Last Updated on 16/08/2022 by Tabibu Fadhili Paulo
Maneno mawili mhimu zaidi ya neno NAKUPENDA kwenye mapenzi na mahusuiano
Nakusalimu kwa jina la jamhuri ya muungano wa Tanzania …
Leo tena ninapenda kuongelea maneno mawili mhimu zaidi ya neno NAKUPENDA kwenye mahusiano na mapenzi kwa ujumla.
Kila mmoja wetu anafahamu umhimu wa neno NAKUPENDA kwenye mahusiano na mapenzi kwa ujumla.
Naamini hakuna mtu hafahamu umhimu wa neno NAKUPENDA linapokuja suala la mahusiano na mapenzi kwa ujumla.
Neno nakupenda ndilo neno la kwanza na kuu kabisa kwenye mahusiano, ni neno ambalo hutakiwi umalize masaa 24 hujalitamka kwa mwenza wako au kwa mpenzi wako.
Kwa wanandoa hasa mwanaume anatakiwa kumtamkia mkewe NAKUPENDA walau mara 5 kwa siku.
Lakini bado kuna wanandoa wanaweza kumaliza mwezi, miezi hata mwaka hajamtamkia mwenza wake neno nakupenda.
Wengine walilisikia neno nakupenda likitoka midomoni kwa wenza wao wakati ule walipokuwa wanatongozana, baada ya hapo hakuna neno nakupenda tena.
Kama unavyoona mwenyewe neno kuu la kwanza kwenye mahusiano ni neno NAKUPENDA ni neno ambalo kila mtu analifahamu.
Lakini ukiacha neno nakupenda kuna maneno mengine mawili mhimu sana kuliko hata hili neno nakupenda ambayo wanandoa na watu wengi waliopo kwenye mahusiano hawajuwi umhimu wake.
Na kwenye makala hii najadili kwa undani maneno hayo mawili na umhimu wake kwenye ndoa au kwenye mahusiano yoyote hasa yale ya kimapenzi.
Maneno mawili mhimu zaidi ya neno NAKUPENDA kwenye mapenzi na mahusuiano;
1. AHSANTE
Neno AHSANTE ni neno la pili la mhimu sana kwenye mahusiano na mapenzi.
Ni neno ambalo kama wanandoa watalifahamu na kutambua umhimu wake basi ndoa nyingi sana na mahusiano mengi sana yatakuwa salama na mahali pa kukimbilia.
Ndoa nyingi sana ambazo wanandoa wanalifahamu na kulitumia hili neno huwa ni ndoa zenye furaha sana.
Ikiwa una mme au mke au mpenzi mwenye tabia na kawaida ya kutumia neno AHSANTE mara kwa mara kwenye mahusiano yenu basi hakuna shaka yoyote mahusiano yenu ni imara na yenye furaha sana.
Watu wengi sana hawajuwi umhimu na faida ya hili neno AHSANTE.
Na mara nyingi sisi binadamu tunakawaida ya kusema ahsante baada ya kufanyiwa jambo fulani zuri wakati Mungu yeye anapenda tumwambie ahsante hata pale tunapokutana na mabaya au na shida.
Hapo ndiyo unaweza kuanza kufahamu umhimu wa neno hili, kwamba wakati sisi tuna mazoea ya kusema AHSANTE baada ya kufanyiwa jambo zuri, Mungu yeye anataka kuambiwa AHSANTE hata pale mambo yetu yanapokuwa magumu.
Umeona?
Au bado upo usingizini?.
Kwahiyo ili uishi kwa amani na mpenzi au mwenza wako ni mhimu kujizoesha kutumia neno AHSANTE kwenye mazungumzo yenu mengi.
Kile tu sitaki ufanye ni kusema AHSANTE kwa mwenza wako hata pale anapokufanyia mabaya, hilo tumwachie Mungu kwani yeye tu ndiye anayetaka kuambiwa ahsante hata kama anatupitisha kwenye shida na majaribu.
Kila mtu huwa anapata hamasa ya kufanya zaidi na kujitoa zaidi pale anapogundua mchango wake unathaminiwa, mchango wake unatambuliwa na anarudishiwa AHSANTE.
Neno AHSANTE ni zaidi ya limbwata kwenye mahusiano.
