Je madhara ya punyeto hupotea baada ya muda gani

Last Updated on 02/11/2021 by Tabibu Fadhili Paulo

Je inachukua muda gani madhara ya punyeto kupotea

OK ok

Hili ni swali nimekuwa nikiulizwa mara kadhaa na wanaume huko WhatsApp

Nafikiri leo utapata jibu sahihi na la kueleweka zaidi kuhusu swali hili.

Moja ya tabia ya mtu anayependa kujichua au moja ya tabia ya mtu anayepiga punyeto mara nyingi huwa ni tabia ya kupenda vitu vya haraka haraka.

Yaani anaona kwenda kumtongoza mwanamke ni kazi ngumu na inachukua muda na process nyingi, hivyo kuliko kwenda kumbembeleza mwanamke na kusubiri majibu, ni bora tu ajichue haraka na maisha yaendelee.

Hii ni tabia mbaya watu wengi wanaopiga punyeto wanayo.

Tabia ya kutaka vitu vitokee kwa haraka haraka.

Watu wengi siku hizi hawana subira kwa mambo mengi na wanataka wapate kila kitu kwa haraka na ikiwezekana leo leo!

Kwa bahati mbaya maisha hayapo hivyo na kuna vitu ni vema kusubiri na kuwa mvumilivu.

Zamani tulikuwa tunaandika barua tunapeleka posta na kusubiri majibu wiki mbili hata mwezi.

Baada ya maendeleo kwenye sekta ya mawasiliano siku hizi tunazo simu na watu wanataka majibu ya haraka haraka hata kwenye mambo ya mhimu ambayo hayawezi kutatulika kwa haraka haraka.

Sasa unajua kabisa umepiga punyeto kwa muda mrefu miaka mitatu, miaka mitano au miaka kumi na unataka dawa au suluhisho la kutibu madhara hayo ya miaka kwa wiki mbili!

HAPANA ndugu, huwezi kumaliza matatizo ya miaka mitano ndani ya wiki 2.

Jipe muda na uwe mvumilivu. Hatimaye yatapita.

Kumbuka Roma haikujengwa kwa siku moja.

Punyeto ina madhara makubwa kiafya kuliko hata sigara, kuliko bangi, kuliko pombe na kuliko hata dawa nyingine yoyote ya kulevya.

Madhara ya punyeto ni makubwa na mbaya zaidi mhusika anaweza kuwa nayo na asijione kama anayo.

Najua wapo baadhi ya madaktari ambao husema punyeto haina madhara na kwamba ni ngono salama, najua wapo wanaokutia moyo uendelee na kupiga punyeto.

Lakini ukweli wa mambo unaujua mwenyewe.

Kama tayari umeshapiga punyeto miaka mitatu au mitano tayari unafahamu nini kinaendelea kwenye afya yako kwa sasa.

Wakati unapiga punyeto unapata raha sawa na mtu anayejidunga madawa ya kulevya.

Unapoangalia picha za uchi na kupiga punyeto kemikali ya ubongo ijulikanayo kama DOPAMINE hupanda usawa wake asilimia 200 mpaka 300.

Wakati ukitumia dawa ya kulevya dopamine haiwezi kupanda hata kwa asilimia 100 tu.

Lakini punyeto inaipandisha dopamine mpaka usawa wa asilimia 300.

Na ndiyo maana ni rahisi sana kuacha pombe ila siyo kuacha punyeto

Inahitajika kazi ya ziada kuacha punyeto. Siyo jambo au kazi rahisi kama watu wanavyofikiri.

Miaka ya sasa punyeto imekuwa ngumu kuiacha sababu ya simu. Tofauti na zamani kwamba ukitaka kuangalia picha za uchi lazima ukakae kwenye TV ndani au uende usiku kwenye vibanda umiza na ulipie, sasa ni tofauti, zipo kwenye simu yako kiganjani kwako popote uendako.

Punyeto ni moja ya mipango mikakati ya shetani ya kuharibu kizazi hiki cha sasa cha wanaume kwa kutumia picha za uchi.

Ukisoma historia kila mara kumekuwa na mipango maalumu na mingine ya siri ya kuharibu afya ya wanaume na kupunguza uwezo wao wa nguvu na akili.

Soma vitabu vya dini utaona kuna nyakati baadhi ya wafalme walitoa amri watoto wa kiume wauliwe ili idadi yao ipungue na wao watawale kwa urahisi.

