Mtongoze mwanamke yoyote kwa kutumia mbinu hii

Last Updated on 12/11/2021 by Tabibu Fadhili Paulo

Mtongoze mwanamke yoyote kwa kutumia mbinu hii

Kwa wale wenzangu na mimi a.k.a kina domo zege leo ni bahati yetu na hatimaye shida kubwa iliyokuwa ikitusumbua inaweza kuisha leo!

Ndiyo kwa mwanaume ambaye ni muoga wa kutongoza mtaani tumezoea kumuita domo zege.

Mara nyingi kuogopa kutongoza ni matokeo ya aibu kubwa aliyonayo mtu na uoga wake binafsi.

Awali ya yote niombe radhi kwanza kwa kichwa cha habari hapo juu ambacho kinasema ‘Mtongoze mwanamke yoyote kwa kutumia mbinu hii’.

Ukweli ni kuwa hakuna mbinu wala namna yoyote inayoweza kukusaidia kumtongoza mwanamke yoyote!

Huwezi kumtongoza mwanamke yoyote! ingekuwa hivyo maisha yasingewezekana.

Kuna wanawake inabidi uwatazame tu na wala usipoteze muda wako kujidai wewe ni mwanaume na hivyo unaweza kutongoza yoyote, hakuna maisha ya namna hiyo.

Kwa mfano wanawake wafuatao hawawezi kutongozwa na mtu yoyote; mwanamke ambaye ni mkuu wa mkoa au ni waziri katika wizara fulani au ni jaji katika mahakama fulani au ni mfanyabiashara mkubwa mwenye maisha yake hawezi kutongozwa na mtu yoyote.

Hata hivyo huwa inatokea wanawake wa namna hiyo hapo juu wakaolewa na mtu wa kawaida kabisa ambaye huwezi hata kumtarajia, hiyo ni kutokana na bahati tu kutoka kwa Mungu mwenyewe au inaweza kutokea mwanamke mwenyewe ndiyo amekuchagua na kuamua kukutunuku penzi lake au maisha yake.

Kwahiyo mbinu ninayoenda kukufundisha leo inaweza kukusaidia kumtongoza mwanamke yoyote umtakaye na kumpenda LAKINI HAIFANYI KAZI KWA KILA MWANAMKE. Kuna wanawake wengine kubali kwamba huna uwezo wa kuwatongoza labda wakutake wao wenyewe.

Ukweli ni kuwa kuna vijana wengi sana wa kiume ambao ni waoga sana kutongoza, yaani ana aibu na uoga uliopitiliza wa kumtaka mwanamke na yupo tayari kupiga punyeto miaka na miaka lakini siyo kufungua mdomo wake na kumtongoza mwanamke.

Kama tujuavyo wote punyeto ina madhara makubwa kwa afya ya mwanaume na inaweza kuharibu hadi afya ya akili yake.

Wapo wazazi wanaona wazi mwanangu ni muoga wa kutongoza lakini kwa sababu ya tamaduni zetu za kiafrika wanalazimika kukaa kimya tu bila kumwambia chochote huku wakimuacha akijidhuru kwa kujicua mwaka hadi mwaka.

Ukweli ni kuwa hakuna mzazi anayependa mwanae wa kiume awe muoga wa kutongoza.

Hakuna mzazi wa namna hiyo.

Hata mama yako mzazi anatamani uwe na mchumba na siyo ujichue ila hawezi kukuambia moja kwa moja kwa sababu ya tamaduni zetu za kiafrika.

Hata mama yako mzazi anatamani uwe na mchumba na hatimaye uoe uwe na mke wako umletee wajukuu na uwe na maisha yako na siyo ukae hapo nyumbani kwa wazazi miaka na miaka hutaki kuoa upo bize na kupiga punyeto!

Unaweza kusoma zaidi madhara ya punyeto kwa kubonyeza tu hapa.

Kabla sijakuambia ni mbinu gani hasa unaweza kuitumia kumtongoza mwanamke yoyote umtakaye nikupe kidogo historia kuhusu jambo hili la kutongoza lilivyokuwa miaka mingi huko nyuma.

Miaka mingi huko nyuma kijana wa kiume hakulazimika kumtongoza mwanamke yoyote. Hii ilikuwa ni kazi ya baba yako mzazi.

Hata kijana wa kike hakuwa na jukumu la kutafuta mwanaume wa kuolewa naye kama tunavyoona miaka ya sasa, hilo lililikuwa ni jukumu la wazazi wake.

Msichana alitakiwa kujilinda, alitakiwa kutokuwa mhuni wala kuwa na tabia yoyote mbaya; basi hayo tu yalikuwa yanatosha kumuhakikishia kupata mwanaume wa kuolewa naye kupitia wazazi wake.

