Last Updated on 29/11/2021 by Tabibu Fadhili Paulo
Hasara inayoweza kutokea mke anapoishiwa hamu ya tendo la ndoa mara kwa mara
Nakusalimu kwa jina la jamhuri ya muungano wa Tanzania …
Ni matumaini yangu umzima na unaendelea na kazi na majukumu yako ya kujenga maisha yako na taifa kwa ujumla.
Leo tena nimepata muda na nimeona niliongelee hili nalo.
Nataka upate kufahamu ni hasara kiasi gani anaweza kuipata mme ikiwa mke wake anayeishi naye ana tatizo la kukosa au kuishiwa hamu ya tendo la ndoa mara kwa mara au kwa muda mrefu mfululizo.
Huwa inatokea kwenye maisha ya ndoa inafika mahali mke anakosa hamu ya tendo la ndoa, hana hamu na mmewe yaani hajisikii kabisa kufanya tendo la ndoa.
Inawezekana ikawa ni jambo lililo nje ya uwezo wake huyo mwanamke au inawezekana ni jambo analolipanga tu mwenyewe kwa maksudi kwa maslahi yake binafsi.
Ni kawaida kwa hali hii kutokea kwa wanandoa baada ya miaka kadhaa ya kuishi pamoja.
Ni nadra sana ukute watu wameoana ndani ya mwaka mmoja au miwili au mitatu na ukutane na mgogoro wa namna hii ndani ya ndoa.
Ni hali inayotokea baada ya miaka kadhaa ya wawili hao kuishi pamoja.
Sababu za mwanamke kuishiwa au kukosa hamu ya tendo la ndoa ni nyingi na unaweza kuzisoma zote kwa kubonyeza tu hapa.
Vyovyote itakavyokuwa ifahamike kuna hasara itatokea upande wa mwanaume endapo atakutana na tatizo kama hilo kwa mke wake.
Tatizo la mwanamke kukosa hamu ya tendo la ndoa linaweza kuisha kwa majadiliano ya kina na ya kiutuuzima baina ya mme na mke au kwa msaada wa daktari wa masuala ya saikolojia na mahusiano.
Narudia tena; tatizo hilo linaweza kuisha kwa majadiliano ya kina, siyo kwa sms mbili au tatu za WhatsApp.
Kwa jicho la haraka haraka unaweza kufikiri labda ni tatizo dogo tu na ni la kawaida.
Ila kama una macho makubwa na akili iliyotulia hilo siyo tatizo dogo na linaweza kugharimu pesa nyingi na muda mwingi sana usipokuwa makini.
Sasa ukiniuliza mimi ni hasara kiasi gani inaweza kutokea pale mkeo anapokuwa na tatizo la kukosa hamu ya tendo la ndoa; Jibu la haraka ni kuwa hiyo hasara haiwezi kufikirika, ni kubwa kiasi kwamba siwezi kuisema.
Ingekuwa ni hasara ya kama bilioni 2 ningesema, ingekuwa ni hasara ya kama tilioni 3 ningesema lakini tatizo ni kuwa hasara yake ni kubwa mno kiasi kwamba ni vigumu kuisema.
Kumbuka tendo la ndoa ni sehemu ya mahitaji ya mhimu kwa mwanaume ili awe na akili timamu, ubongo uliotulia na ili aweze kufanya kazi zake kwa ufanisi na ubora wa hali ya juu.
Tendo la ndoa kwa mwanaume siyo anasa au starehe kama watu wengine wanavyodhani, ni hitaji lake la mhimu kama ilivyo chakula ili aweze kufanya kazi zake zingine vizuri.
Ndiyo maana mwanaume yupo tayari hata kununua mwanamke anayejiuza ili tu akapunguze uzito.
Lingekuwa ni jambo la kawaida tu na ni hitaji la kawaida tu hakuna mwanaume angejitoa ufahamu hata kwenda kununua malaya; ila inawabidi kufanya hivyo kuliko kupiga punyeto kwa sababu punyeto ina madhara zaidi kiafya.