Sasa punyeto ni mbinu nyingine inatumika miaka ya sasa kuharibu afya na nguvu za wanaume ili tupate wanaume lege lege, waoga, wasiojitambua, mashoga, na wanaopenda vitu vya haraka haraka na vya kubahatisha

Nimeshaandika sana kuhusu madhara ya punyeto kwenye blog hii, jaribu kupekua pekua utaona na kusoma bure kabisa sichaji gharama yoyote ni elimu ya bure kwa asilimia 100 wala hauhitaji kuwa mwanachama (member) ili kusoma au kucomment (zipo blog huwezi kusoma content zake au ucomment bure bila kuwa member).

Je madhara ya punyeto hupotea baada ya muda gani?

Hakuna jibu la moja kwa moja kwa swali hili.

Jibu rahisi ni inategemea umeshapiga kwa muda gani na umeshaathirika kiasi gani.

Inaweza kuchukuwa miezi mitatu mpaka mwaka hadi miaka kadhaa hadi madhara yote kupotea

Kumbuka tunapozungumzia kuhusu madhara ya punyeto hatuongelei kuhusu kuwahi kufika kileleni na kushindwa kurudia tendo la ndoa pekee.

Hatuzungumzii tu kuhusu uume kusinyaa na kuwa mdogo kama wa mtoto.

Madhara ya punyeto ni zaidi ya hayo.

Punyeto haiathiri mwili tu bali inaathiri mpaka saikolojia yako na namna unavyofikiri na kuongea.

Punyeto inaathiri uwezo wako wa kufikiri na akili yako yote kwa ujumla.

Unaweza ukapata dawa na ukapona tatizo la kuwahi kufika kileleni lililotokana na punyeto lakini akili na saikolojia yako vinaweza kuchukuwa miaka kukaa sawa.

Ili kupona madhara ya punyeto hatua ya kwanza na ya mhimu ni kuacha kupiga punyeto na uondoe vishawishi vyote vinavyokutuma kwenda kujichua.

Inaweza lisiwe jambo rahisi lakini ukiwa ni mvumilivu na mtu unayeipenda afya yako utaweza.

Hakikisha hupigi tena punyeto hata iweje.

Siyo jambo rahisi lakini linawezekana.

Hatua ya pili ni uonane na daktari uso kwa uso kama inawezekana au hata kwa njia ya mtandao akusaidie kuondoa matatizo mengine hasa ya kisaikolojia.

Hatua ya tatu tumia dawa rafiki za kuondoa madhara hayo hasa za asili ambazo hazina madhara mabaya na uziepuke zile zinazokuahidi miujiza na matokeo ya haraka haraka.

Kumbuka chanzo cha tatizo hili ni wewe mwenyewe, ni wewe mwenyewe kwa maamuzi na ujinga wako binafsi uliamua kuharibu afya yako, hivyo uwe mpole na mvumilivu.

Usipende njia za mkato kutatua tatizo lililodumu kwa miaka, ni lazima ujitoe kwa hali na mali ili hatimaye uwe huru tena na hakuna uhuru unaopatikana kirahisi rahisi.

Imesomwa na watu 4,735
Je madhara ya punyeto hupotea baada ya muda gani

26 thoughts on “Je madhara ya punyeto hupotea baada ya muda gani

  1. Nashukuru kwa somo lako na kujitoa kwako kutoa elimu kwaajili ya kusadia maisha ya wengine mm binafsi ni mhanga wa tatizo hili na nahisi nitakuwa nimepata madhara kiakili,kiafya kisaikolojia na kimwili naamini ww ni mtaalamu waweza kuwa msada ili niweze kupona

    1. Hakika elimu yenu ni nzurii sanaaaaa na Mwenyezi Mungu awabariki hakika masomo mazuri pia yanajenga na kila mwenye akili l hope amepata SoMo Mwenyezi Mungu akubariki sanaaaaa mtaalam wetu wa hii kitu πŸ™πŸ™πŸΌπŸ™πŸΌπŸ™πŸΌ

  2. Shukrani Sana brother umezungumza Jambo limenigusa Sana Mungu Akupe Afya njema zaid

  3. Asante san dokta kwa ushaur wak maan mm mwenyew ni muhanga wa tatzo hlo nahtaj ushaur wak zaid

  4. 0626019203 hii ni number yang nakuomb unitumie number yak il tuongee zaid mak mi nina sim ndog siwez kuingia ndan zaid

    1. Tafuta simu kubwa. Mimi nimekuwa nikiandika tuwasiliane WhatsApp tangu 2013 karibu miaka 10 sasa na hakuna dalili yoyote kwamba nitaacha kutumia WhatsApp

  5. asante kwa elimu yako imen gusa me nilpg punyet nusu mwaka lakn tok apo niliacha mpaka xax nimwaka wapil toka nime acha na saivi natumia vilutubisho je nita pona jaman lakn kwagemu namalza alak kwa dk 2 au 3 na siludi laudi nyingne jaman naomba ushauli

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WhatsApp 0714800175