Kwa kijana wa kiume ni baba yako mzazi ndiyo alikuwa na jukumu la kukutafutia mke.

Baba yako mzazi anakutana na baba wa binti ambaye unatakiwa kumuoa.

Binti huyo huenda hata hujawahi kumfikiria kama utakuja kumuoa, lakini yeye baba yako mzazi kwa kushauriana na mama yako watakuwa wamemuona msichana huyo kuwa anafaa kuwa mke wako.

Hivyo baba yako atamfuata baba wa binti huyo atakayekuja kuwa mke wako na kumwambia nataka kumuolea mwanangu binti yako.

Baba yako na baba wa msichana huyo watajadiliana kila kitu na kufikia muafaka na makubaliano.

Basi baba yako atakuja nyumbani na kukuambia utamuoa binti fulani kutoka familia fulani, baba yako pia atatoa mahari na gharama zingine zozote zinazohitajika na kukukabidhi wewe mke!

Ndivyo ilivyokuwa.

Hakukuwa na mambo mengi wala wewe kama kijana hukuwa na kazi yoyote ya kutafuta mwanamke wa kumuoa.

Hakukuwa na simu wala facebook wala WhatsApp nyakati hizo.

Wazazi wako walikuwa na jukumu la kukuletea mke na jukumu la kuangalia kwenye jamii yenu au kijiji chenu ni msichana yupi kutoka familia ipi ana tabia nzuri ambazo wao wamezipenda na wamependa huyo awe ni mke wako.

Mpaka leo kuna baadhi za jamii na makabila huko vijijini ndani kabisa wanaishi kwa namna hii.

Basi maisha yalienda hivyo kwa miaka mingi na ndoa zilikuwa nzuri na zilikuwa zinadumu miaka na miaka hakuna kuvunjika hovyo hovyo kama ilivyo sasa.

Baada ya hapo shule zikaja tukajua kusoma na kuandika.

Kwa kujua kusoma na kuandika tukapata urahisi kidogo kwenye kutongoza.

Sasa ukawa ni mwendo wa kuandikiana barua tu na kusubiri majibu kwa wiki 2 hadi miezi kadhaa.

Na nyakati hizo ilikuwa ni vigumu umtongoze mwanamke leo na akupe jibu leo leo kama ilivyo miaka ya sasa.

Hapo ukimtongoza mwanamke jibu la kwanza lilikuwa ni subiri nikafikiri na kushauriana na wazazi kwanza halafu nitakujibu tena na inaweza kuchukua miezi hadi ujibiwe tena.

Basi tuliishi hivyo kwa miaka mingi mpaka ilipokuja simu, facebook, WhatsApp na instagram.

Hapo sasa muda wa kusubiri majibu ulipungua sana kutoka miezi kadhaa mpaka ndani ya siku 1 au ndani ya masaa kadhaa umeshajibiwa kama mambo safi au hapana!

Ni mwendokasi tu ndiyo maisha tuliyonayo kwa sasa.

Kwahiyo huwa inanishangaza sana ninapokutana na kijana wa kiume anayedai ni muoga wa kutongoza na hivyo yupo tayari hata kupiga punyeto na siyo kumtongoza mwanamke sababu ya woga au hofu ya kukataliwa.

Kabla sijakupa mbinu hiyo moja unayoweza kuitumia ili kumtongoza mwanamke yoyote napenda nikupe baadhi ya kweli kuhusu wanawake;

1. Wanawake wote wanapenda kutongozwa.

Wanawake wote wapo hivyo.

Ndiyo maana wanatumia muda mwingi sana kujipamba na kujilemba kabla ya kutoka ndani ya nyumba.

Ni furaha kubwa kwa mwanamke kuona anatongozwa ingawa kwa mara ya kwanza lazima ajifanye hataki, hakupendi na hakuhitaji, lakini kutoka moyoni kabisa wanapenda sana kutongozwa.

Msichana asipotongozwa kwa miezi 6 mfululizo kuna uwezekano mkubwa akapatwa na msongo wa mawazo na pengine anaweza kulazimika kwenda hata kwa mganga wa kienyeji kutafuta dawa ya kusafisha nyota yake!

2. Mwanamke mwenye akili hawezi kukubali kuwa wako kwa kumtongoza mara moja tu

Hapa ndipo siri kubwa ilipo kuhusu wanawake.

Na ndipo vijana wengi wa kiume hawapataki hasa wale wavivu.

