Dalili za mwanamke anayetaka kushiriki tendo la ndoa

Last Updated on 18/05/2023 by Tabibu Fadhili Paulo

Dalili za mwanamke anayetaka kushiriki tendo la ndoa

Shida moja kubwa iliyopo upande wa wanawake hasa wanawake wa Afrika ni kuwa kwao suala la tendo la ndoa ni suala la mwanaume.

Jamii hapa Afrika zimempa mamlaka yote kuhusu tendo la ndoa mwanaume.

Mwanaume ndiyo anapaswa kumtongoza mwanamke, na ndiyo atahitajika kila mara kuanzisha habari ya mechi kitandani.

Hata kama mwanamke ana hamu siku hiyo bado kitendo cha kumwambia mmewe au mchumba wake kwamba leo nataka huonekana kama ni jambo gumu sana.

Kumbe mwanamke mzungu haoni shida yoyote kumwambia mwanaume nimekupenda na natamani tuwe wachumba au tuoane, haoni tabu yoyote kumwambia mmewe leo nahitaji tendo la ndoa.

Kwa huku kwetu Afrika bado wanawake wanatumia ishara kupeleka ujumbe kwa waume au wachumba zao.

Kama mwanaume napenda kukushauri kuwa usiache kumwambia mkeo kwamba siku ukihitaji usione shida wala usiogope kuniambia.

Kama utamfanya mkeo kuwa ni rafiki yako wa karibu na siyo mama ya watoto wako basi pia itampa ujasiri wa kukuambia wazi mara kadhaa kwamba leo nahitaji.

Basi kwenye makala hii nimekuwekea dalili na ishara anazozionyesha mwanamke anayetaka kushiriki tendo la ndoa na wewe siku hiyo ;

1. Anavaa nguo nzuri sana za mitego

Kama mme umerudi nyumbani jioni au usiku na ukakuta mkeo kavaa nguo nzuri sana hasa kama ni nguo za rangi nyekundu au nyeupe na ni za kitambaa chepesi sana kiasi cha kukaribia kuonekana mwili wake, basi ujue anataka.

Kama amevaa kweli kweli tofauti na siku zingine, amepaka rangi mdomoni na pengine ameweka na makeup basi ujue siku hiyo anahitaji huduma kutoka kwako.

Ukaona kajipuliza na marashi mazuri (perfume) ya kuvutia, basi jiongeze tu kwa kumwambia twende chumbani tukaangalie taa zinavyowaka vizuri.

Hapa hata kama utamuuliza mbona leo hivi bado hawezi kukuambia ukweli lakini wewe jiongeze.

2. Anakushika na kutaka kugusana na wewe

Kama upo sebuleni au hata chumbani anaweza kukufuata na kutaka kukugusa au kukushika sehemu kadhaa kwenye mwili wako.

Anaweza kuja juu ya miguu yako na kukukalia kabisa.

Kama ujuavyo wanawake wengi ni waoga na wenye aibu sana kusema wazi kwamba wanahitaji tendo la ndoa na hivyo uonapo dalili hizi ujuwe tayari siku hiyo mwenzako anahitaji huduma.

Kama mmelala kitanda kimoja cha kwanza atataka kugusanisha miguu yake na yako, anaweza pia kuja kulala kifuani mwako.

Ndugu yangu mwanaume uonapo dalili hii kamwe usifanye makosa, mpe haraka mtoto wa watu kile roho yake inahitaji.

3. Atakufanyia jambo moja zuri analojua unalipenda

Kwa kawaida kwenye mahusiano ya ndoa siyo kila siku mwenza wako anakuwa na hamasa ya kukufanyia jambo zuri la kukushangaza.

Lakini siku ikitokea ana hamu ya kutaka kushiriki tendo la ndoa na wewe basi ukirudi lazima ukute amekuandalia jambo moja zuri sana la kukushangaza hasa lile analohisi unalipenda.

Mfano kama anajua siku za mapumziko (weekend) huwa unapenda kunywa mvinyo mwekundu (red wine) basi usishangae siku hiyo kukuta amekununulia chupa ya wine na kuweka mezani chumbani na glasi zake.

Ukiona hivyo ndugu yangu wewe sema ahsante sana mke wangu, fungua chupa kunywa na kama na yeye huwa anapenda kunywa mpe na yeye glasi yake mnywe na mkimaliza tu usichelewe kumpa haki yake.

Kama ni mpenzi wa kula chakula fulani na anajua basi siku hiyo lazima atajitahidi akuandalie chakula hicho na mara nyingi atakutengea chumbani.

Kuna vitu vingi anaweza kufanya ili kukusisimua na kukushangaza zaidi ya hiyo mifano miwili niliyotoa, wewe fuatilia tu na kuwa makini.

Dalili za mwanamke anayetaka kushiriki tendo la ndoa

4. Anakuomba muangalie pamoja video za wakubwa

Ukiona ni muda mrefu umepita na hamjaangalia video yoyote ya wakubwa na ghafla tu ukasikia naomba kuangalia video hizo au kama anazo tayari kwenye simu yake au computer yake na akakutaka muangalie basi ujue tayari mashetani yamempanda na kazi ni kwako.

