Jinsi ya kuongeza nguvu za kiume bila kutumia dawa

Last Updated on 26/10/2022 by Tabibu Fadhili Paulo

Jinsi ya kuongeza nguvu za kiume bila kutumia dawa

Kwenye makala hii nafundisha jinsi unavyoweza kuongeza na kuimarisha nguvu zako za kiume bila kutumia dawa.

Ni kweli inawezekana kabisa kuimarisha nguvu zako za kiume bila kutumia dawa kama unafahamu ni vitu gani na gani hasa vinahitajika.

Kabla ya yote unatakiwa uwe na ufahamu wa kutosha juu ya nguvu za kiume ni nini hasa na nimejitahidi kufafanua hilo kwenye post mbalimbali ndani ya tovuti hii.

Ni mhimu kufahamu kuwa nguvu za kiume zinahusu vitu viwili vikuu ambavyo ni ;

1. Nguvu za ubongo wako na

2. Nguvu za mwili

Lazima ubongo wako uwe na nguvu za kutosha sawa na zile za mwili wako.

Ili kuongeza nguvu za kiume bila kutumia dawa unahitaji ufanye yafuatayo;

1. Hakikisha huna msongo wowote wa mawazo (stress)

Hakikisha unakuwa mtulivu bila kuwa na mawazo mawazo yoyote.

Ni lazima akili yako iwe katika hali ya utulivu mkuu.

Kama akili yako inawaza madeni unayodaiwa, unawaza wapi utapata kodi ya nyumba, ada za watoto, na huna uhakika wa kupata chakula, basi itakuwa vigumu wewe kuwa na nguvu za kiume.

Hayo hapo juu ni mifano tu ya vitu vinavyoweza kukuondolea amani ya moyo wako na ukaishiwa nguvu za kiume.

Kwahiyo jitahidi usiwe mtu wa mawazo au stress kila mara.

Wewe binafsi unafahamu ni kitu gani hasa kinachokufanya uwe mtu wa mawazo mawazo, shughulika na hicho kinachokuletea mawazo na utakuwa na nguvu za kutosha kitandani.

2. Pata usingizi wa kutosha

Ili uwe na nguvu za kiume bila kutumia dawa ni lazima upate usingizi mzuri, mwingi, na mtulivu kila siku.

Katika vitu vyote vinavyoweza kukusaidia kuwa na nguvu nyingi za kiume usingizi ni namba 1.

Kama hupati usingizi mzuri na wa kutosha kila siku sahau suala la kuwa na nguvu kitandani.

Kama wewe ni mtu wa kukesha unaangalia mpira au tamthilia kwenye TV mpaka usiku wa manane kamwe huwezi kuwa na nguvu za kiume.

Usingizi husaidia kuripea mwili upya, kupumzisha ubongo na kuleta maisha mapya.

Nguvu za kiume mwilini hutengenezwa kati ya saa nane usiku na saa kumi na moja kama uliwahi kulala na ulipata usingizi mzuri.

Hakikisha unapata masaa 8 mpaka 9 ya usingizi kila siku.

Kama kazi yako ni ulinzi basi asubuhi hakikisha unaingia kulala na siyo unaendelea na kazi nyingine tena.

Jinsi ya kuongeza nguvu za kiume bila kutumia dawa

3. Fanya mazoezi ya viungo

Mazoezi ya viungo ni mhimu sana kwa ajili ya kuimarisha nguvu za kiume.

Mazoezi ni lazima kwa mwanaume hata kama huna tatizo lolote la kiafya bado mwanaume lazima ushiriki mazoezi mara kwa mara.

Mazoezi yanasaidia mwili kutumia mafuta kama chanzo cha nguvu badala ya sukari na unapata nguvu mara 3 zaidi ya ile ya nguvu ya sukari.

Mazoezi yatakusaidia kuondoa msongo wa mawazo, yatakusaidia pia kupata usingizi mzuri ambao ni mhimu sana ili kuwa na nguvu za kiume.

Kila mtu ana mazoezi yake kwa mjibu wa umri wake, uzito wake na afya yake kwa ujumla.

Bali mazoezi mazuri kwa kuongeza nguvu za kiume ni pamoja na mazoezi ya kukimbia pole pole (jogging), ya kuchuchumaa na kusimama (squatting), kuogelea, kuruka kamba, ya kichurachura nk

Mhimu mazoezi yawe ni ya mara kwa mara walau mara 4 mpaka mara 5 kwa wiki.

Kama unafanya mazoezi siku 1 tu kwa wiki huwezi kuona faida yoyote.

4. Kula vyakula sahihi

Kama unakula tu na hujuwi unakula nini na kwa ajili ya nini huwezi kuwa na nguvu za kiume.

