Mambo 6 ya uongo uliyofundishwa kuhusu nguvu za kiume

Last Updated on 01/05/2023 by Tabibu Fadhili Paulo

Mambo 6 ya uongo uliyofundishwa kuhusu nguvu za kiume

Wakati tukiwa watoto, tukiwa vijana wakubwa wakati mwingine hata tukiwa watu wazima hata wazee kuna elimu na maelekezo huwa tunafundishwa na watu wengine mhimu kwenye maisha yetu.

Walimu hao wanaweza kuwa ni walimu wa darasani kabisa shuleni, anaweza kuwa ni baba yako, ndugu yako, daktari, mchungaji wa kanisani au shekhe wa msikitini au hata marafiki zetu wengine wa kawaida.

Shida moja kubwa ni kwamba siyo kila unachofundishwa na kuelekezwa huwa ni sahihi na cha kweli.

Kuna vitu vingi sana tumefundishwa na kuelekezwa na watu mbalimbali lakini ukivichunguza unakuja kugundua havina ukweli kwenye uhalisia wa maisha na ni uongo mtupu.

Ndiyo hapa ukaambiwa mwisho wa siku “ZA KUAMBIWA CHANGANYA NA ZAKO”.

Kwa lugha nyepesi ni kwamba usiwe mtu wa kuamini kila unachofundishwa, vingine jaribu kutumia akili yako binafsi kutokana na uhalisia wa maisha ulivyo.

Sasa linapokuja suala la nguvu za kiume basi kumekuwa na mambo mengi, upotoshaji mwingi na mwisho wa siku kama hutakuwa makini basi unaweza kuharibu zaidi afya yako badala ya kuitengeneza.

Jina langu naitwa Fadhili Paulo, ni Tabibu wa Tiba asili na ni Mtanzania, ofisi yangu inaitwa *Tumaini Herbal Life* ipo Kibugumo Mji Mwema Kigamboni Dar Es Salaam.

Hapa chini naeleza mambo 6 ya uongo ambayo umeelezwa na kufundishwa kuhusu nguvu za kiume;

1. Upungufu wa nguvu za kiume huwapata watu wazima na wazee pekee

Kwa muda mrefu sana umeambiwa na ukaamini kwamba upungufu wa nguvu za kiume unatokea kwa watu wenye umri mkubwa sana na wazee!

Ukweli ni kuwa upungufu wa nguvu za kiume unaweza kumpata mtu wa umri wowote hata mwenye miaka 18.

Tena kwa miaka ya sasa upungufu wa nguvu za kiume unatokea zaidi kwa vijana kuliko hata kwa wazee sababu ya kupanda kwa gharama za maisha na stress za maisha ya kisasa.

Aidha vijana wengi wametumbukia kwenye matamanio ya kupenda kujichua na kupiga punyeto hali inayowafanya wawe dhaifu zaidi kwenye tendo la ndoa kuliko hata watu wazima sana na wazee.

2. Wanaume pekee ndiyo wanaoathirika na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume

Inawezekana umeambiwa na umeamini kwamba inapotokea mwanaume ana tatizo la upungufu wa nguvu za kiume basi anayepata shida ni huyo mwanaume peke yake na siyo wote wawili pamoja na mkewe.

Ukweli ni kuwa mme anapokuwa anasumbuliwa na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume wanaoathirika na kupata shida ni wote wawili yeye mme pamoja na mke wake.

Upungufu wa nguvu za kiume unaweza kupelekea mawazo ya kutokuwa sawa au kujisikia haupo sawa, tatizo linaweza kuleta msongo wa mawazo (depression) na kuathiri ustawi na mstakabali wa ndoa na familia husika.

Kama mke hafikishwi kileleni kwa muda mrefu na hakuna dalili za mme kupona tatizo lake la upungufu wa nguvu za kiume, mke anaweza kufikia hatua ya kutaka kuchepuka na hatimaye ndoa inaweza kuyumba vibaya.

Kwahiyo mwanaume anapokuwa na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume hali hii haimuathiri yeye peke yake bali inamuathiri pia mkewe na inaweza kuleta shida kwenye familia nzima hadi ukoo.

Mambo ya uongo kuhusu nguvu za kiume

3. Upungufu wa nguvu za kiume siyo ugonjwa na wala siyo tatizo kubwa

Okay!

Inawezekana ni kweli upungufu wa nguvu za kiume siyo ugonjwa na wala siyo tatizo kubwa kivile.

Hata hivyo upungufu wa nguvu za kiume ni dalili au ishara ya uwepo wa magonjwa mengine hatari zaidi ndani ya mwili wako kama vile shinikizo la juu la damu, ugonjwa wa moyo, upungufu wa damu, msongo wa mawazo, vidonda vya tumbo, bawasiri na ukosefu wa virutubisho mhimu mwilini.

Kwahiyo wakati ukiendelea kuambiwa kwamba upungufu wa nguvu za kiume siyo ugonjwa basi usifurahi na kuchukulia poa.

Ingawa upungufu wa nguvu za kiume wenyewe kama wenyewe siyo ugonjwa, bado ni ishara ya uwepo wa magonjwa mengine hatari zaidi ambayo unatakiwa kuchukua hatua kwa haraka.

4. Nguvu za kiume ni kukaa kifuani masaa mawili na kupiga bao 7

Hapa ndipo kwenye shida kubwa kuhusu nguvu za kiume.

Waganga, madaktari na baadhi ya washauri wengine wa masuala ya tendo la ndoa wamekuwa wakiwaambia watu kwamba nguvu za kiume ni kukaa kifuani kwa mwanamke masaa mawili na upige magoli mengi hata 7.