Kwa kawaida wanandoa wenye akili na wanaojitambua hawaangalii mara kwa mara wala kuziweka karibu video za namna hii.

Hata hivyo mara moja kwa miezi miwili au mitatu au mara 4 kwa mwaka kuziangalia pamoja na mwenza wako hazina madhara yoyote mabaya.

Zitawaletea shida na kuharibu ndoa yenu kama mnazo muda wote kwenye simu zenu na mnazitazama mara kwa mara.

Nitaeleza siku nyingine faida ya mme na mke kutazama video za wakubwa mara moja moja kwenye uhusiano wenu.

Kwahiyo ukiona miezi imepita hamjaangalia picha hizo halafu ghafla akakuambia leo nataka kuangalia ujue tayari yupo tayari anakuhitaji kitandani.

Picha hizi ni kama vile ukimwi kila mtu anasema hana, ni kama vile bangi kila mtu anakataa hatumii lakini watu wote hata wale usiowadhania wanaziangalia pia.

5. Ukiona anakukumbusha kwamba ni muda mrefu sana tangu mliposhiriki tendo la ndoa

Ukiona mkeo anakuambia ni siku nyingi zimepita tangu mmeshiriki tendo la ndoa ujue anakukumbusha kwamba leo tena anahitaji.

Ukiona anasema siku 7 sasa zimepita au siku 10 sasa zimepita ujue na leo yupo tayari anakutaka na ni jukumu lako kujiongeza.

Na hii ni hali inayotokea sana kama baba ni mtu wa kusafiri safiri na upo bize sana basi lazima atajidai anakukumbusha kwamba siku nyingi zimepita hamjashiriki, lengo lake hapo ni kusema nahitaji sasa au nahitaji leo na ni jukumu lako baba kutimiza wajibu wako kumbeba na kumpeleka kitandani akalale.

6. Muda mwingi anazungumza kuhusu mapenzi

Hii nayo ni dalili nyingine kwamba mkeo leo damu imepamba moto.

Ukiona siku hiyo muda mwingi anapenda kuzungumza kuhusu mapenzi na tendo la ndoa ujue anataka wewe uiendeleze hiyo mada na mwisho wa siku umpe haki yake ya kitandani.

Wanawake ni wachokozi sana, ukiona anakuuliza kama unapenda avae shanga kiunoni au anakuuliza kama nguo yake ya ndani ni nzuri basi siku hiyo yupo tayari na unatakiwa usifanye kosa la kushangaa shangaa tena maghorofa, wewe mchukuwe mtoto wa watu kamlaze kitandani mpe anachopenda.

7. Mapaja yake anaacha wazi

Hii ni mbinu ya zamani sana wanawake wamekuwa wakiitumia kufikisha ujumbe kwa waume zao au kuwatega wanaume wanaowataka.

Ni rahisi tu, siku hiyo atavaa nguo fupi sana ambayo sehemu kubwa ya mapaja yake yanaonekana.

Kama ndani ya nyumba hiyo hakuna watu wengine au watoto basi anaweza kuja kukaa mbele yako kuacha uwazi fulani unaoweza kuonyesha hata nguo yake ya ndani.

Anafanya hayo yote kwa mapenzi mema tu kwako na lengo lake ni kukuamsha kihisia ili hatimaye umbebe mgongoni uende naye chumbani kuangalia namna taa zinavyowaka vizuri.

Kama mwanaume unapaswa kuwa mfuatiliaji na mwelewa wa ishara hizi.

Ukiacha ishara hizi hapa chini napenda nikuandikie baadhi ya nyakati ambazo kwa asili mwanamke huwa anapandwa sana na hisia na matamanio ya kutaka kushiriki tendo la ndoa.

Ndani ya nyakati hizi hata kama hata kuonyesha dalili zozote za kutaka kushiriki tendo la ndoa lakini ukimuomba ndani ya nyakati hizi ni vigumu sana kukunyima sababu ni nyakati kwa asili yeye mwenyewe anakuwa anahitaji sana kushiriki tendo la ndoa;

Nyakati hizo ni hizi zifuatazo :

1. Wakati ambapo anaachilia mayai yake (ovulation days)

2. Mwezi wa nne baada ya kupata ujauzito

3. Wakati akiwa kwenye siku zake

4. Wakati siku zake zinapokaribia kukoma (menopause)

Kama wewe ni mwanaume na unahitaji dawa ya asili ya kuimarisha nguvu za kiume pengine na kutibu madhara yatokanayo na punyeto niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175.

Jina langu ni Fadhili Paulo, ni Tabibu wa Tiba asili, ofisi yangu inaitwa TUMAINI HERBAL LIFE ipo Kibugumo Mji Mwema Kigamboni Dar Es Salaam.

Imesomwa na watu 101
Dalili za mwanamke anayetaka kushiriki tendo la ndoa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WhatsApp 0714800175