Kila siku unakula chips na mayai vyote vya kisasa nguvu za kiume zitatoka wapi?

Kama unataka kuwa na nguvu za kiume bila kutumia dawa kula chakula sahihi cha asili kila siku.

Kula vyakula hivi vifuatavyo mara nyingi na utakuja kunishukuru (ingawa wengi wenu hamna shukrani) ;

*ugali wa dona
* ugali wa mtama
* wali nazi
* samaki
* matikiti
* mbegu za maboga
* kitunguu swaumu
* kitunguu maji
* tende
* mtindi
* pweza
* kuku wa kienyeji
* mayai ya kienyeji
* karanga
* korosho
* mvinyo mwekundu
* asali
* chai ya tangawizi
* mkate wa ngano ambayo haijakobolewa (brown bread)
*parachichi
* ndizi za kuiva

Hivyo hapo juu ndiyo viwe sehemu kubwa ya chakula chako kila siku.

Kumbuka pia kunywa maji ya kutosha kila siku kwa mjibu wa uzito wako.

Pia tumia chumvi ya kutosha kwenye vyakula vyako hasa chumvi ya mawe ya baharini ambayo haijapita kiwandani.

5. Dhibiti uzito wako

Kuwa na uzito sahihi ni mhimu sana ili kuwa na nguvu za kiume za kutosha.

Uzito uliozidi, kitambi na uzito uliochini sana vitakuzuia kuwa na nguvu za kiume bila kutumia dawa.

Uzito uliozidi na kitambi vitakufanya kuwa na stamina na pumzi ndogo huku vikikuandalia magonjwa mengine yanayoleta upungufu wa nguvu za kiume kama vile shinikizo la juu la damu, kolesto na kisukari.

Wakati huo huo kuwa mwembamba sana au mwenye uzito mdogo nalo ni jambo linaloweza kukuzuia usiwe na nguvu za kiume za kutosha.

Unaposhiriki tendo la ndoa nguvu zinatumika, protini inatumika na mafuta kidogo yanatumika, sasa kama umekonda si utakufa tu kifuani kwa mtu?

Hakikisha una uzito sahihi ndipo utakuwa na nguvu.

6. Shiriki mara kwa mara tendo la ndoa

Ili uwe na nguvu za kiume ni mhimu uwe unashiriki mara kwa mara tendo la ndoa.

Walau mara 4 au 6 kwa mwezi.

Kama unakaa miezi miwili au mitatu bila kushiriki huwezi kuwa na nguvu na utakumbwa na tatizo la kuwahi kufika kileleni kila mara utakaposhiriki.

Hata gari mpya ikikaa tu miaka mingi bila kutumika vitu vingi ndani yake vitakutwa vimekufa.

Sasa hapa kuna angalizo, ukishiriki mara nyingi zaidi bila kupumzika nayo inaleta upungufu wa nguvu za kiume, kuwe na kiasi na mapumziko ya hapa na pale siyo kila siku.

Shiriki mara nyingi, isiwe chini ya mara 4 kwa mwezi na isizidi mara 21 kwa mwezi.

7. Punguza vilevi

Vilevi vyote vinapunguza nguvu za kiume hasa kama unatumia kupita kiasi na bila ustaarabu.

Sigara, bangi, madawa ya kulevya, pombe zote kama havitatumika kwa kiasi vinaleta upungufu wa nguvu za kiume.

Glasi moja au mbili au bia moja mbili havina madhara na vinaweza hata kukuongezea nguvu kidogo na kukuamsha kuwa na msisimko zaidi, lakini vinapozidi madhara yake ni makubwa.

Kuwa na kiasi au basi ukiweza ni bora usitumie kabisa kilevi chochote.

Sihitaji kueleza mengi sana kuhusu vilevi sababu hata watengenezaji wenyewe wamekuwa wakiandika kwamba vina madhara visipotumika kwa kiasi na kwa ustaarabu.

…….

Ukizingatia mambo hayo 7 niliyoeleza hapo juu ndiyo ni uhakika unaweza kujiongezea nguvu za kiume bila kutumia dawa.

Pamoja na hayo bado nakushauri usiache kuonana na daktari kwa uchunguzi zaidi kubaini nini hasa inaweza kuwa ndiyo sababu ya tatizo lako la kupungua kwa nguvu za kiume.

Na kama unatafuta dawa ya kutibu madhara yatokanayo na punyeto niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175

Kumbuka nimeandika tuwasiliane kwenye WhatsApp.

Share post hii na wengine uwapendao

Imesomwa na watu 1,168
Jinsi ya kuongeza nguvu za kiume bila kutumia dawa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WhatsApp 0714800175