Dalili kuu 5 zitakazokuonyesha unapungukiwa nguvu za kiume

Last Updated on 21/03/2022 by Tabibu Fadhili Paulo

Dalili kuu 5 zitakazokuonyesha unapungukiwa nguvu za kiume

Unazifahamu dalili za kukuonyesha kuwa unapungukiwa au una tatizo la upungufu wa nguvu za kiume?.

Kwenye mwili wa binadamu kuna mambo mengi ambayo hatuyaelewi na mara nyingi huwa hatuna muda wa kuyapeleleza.

Kwahiyo unapojihisi huenda kuna kitu siyo sawa kwenye afya yako ya kitandani huo ndiyo wakati wa kujaribu kuona kama yanayokutokea ni dalili za kupungukiwa nguvu za kiume au la.

Dalili hizo zinaweza kukusaidia kufahamu ikiwa shida iliyokutokea kitandani mara ya mwisho ni jambo la kupita tu au umekuwa ukiumwa muda mrefu bila kujua.

Kufahamu dalili hizi kutakusaidia katika mipango yako ya kurudi kwenye stamina yako kama zamani.

Je zipi ni dalili za kupungukiwa au kuishiwa nguvu zako za kiume?

Ukweli ni kuwa kila mwanaume, narudia tena KILA MWANAUME haijalishi ni nani mara moja moja katika kuishi kwake atatokewa na hali isiyoeleweka ya uume wake kugoma kusimama vizuri, ni jambo la kawaida kabisa.

Inaweza kukutokea mara moja na kupotea.

Bali kama linakuwa ni jambo linalokutokea mara nyingi na kwa kipindi kirefu mfululizo labda ndani ya miezi 6 na kuendelea, basi ni wazi kuna kitu si sawa kwenye afya yako ya uume na ni dalili unapungukiwa nguvu zako za kiume.

Mara nyingi kwenye tovuti hii nimeeleza jinsi tatizo la kupungukiwa nguvu za kiume linavyoweza kuwa ni sababu ya afya mbovu ya mwili au ya akili.

Dalili zitakazokuonyesha unapungukiwa nguvu za kiume ;

1. Kuishiwa au kukosa hamu ya kutaka kushiriki tendo la ndoa

Ni jambo la kawaida kwa mtu kutojisikia hamu ya tendo la ndoa kwa siku 1 au mbili ndani ya mwezi.

Lakini kama hujisikii kabisa hamu ya tendo la ndoa kwa kipindi kirefu mfululizo na unaishi na mke ndani kuna uwezekano mkubwa umeanza kupungukiwa nguvu za kiume na ni wakati mzuri kuanza kujipeleleza zaidi.

2. Uume unakuwa mlegevu wakati wa tendo la ndoa

Dalili nyingine ya kuanza kupungukiwa nguvu zako za kiume ni uume wako kuwa mlegevu wakati wa tendo la ndoa.

Kama ni jambo linalokutokea na kujirudia mara kwa mara ni dalili unapungukiwa nguvu zako za kiume.

Kawaida mwanaume anapokuwa na mwanamke chumbani na anataka kushiriki tendo la ndoa uume wake lazima usimame vizuri na uwe mgumu siyo legevu legevu.

Uume unatakiwa uwe umesimama na ni mgumu kiasi cha mwanamke kuogopa kidogo.

Kama unakuwa na uume mlegevu na unapata shida kutaka uume usimame au unapata tabu hata kuingia ukeni na ni jambo linalotokea mara kwa mara, basi ni wazi umeanza kuishiwa nguvu zako za kiume.

3. Kukosa hisia kwenye uume

Kwenye uume kuna miishio mingi ya neva mbalimbali na hivyo unapoingia kwa mwanamke lazima upate hisia nyingi kwenye uume (sensations) na ndiyo sababu ya tatizo la kuwahi kufika kileleni.

Kama unatokewa na hali ya kutokuhisi chochote kwenye uume wako wakati unaendelea na tendo la ndoa ni dalili unapungukiwa nguvu za kiume.

Yaani uume unakuwa kama vile umepigwa ganzi. Ni hali inayotokea kama vile umepaka dawa ya asili ya kusaidia kuchelewa kufika kileleni (vumbi la Kongo).