Kama unataka kumteka mmeo au mkeo akufanyie hata yale hukuwahi kufikiri anaweza kukupatia basi jizoeshe kumwambia AHSANTE mara kwa mara na hutakawia kuona mabadiliko mazuri kwenye mahusiano yenu.
Labda nikuulize wewe hapo unayesoma ujumbe huu sasa, ni lini ulipofanyiwa jambo zuri na mwenzio na ukasema AHSANTE? lini ilikuwa ndiyo mara ya mwisho kusema hivyo?
Hebu nijibu tuone ….
Kwa mjibu wa tafiti mbalimbali zilizowahi kufanywa kuhusu mahusiano imegundulika ndoa nyingi sana huishia njiani kwa sababu tu ya kukosekana kwa neno AHSANTE baina ya wenza.
Ahsante ni neno la mhimu sana kwenye mahusiano kuliko hata neno NAKUPENDA.
Ni neno lenye nguvu sana ya kumteka mwenza wako na hakuna namna naweza kukueleza ukaelewa mpaka umefanya majaribio wewe mwenyewe.
Cha ajabu na cha kusikitisha sana ni kwamba kuna mwanandoa anaweza kumaliza hata mwaka mzima yaani miezi 12 bila kumtamkia mwenza wake neno ahsante!
Unaweza ukashangaa lakini hali ndivyo ilivyo.
Chanzo chake kikuu ni kuwa mkishaishi pamoja kwa muda mrefu au mkishakuwa kwenye mahusiano kwa muda mrefu kila mmoja anaanza kumuona mwenzake ni wa kawaida na kila unachofanyiwa na mwenzio unaona kama vile ni haki yako na ni lazima akufanyie hayo na huoni sababu yoyote ya kusema AHSANTE.
Mwenza wako amepika chakula kizuri, mwambie AHSANTE. Amekuletea pipi, mwambie AHSANTE. Amekununulia nguo, mwambie AHSANTE. Umemuomba haki yako ya kitandani na amekupa bila kinyongo na kwa furaha zote, mwambie AHSANTE.
Penda kuwa mtu wa ahsante siku zote hata kwa vitu vidogo vidogo na hutachelewa kuona mabadiliko mazuri kwenye maisha yako.
Kadri unavyokuwa mtu wa ahsante kwa mwenzako ndivyo unavyozidi kumpa hamasa ya kufanya mengine zaidi kwako kwani anaona wewe ni mtu mwenye shukrani.
Kama Mungu anapenda kuambiwa AHSANTE hata pale anapotupitisha kwenye majaribu na shida, je si mhimu zaidi ukimwambia mwenza wako AHSANTE pale anapokupatia au kukufanyia jambo lolote zuri hata kama ni dogo?.
Chunguza nchi nyingi na jamii nyingi za watu wenye furaha utagundua watu hao wana desturi ya kuwa na neno AHSANTE kwenye midomo yao mara kwa mara.
Mwingine kusema ahsante ni mpaka afanyiwe jambo kubwa au aletewe zawadi yenye thamani kubwa, tofauti na hapo haoni sababu yoyote ya kusema ahsante.
Umepigiwa simu, umetumiwa sms mwambie mwenzio AHSANTE KWA KUNIKUMBUKA.
Kuna mwingine hata haya maelezo ninayowaandikia anayachukulia poa anaona ni ya kawaida tu na anafikiri labda ni haki yake au ni lazima niyaandike na yeye ayasome BURE.
Hajuwi ni gharama ngapi huwa naingia ili nitenge muda kuandika yote haya, niweke bando kwenye computer yangu, nilipie bill za umeme, niache kucheza na watoto au na mke wangu; lakini nitenge muda kukuandikia yote haya na bado huna shukrani na wala huoni umhimu wangu.
Kuna wana ndoa hulipia maelfu hata mamilioni kuhudhuria semina au kozi mbalimbali zinazofundisha mambo kama haya, lakini wewe unaandikiwa BURE hata kusema tu siku moja unitumie japo 1000 na mimi ninunue soda huna muda huo.
Unaona ni haki yako kufundishwa haya yote BURE.