Kwa hiyo ili kupata picha kidogo juu ya hasara kiasi gani mwanaume anaweza kuipata pale mke wake anapokuwa na tatizo la kuishiwa au kutokuwa na hamu ya kushiriki tendo la ndoa ni kuangalia ni gharama kiasi gani aliingia ili kumpata hata kumuoa na kumhudumia huyo mke kwa miaka kadhaa.
Fikiri ni gharama ngapi aliingia huyo mme ili kuwa na wewe.
Kwanza kabisa huyo mme ana ndugu zake wa kike wengi tu.
Ana shangazi yake mmoja ana watoto wakike, ana mjomba wake ana watoto wa kike, kuna mama mdogo wake, kuna watoto wa kike wa mama mdogo wake na ndugu wengine wengi wa kike, lakini hakuweza kumchukua ndugu yoyote wa kike kati ya hao ili kuishi naye kama mke akaja kukuchukua wewe mtu mwingine kutoka familia na ukoo mwingine ili uishi naye.
Hiyo nafasi yako kama mke ingeweza kuchukuliwa na ndugu yake mwingine yoyote na hela zikaendela kubaki kwenye familia yao na ukoo wao lakini akaamua kuzileta kwenu kwenye ukoo na familia yenu.
Akapoteza muda wake kukutongoza, kukuhonga mara kwa mara, kukuposa, kukulipia mahari, kuingia gharama za harusi, kukujengea nyumba, kuhakikisha ukiumwa unaenda hospitali kwa gharama zake na kadharika na kadharika.
Lakini baada ya miaka miwili tu au mitatu tayari wewe huna ny*ge tena, kila siku ni visingizio mara sijisikii vizuri, sina mzuka, sijuwi sipo sawa, mara naumwa na sababu nyingine kibao za uongo na kweli.
Kwa hiyo ni vigumu kufahamu ni hasara kiasi gani inaweza kutokea hasa upande wa mme inapotokea mke hana hamu ya tendo la ndoa na ni jambo linalojirudia mara kwa mara.
Wapo wanaume ambao huamua kuwa na mahusiano na mwanamke mwingine wa pembeni kwa siri tunaita mchepuko na hii ni gharama nyingine mpya na inaweza kumgharimu kweli kweli na pengine akaingia mkenge wa kuitelekeza hata familia yake ya kwanza.
Wanaume wengi wenye michepuko hawafanyi hivyo kwa kujipendea au kwa tamaa bali hutokea wanafanya hivyo kwa kukosa huduma ya kutosha na sahihi kutoka kwa wake zao wa nyumbani.
Kama hiyo haitoshi wanaume wengine hufikia hatua ya kuamua kuvunja kabisa hiyo ndoa na kuanza tena upya kwa kuoa mwanamke mwingine upya na kuanza maisha mengine mapya kwa gharama nyingine nyingi sana ambazo zingeepukika endapo mke angekuwa mwelewa na hamnyimi mmewe tendo la ndoa.
Umeona?
Kama bado hujaona basi wewe ni kipofu.
Kama utapata muda soma pia hii > Madhara 10 ya kupiga punyeto kwa mwanamke
Ndiyo; wapo wanaume baada ya kuhangaika sana na mwanamke asiye na hamu na ambaye hana ushirikiano kitandani huamua kuoa upya na kuanza maisha mapya.
Sasa hapo gharama na hasara haziwezi kuelezeka.
Sababu kubwa ya gharama kutoelezeka ni kuwa hatuangalii gharama ya pesa tu kama wengine wanavyofikiri, bali tunahesabu pia na gharama ya muda aliupoteza kuwa na wewe kumbe wewe huna msaada wowote kwake.
Alikuoa ili uwe mshirika wake wa kitandani. Mambo mengine yote anaweza kufanya yeye mwenyewe au kwa kushirikiana na rafiki zake au jamaa au ndugu zake wengine au hata kwa kuajiri watu.
Hakukuoa ili uje kumpikia, kupika anaweza kupika hata mwenyewe au akaajiri mfanyakazi.
Hakukuoa ili uje kumfulia nguo, anaweza kufua mwenyewe au akanunua mashine ya umeme ya kufua nguo.