4. Kuanza kuona hakuna sababu ya kushiriki tendo la ndoa

Hapa mwanaume anaweza kuacha kabisa habari ya kuwa na mwanamke.

Kama hajaoa basi hata kuwa na mpenzi au Mchumba hataki tena.

Hataki kuwa kwenye mahusiano yoyote ya kimapenzi kwa hofu kwamba hatamridhisha mwanamke na hivyo ili kuondoa aibu hiyo ni bora abaki peke yake.

Mwanaume anaanza kuwakwepa na kuwaogopa wanawake.

Kama ana Mchumba basi kila mara mchumba atakapohitaji waonane yeye atakuwa na sababu nyingi za kukataa mwaliko huo kwa madai yupo bize, ana kazi, ana safiri, anaumwa na mengine mengi ilimradi tu asishiriki tendo la ndoa.

5. Kuwahi sana kufika kileleni na kukosa uwezo wa kurudia tena tendo

Kama unatokewa na hali ya kuwahi kufika kileleni kila mara kwa kipindi kirefu na unakosa nguvu ya kusimama na kuendelea tena mara ya pili basi ni wazi unapungukiwa nguvu zako za kiume.

Hata hivyo kurudia tena tendo la ndoa mara ya pili au ya tatu siyo dalili kwamba una nguvu za kiume.

Siyo lazima kurudia mara ya pili.

Unaweza kufanya mara moja tu na ikawa imetosha na mkeo akalala usingizi hasa kama hukuwahi kufika kileleni lile la kwanza.

Kama goli moja tu la kwanza linachukuwa muda mrefu labda dakika 15 au 20 au dakika 25 basi siyo lazima urudie mara nyingine kwani ni wazi mkeo atakuwa na yeye amefika tayari kileleni na kutosheka.

Ila kama unawahi sana kufika kileleni bao la kwanza basi unawajibika kurudia tena ili uweze kumfikisha mwenzako.

Lakini kama kila mara unawahi sana kufika kileleni, yaani ukiweka tu tayari wazungu hao ndani ya dakika 3 au 5 na huwezi kurudia tena kwa haraka na ukadumu muda mrefu ni dalili ya wazi umepungukiwa nguvu zako za kiume.

Upungufu wa nguvu za kiume ni jambo linalotibika na kupotea.

Lakini nasisitiza watu kutokupenda njia za mkato au njia rahisi rahisi katika kutatua tatizo hili.

Kuna watu hukimbilia kumeza vidonge vya kizungu kama vile viagra, erecto na vidonge vingine kama hivyo ili kupata suluhisho la haraka.

Tatizo ni kuwa hilo si suluhisho la kudumu, ni suluhisho la muda mfupi tu na hukuacha na madhara mengine ya kiafya hapo baadaye.

Baba mmoja alinitafuta siku moja kutaka msaada wa tatizo hili na akaniambia mwanzoni alikuwa anaona kama ni utani, alikuwa akimeza kidonge kimoja mambo yanakuwa vizuri lakini siku zilivyoenda akajikuta analazimika kumeza vidonge mpaka vinne ndiyo mheshimiwa asimame na baadaye ikawa hata akimeza vidonge hawezi kusimama tena hata mkewe akae bila nguo yoyote mbele yake bado hasisimki chochote.

Usipende njia za mkato kwenye mambo ya mhimu kama hili.

Kama upo Dar Es Salaam fanya mpango tuonane tuongee kwa kirefu uso kwa uso.

Hakuna sababu ya kuwa na aibu, mimi nipo tayari kukusaidia kuondokana na tatizo hili kwa kutumia dawa za asili zisizo na madhara yoyote mabaya leo wala kesho na ni za hapa hapa Tanzania naziandaa mwenyewe kwa kutumia mikono yangu na ni za kutumia kwa kipindi kirefu zikishughulika na mwili wako wote kwa ujumla na siyo uume peke yake.

Tuwasiliane kwenye WhatsApp +255714800175

SHARE post hii na wengine uwapendao

Imesomwa na watu 641
Dalili kuu 5 zitakazokuonyesha unapungukiwa nguvu za kiume

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WhatsApp 0714800175