegemea kunaongezeka
Ukiona mkeo sasa vitu vingi anafanya mwenyewe bila kukushirikisha au kukuomba ushauri basi ujue tayari!
Hahitaji tena umpitie kazini umrudishe nyumbani, hataki mfanye kazi pamoja hata za nyumbani, mambo mengi anaamua mwenyewe bila uwepo wako ujue tayari amepata mwingine.
Ukiona anaonyesha dalili kwamba anaweza yote bila wewe basi tambua tayari kuna mtu anamshika masikio huko nje.
14. Hataki kujua mengi kuhusu wewe mmewe
Ukiona mkeo haulizi tena ikiwa umekula au unajisikiaje au haulizi chochote kuhusu afya yako ikiwa unaumwa au la
Yaani ukiona hataki kufahamu lolote kuhusu wewe, haoni umhimu wowote wa kukupikia chakula na majukumu yote amemuachia Dada wa kazi basi tambua tayari!
Hapendi kuongea ongea na wewe hata mnapokuwa pamoja, hakutambulishi tena kwa ndugu wengine na marafiki, hapendi tena kupiga picha na wewe, basi ujue tayari.
15. Yupo bize na simu
Mnaweza kuwa mmeingia kulala kitandani mme ukapata usingizi lakini yeye yupo bize na simu hadi usiku wa manane, basi ujue tayari!
Mwanamke anayekupenda wewe peke yako hawezi kubaki na simu na kukuacha wewe ukilala usingizi.
16. Hakupi tena tendo la ndoa kama zamani
Zamani ukimuomba anakupa wakati wowote na nyakati zingine yeye ndiye anaweza kukukumbusha kwamba anahitaji.
Lakini ghafla mambo yanabadilika, ukimuomba hakosi visingizio mara leo naumwa tumbo, mara leo nipo kwenye siku zangu, mara leo sijisikii vizuri yaani hakosi sababu ya kukunyima huduma ya kitandani, basi ujue tayari.
Ukiona umeanza kupangiwa ratiba za tendo la ndoa ujue tayari kuna mtu anapewa huko nje na wakati mwingine anatunziwa kabisa kwa kunyimwa wewe wa ndani.
Ukiona mkeo hana ushirikiano kitandani kama mwanzo, mwanzoni alikushika mwili wako kwa furaha na kukukumbatia lakini sasa hataki na hata akikupa hana ushirikiano wowote na anakuhimiza umalize haraka ili alale, basi ujue tayari.
17. Kazi nyingi ofisini
Zamani akimaliza tu kazi au biashara yake atakimbia haraka nyumbani
Sasa mambo ni moto badala ya kazini kutoka saa kumi sasa anatoka saa kumi na mbili au hata saa mbili kwa kisingizio boss amemuongezea kazi nyingine za ziada.
Kazi hadi siku za weekend, kila weekend ana safari fulani sehemu fulani tena bila wewe na anatoka amependeza sana, basi ujue tayari.
Mwanamke mwaminifu lazima aheshimu muda wa kazi na muda wa nyumbani na familia.
Ukiona yupo bize sana na kazi kuliko alivyo bize na familia na kuwa nyumbani, basi ujue tayari.
Hitimisho:
Mwanamke kuchepuka kunaweza kutokea kama sababu ya wewe mme wake kutokuwa naye makini au inaweza kutokea tu kama matokeo ya vishawishi na maamuzi yake binafsi.
Kwa vyovyote itakavyokuwa Kumbuka hizi ni dalili tu na bado huwezi kufanya uamuzi wowote bila kuwa na uhakika na uthibitisho wa wazi kwamba kweli mkeo amepoteza uaminifu.
Na yote katika yote Kumbuka kutunza amani huku ukijipa moyo kwamba haijalishi unapitia nini muda ukifika hilo nalo litapita!
Mkeo kuchepuka haina maana ndiyo mwisho wa dunia kwako, bado unatakiwa kutunza amani na ukiwa na uhakika kweli kwamba anachepuka na huwezi kumsamehe na yeye mwenyewe hawezi kubadilika basi unaweza kumuacha kwa siri bila ugomvi wala shida yoyote huku ukiruhusu maisha mengine yaendelee.
Je wewe ni mwanaume na unahitaji dawa ya asili ya kuimarisha nguvu za kiume na kutibu madhara yatokanayo na punyeto? Kama ndiyo niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175.
Tafadhali SHARE post hii kwa ajili ya wengine uwapendao.