Huu ni uongo mkubwa kuhusu nguvu za kiume na ikiwa utaendelea kuamini madai haya unaweza kuharibu afya yako bila kujua.

Nguvu za kiume siyo idadi ya mabao.

Unaweza kwenda hata mara 7 na bado ukaonekana huna nguvu za kiume!

Kuna mwingine anaweza kwenda bao moja tu na bado akaonekana ana nguvu nyingi za kiume kuliko wewe uliyetoa goli 4.

Ili uonekane una nguvu za kiume unatakiwa ubaki kifuani kwa mkeo kwa dakika 15 mpaka 25 bila wewe mwanaume kufika kileleni.

Ndani ya dakika 15 mpaka 25 za mfululizo za wewe mwanaume bila kufika kileleni ndiyo hutafsiriwa kama nguvu za kiume kwa upande wa mwanamke sababu ndani ya muda huo lazima na yeye atakuwa amefika kileleni na kutosheka.

Lakini kama unatumia dakika 3 kufika bao la kwanza, Kisha unapumzika dakika 20 halafu unapanda tena na ndani ya dakika 5 umeshafika tena kileleni na unapumzika tena lisaa limoja halafu unapanda tena na ndani ya dakika 7 tayari umefika kileleni wewe bado huna nguvu za kiume hata kama umerudia tendo la ndoa mara 3.

Kinachoangaliwa hapa siyo wewe mwanaume umerudia tena na tena mara ngapi, Kinachoangaliwa hapa ni umedumu dakika ngapi mfululizo bila kupumzika ndiyo kitu kitakachomfikisha mkeo kileleni na siyo idadi ya mabao!

Wanawake wengi hata kama utaenda mfululizo bila kupumzika huwa wanakuwa wamechoka kuendelea na tendo la ndani ya dakika 20 au 25 au 40.

Kwahiyo mtu anayekuambia kushiriki tendo la ndoa masaa mawili au lazima urudie mara 3 au 4 ndiyo uonekane una nguvu za kiume anataka kukuharibia afya yako na kukuua mapema.

5. Uume ukishindwa kusimama vizuri basi tayari unaumwa upungufu wa nguvu za kiume

Kuna baadhi ya wanaume wameambiwa na kufundishwa na wakaamini kwamba ikitokea siku umejaribu kushiriki tendo la ndoa na uume ukagoma kusimama au ukasimama kwa shida basi tayari una tatizo la upungufu wa nguvu za kiume!

Hili limeleta shida kwenye afya za wanaume wengi sana na kukimbilia kutumia madawa na vidonge bila sababu yoyote ya maana.

Sikia nikuambie, hakuna mwanaume hapa chini ya jua ambaye nguvu zake za kiume zitakuwa sawa kila siku januari mpaka disemba.

Hakuna mwanaume wa namna hiyo.

Mwanaume yoyote haijalishi ni nani au ana nini, mara moja moja inaweza kumtokea tu siku hiyo uume ukagoma kusimama au ukasimama kwa ulegevu.

Hilo huwa linatokea sababu ya mambo mengi labda uchovu mwingi wa kazi kwa siku hiyo, labda mawazo mawazo ya siku hiyo, labda hofu tu ya muda mfupi, labda ni jambo tu la siku hiyo moja.

Tunaweza kusema mwanaume ana upungufu wa nguvu za kiume kama hali ya kutosimama vizuri uume na kuwahi sana kufika kileleni inamtokea kila mara anaposhiriki tendo la ndoa au inamtokea kama mara asilimia 25 ya mara zote anaposhiriki tendo la ndoa.

Lakini kama imekutokea mara 1 au mara 2 ndani ya mara 21 ulizoshiriki tendo la ndoa basi hilo siyo tatizo la upungufu wa nguvu za kiume na wala hauhitaji dawa, unahitaji tu kulala na kupumzika kwa muda mrefu na hali yako itarudi kuwa sawa.

6. Nguvu za kiume zinaleta heshima ya ndoa

Moja ya kelele nyingi za watu wa zamani wanaojidai ni wataalamu wa masuala ya tendo la ndoa hasa upande wa nguvu za kiume ni kuwa nguvu za kiume zinaleta heshima ya ndoa!

Okay!

Ndiyo ni kweli mwanaume anapokuwa na nguvu za kiume za kutosha na akawa anamfikisha kileleni mkewe mara kwa mara kuna aina fulani ya amani hupatikani ndani ya ndoa yao.

Lakini nguvu za kiume peke yake siyo kitu pekee kinacholeta heshima ndani ya ndoa.

Kuna jumla ya mambo mengi sana yanayoleta heshima kwenye ndoa na siyo nguvu za kiume peke yake.

Kwahiyo kama wewe ni mwanaume unapotaka kuboresha ndoa yako usiwe bize na nguvu za kiume pekee.

Maneno yako yawe ni mazuri na matamu, uwe ni mtu mpole na unayejali na kusikiliza mwenza wako, uwe na utu, uipende familia yako yote na uwapende ndugu wa mkeo, jitahidi mkeo awe na amani muda mwingi

Mfundishe mkeo kuridhika na hali mliyonayo na asiwe na tamaa ya mali nyingi za kidunia.

Kwa kifupi uwe mtu unayejali ndipo utapata hiyo heshima ya ndoa na siyo nguvu za kiume tu.

Kama una nguvu za kiume halafu mdomo wako unatoa maneno ya kuudhi na kukera kila mara, huonyeshi dalili ya upole na kujali basi nguvu zako za kiume haziwezi kukuletea heshima unayoitaka.

Imesomwa na watu 159
Mambo 6 ya uongo uliyofundishwa kuhusu nguvu za kiume

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WhatsApp 0714800175