Alikuoa ili uwe mshirika wake wa kitandani. Kuna huduma mhimu sana ambayo hawezi kuipata kwa ndugu yake mwingine yoyote isipokuwa kwako wewe mkewe ndiyo maana alikuwa tayari kuingia gharama zote hizo ili kukupata.
Kuna sababu nyingi sana zinazopelekea ndoa nyingi kuvunjika lakini hii sababu ya mke kutokuwa na hamu ya tendo la ndoa ndiyo sababu namba moja ya migogoro mingi kwenye familia nyingi.
Ni vile tu ni sababu ya aibu ambayo wanaume hawawezi kuisema hadharani lakini ukiuliza viongozi wengi wa dini watakuambia kesi nyingi wanazopelekewa za wanandoa chanzo chake ni mke au mme kutokuwa na ushirikiano mzuri kitandani.
Ni ngumu sana umkute mwanaume anaenda kushtaki kwa kiongozi wake wa dini eti mkewe hapiki chakula kizuri au hamfulii nguo!
Kuna rafiki yangu mmoja amewahi kunisimulia kitu ambacho ukiambiwa huwezi kuamini. Mkewe alikuwa ana visingizio vya kutotaka kushiriki naye tendo la ndoa mara kwa mara. Anadai kuna wakati mkewe alisafiri safari ya kawaida tu kwenda kusalimia ndugu zake na alikaa huko kwa wiki mbili lakini bado tu hata baada ya kurudi mkewe alimnyima huduma kwa madai kuwa ana uchovu wa safari!
Nini kifanyike sasa ili kunusuru hii hasara ambayo haiwezi kuelezeka au kusimuliwa?
1. Mke awe mkweli ikiwa tatizo alilonalo siyo la kujitakia. Amweleze mmewe ukweli wote toka moyoni kwamba hata yeye haelewi ni nini hasa kinamfanya akose hamu ya tendo la ndoa.
Kama mke hatakuwa mkweli basi mme atajua ni jambo la kujitakia na la maksudi na pengine linatumika ili kumuadhibu yeye mwanaume.
Kama tatizo linatokana na mwanaume kutomridhisha mkewe basi mke asione aibu kumwambia hivyo mmewe kwa lugha ya adabu na staha na yenye lengo la kujenga na siyo kubomoa.
Mke awe kwenye upande wa kutaka kulitatua tatizo na siyo kuliendeleza.
2. Mme amweleze mkewe juu ya kero anazopitia kama matokeo ya yeye (mke) kuishiwa hamu ya tendo la ndoa kila mara.
Mme atapaswa kumwambia hivyo mkewe kwa lugha ya upole na upendo na asiwe na wazo la kuhukumu.
Narudia tena; ‘Mme atapaswa kumwambia hivyo mkewe kwa lugha ya upole na upendo na asiwe na wazo la kuhukumu’.
Isiwe kama vile ni vita au ugomvi bali ni majadiliano ya amani na yanayolenga kuleta amani na kutatua tatizo na siyo kuleta shida zingine zaidi.
3. Kama chanzo cha tatizo kitagundulika kuwa kipo nje ya uwezo wenu wawili, labda ni tatizo la kiafya kama vile homoni kuvurugika, msongo wa mawazo (stress) wa muda mrefu kwa mwanamke au tatizo lingine lolote la kisaikolojia itawapasa kutafuta msaada zaidi wa kitaalamu wa daktari au wa mtalaamu wa masuala ya saikolojia ya mahusiano na mapenzi.
4. Vyovyote itakavyokuwa, kuendelea kulichukulia poa hilo tatizo na kudhani ni tatizo dogo tu au kuliona ni la kawaida tu au kudhani linaweza kuisha tu lenyewe au kwa kuagiza tu dawa ya shilingi elfu kumi mtandaoni litakuja kuwagharimu sana huko mbeleni.
Kama wewe ni mwanamke na unatafuta dawa ya asili inayoweza kukutibu tatizo lako la kukosa hamu ya tendo la ndoa niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175.
Kumbuka; nimeandika nitafute WhatsApp.
Share post hii na rafiki zako wengine uwapendao
Hasara inayoweza kutokea mke anapoishiwa hamu ya tendo la ndoa mara kwa mara Share on X