Last Updated on 14/05/2023 by Tabibu Fadhili Paulo
Je kushiriki tendo la ndoa mara nyingi kunaongeza furaha zaidi?
Je wanandoa wanatakiwa kushiriki tendo la ndoa mara ngapi kwa mwezi ili kujihakikishia uhusiano mzuri na wenye furaha?
Sisi sote tunaweza kukubaliana kwamba tendo la ndoa ni moja ya kitu mhimu sana kwenye mahusiano.
Inaonyesha kunaweza kuwa na ukweli kiasi fulani juu ya uhusiano wa kushiriki tendo la ndoa na kiasi cha furaha anachoweza kuwa nacho mtu katika mahusiano ya ndoa.
Hata hivyo ukweli na uhalisia mara zote ni vitu viwili tofauti.
Kwa hiyo swali lenyewe ni; ‘Je kuna uhusiano wa kiwango cha furaha anachoweza kuwa nacho mtu kama matokeo ya kushiriki mara nyingi tendo la ndoa kwenye ndoa au mahusiano yake?’.
Tafiti mbalimbali zinasema kushiriki tendo la ndoa mara kwa mara kuna faida nyingi za kiafya ikiwemo :
- Kuimarisha kinga ya mwili,
- Kuweka sawa shinikizo la juu la damu,
- Kupunguza shambulio la moyo,
- Kupata usingizi mzuri,
- Kupunguza msongo wa mawazo,
- Kuimarisha uwezo wako wa kumbukumbu,
- Kuongeza uundwaji wa seli mpya kwenye ubongo
- na kadharika.
Utafiti mmoja kutoka chuo kikuu cha Harvard hata ukagundua kwamba kushiriki tendo la ndoa mara 21 kwa mwezi kunaweza kupunguza hadi asilimia 20 ya kupata saratani ya tezidume.
Kabla sijalijibu swali hili la leo la ikiwa kushiriki tendo la ndoa mara nyingi kunaweza kukufanya mwenye furaha zaidi au la, napenda nikukumbushe msemo mmoja maarufu sana duniani na ambao kila mtu anaukubali.
Msemo wenyewe unasema; ‘KITU CHOCHOTE KIKIZIDI KINA MADHARA’
Too much of anything is harmful
Je wewe ni mwanaume na umekuwa ukisumbuliwa na tatizo la kuwahi sana kufika kileleni kwa muda mrefu? Kama jibu ni ndiyo pata suluhisho la tatizo lako kwa kubonyeza HAPA.
Hata wali ni mtamu lakini ukila kila siku na mara nyingi una madhara. Unaweza kuongezeka sana uzito, unaweza kuugua ugonjwa wa bawasiri na matatizo mengine ya kiafya.
Kwa hiyo bila shaka tayari umeshapata jibu la swali letu la leo.
Ni hivi; pamoja na faida zote za kushiriki tendo la ndoa unazoweza kuzipata ambazo nimeziorodhesha hapo juu, bado kushiriki tendo la ndoa mara nyingi hakuwezi kukuongezea zaidi kiasi chako cha furaha.
Kwa hiyo kadri unavyoshiriki mara chache lakini mara kwa mara ndivyo furaha yako inavyoweza kuongezeka.
Wataalamu wa masuala ya mapenzi na tendo la ndoa (sexologists) wanasema watu wanaoshiriki tendo la ndoa mara 2 mpaka 3 kwa mwezi wanaweza kuongeza kiasi chao cha furaha kwa asilimia 33, wale wanaoshiriki mara 4 kwa mwezi wanaweza kuongeza kiasi cha furaha yao mpaka asilimia 55.
Kingine kitakachokushangaza ni kuwa imebainika wazi kwamba wale wenye wapenzi wengi wana kiasi kidogo sana cha furaha kwenye maisha yao.
Kwa mjibu wa utafiti wa Tim Wadsworth mtaalamu wa masuala ya mapenzi kutoka chuo kikuu cha Colorado Marekani ni kuwa mtu yeyote mwenye mpenzi mmoja ana kiasi kingi zaidi cha furaha kuliko yule mwenye wapenzi wawili, watatu au zaidi na hili limekuwa wazi zaidi kwa upande wa wanaume.
Je kushiriki tendo la ndoa mara nyingi kunaongeza furaha zaidi? Share on XKabla hujaondoka soma na hii ?
Je wanawake huwa wanataka mwanaume adumu muda gani kitandani