Kwahiyo kwenye mahusiano yoyote ambayo wenza au wapenzi hao huona umhimu na ulazima wa kumtamkia mwenzake neno AHSANTE mara kwa mara ndoa hizo au mahusiano hayo hudumu sana na huwa ni sehemu yenye furaha siku zote.
Watu wengi hawana shukrani na hawana roho ya shukrani hata wafanyiwe mambo mazuri vipi.
Kuanzia leo badilika.
Na ikiwa elimu hii inakusaidia kuboresha mahusiano yako au afya yako kwa ujumla na unapenda kunipa zawadi yoyote nitafute tu kwenye WhatsApp +255714800175 nitakupa maelezo namna unaweza kunitumia zawadi yako.
2. SAMAHANI
Neno la pili mhimu zaidi kwenye ndoa na kwenye mahusiano zaidi ya neno nakupenda ni neno SAMAHANI.
Neno samahani ukizoea kulitumia litakufikisha mbali sana tofauti na unavyoweza kulichukulia.
Fahamu wewe ni binadamu siyo malaika, hivyo kwa namna moja au nyingine unaweza kumkwaza mwenza wako wakati wowote kwa kukusuida au bila hata kukusudia.
Tofauti hapa itakuwa kwa mtu yule asiyeona shida kutamka neno SAMAHANI.
Kuna baadhi ya watu kusema SAMAHANI ni udhaifu na ni kama kujishusha hivi thamani yake.
Lakini ndoa nyingi zenye furaha na zinazodumu muda mrefu ni zile wanandoa hao hawaoni tabu kusema SAMAHANI pale anapoona amemkosea mwenzake.
Dunia hii ilivyo ya ajabu kuna mtu anaweza kukukosea wazi wazi kabisa lakini badala ya kuomba tu samahani yaishe yeye atajibalaguza, atabadili maneno hata ionekane hana kosa na hawezi kusema samahani.
Dalili nzuri kabisa ya mtu mpumbavu ni yule mvivu kusema SAMAHANI hasa pale inapojulikana wazi ametenda kosa.
Kusema samahani ni ishara ya mtu mwenye akili na muungwana na anayejali wenzake.
Kama wewe huwa unakosa halafu huombi samahani wewe ni mpumbavu mkubwa.
Hata Mungu anatutaka tumuombe samahani, anatutaka tufanye kitubio na kujutia pale tunapomkosea.
Ndugu yangu kama unataka amani, unataka furaha, unataka upendo kutoka kwa wengine jifunze kulitumia neno SAMAHANI kwenye mahusiano yako.
Jambo la mhimu la kuzingatiwa hapa ni kuwa usiwe mtu wa kuomba samahani mara kwa mara tena kwa kosa lile lile moja.
Kama haipiti masaa 24 bila kuomba samahani na wewe utakuwa na matatizo binafsi.
Kuna mtu anafanya kosa anaomba samahani anasamehewa, lakini baada ya siku kadhaa mbele anafanya tena na tena kosa lile lile aliloomba samahani juzi!!!
Ni kweli kuomba samahni ni akili na ni uungwana lakini kama unafanya kosa lile lile mara kwa mara hata baada ya kusamehewa, na wewe ni mpumbavu kabisa.
Kwenye maisha ya ndoa au kwenye mahusiano yoyote ya kimapenzi kukosana ni jambo la kawaida na ni sehemu ya maisha, na ukiona mnaishi miaka mingi bila kugombana japo kidogo tu ujuwe kuna kitu siyo sawa kati yenu na huenda mmoja wenu ameshakufa tayari huku bado anatembea.
Hapo ndipo neno samahani linapochukua nafasi yake.
Ndugu yangu na msomaji wangu sitaki nikuchoshe sana kwa leo.
Mhimu ukumbuke maneno mawili mhimu zaidi ya neno nakupenda kwenye ndoa na kwenye mahusiano ni AHSANTE na SAMAHANI.
Kama wewe ni mwanaume na unatafuta dawa ya asili kwa ajili ya kuimarisha nguvu za kiume au kutibu madhara yatokanayo na punyeto, niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175.
Share post hii na wengine uwapendao.
Maneno mawili mhimu zaidi ya neno NAKUPENDA kwenye mapenzi na mahusuiano Share on X