Mwanamke mwenye akili hawezi kukubali kuwa mchumba wako mara baada ya kumtongoza mara moja tu!

Ukiona amekubali kwa mara moja basi ujuwe huyo hana akili au na yeye mwenyewe alikuwa akikupenda tangu siku nyingi ila alikuwa anaogopa tu kukuambia, lakini bado mwisho wa siku ndoa yenu itakuwa na shida za hapa na pale.

Mwanamke mwenye akili anataka umtongoze mara 2 au mara 3 au hata mara 5 ndiyo akukubalie.

Anataka ajiridhishe kutoka moyoni kwamba ni kweli upo siriasi na unachokisema? ni kweli umemaanisha? umempenda kweli au umemtamani tu?

Vile vile anataka kukuchelewesha kukubalia ili usije ukamchukulia poa na kumuona ni wa rahisi rahisi tu.

Sasa wanaume wenzangu na mimi wavivu akishakataliwa mara moja tu anakimbia na aibu zote zinamjaa.

3. Siyo kila mwanamke utakayemtongoza atakukubalia

Ndiyo sababu niliomba radhi pale mwanzoni tu mwa makala kuhusu hili.

Ukweli ni kuwa siyo kila mwanamke utakayemtongoza atakukubali, hilo ni jambo la kawaida na unapaswa uwe nalo kichwani.

Usilazimishe penzi huo ni upumbavu.

Kama umeshambembeleza mara 3 au mpaka mara 5 na anakukatalia muache na umtafute mwingine, ni jambo la kawaida.

Usitumie cheo, madaraka, au utajiri au chochote ulichonacho kutaka kumlazimisha mwanamke akukubalie.

Najua wapo wanaume wasiojitambua huwa wanalazimisha tu kisa ana kacheo fulani au ka-status fulani kwenye jamii basi anafikiri kwa sababu hiyo anaweza kumtongoza yoyote!

Hapana!

Maisha hayapo hivyo utaishia kufa tu hata kwa kulogwa au kwa njama nyingine yoyote.

Usilazimishe penzi.

Mtongoze mwanamke yoyote kwa kutumia mbinu hii

Baada ya kusema hayo yote sasa ni wakati wa kukuambia mbinu unayoweza kuitumia kumtongoza mwanamke yoyote na ukampata.

Wengi wa wanaume wanaogopa kutongoza ni wale;

1. Wanaoogopa kukataliwa,

2. Wanaotaka majibu leo leo,

3. Wanaotaka majibu ya ndiyo peke yake bila hapana na

4. Wale wanaofikiri lazima uwe na maneno maneno mengi ndiyo mwanamke akukubalie

Wapo baadhi ya wanaume ni hodari sana wa kutongoza na kubembeleza mwanamke, anaweza kupiga hadi magoti, anaweza hadi kutoa machozi ili tu akubaliwe na mwanamke, wapo wanaoenda mbali hadi kuahidi kumnunulia mwanamke ndege ili tu akubaliwe!

Sasa mbinu rahisi ya kumtongoza mwanamke yoyote ni kutokwenda moja kwa moja au kutokwenda kichwa kichwa kwa gia ya kutaka kumtongoza kiasi hadi yeye anakushtukia mwanzoni tu kuwa unataka nini kwake.

Usiende moja kwa moja na kumwambia mimi nimekupenda, nataka uwe mchumba wangu au nataka nije nikuoe!

Wanawake wengi hawapendi hivyo.

Neno moja tu la kumwambia mwanamke yoyote na ukampata bila kutumia nguvu nyingi wala hela zako nyingi ni kumwambia tu naomba uwe RAFIKI YANGU.

RAFIKI.

Mwambie tu naomba niwe rafiki yako, mwambie naomba tuwe marafiki.

Hivyo tu.

Huhitaji kusema mimi nimekupenda, sijuwi wewe ni mzuri sana, sijuwi mara nikinywa maji nakuona kwenye kikombe au usiku silali nakuota wewe tu.

Huko ni kupoteza muda na kujitafutia stress bila sababu.

Mwambie tu naomba tuwe marafiki.

Basi.

Akikuuliza unataka tuwe marafiki tu huhitaji kingine, mwambie ndiyo nataka tuwe marafiki tu sihitaji kingine.

Sasa akishakukubalia muwe marafiki kazi ni kwako na kifuatacho ITV ni taarifa ya habari.

Hakikisha unakuwa karibu sana na rafiki yako.

Mpigie simu, mtumie sms mara kwa mara (siyo kila wakati wala isiwe kero lakini isipite siku hujamtumia hata sms moja).

Ni rafiki yako huyo kuwa naye karibu, mtoe out siku za weekend, nendeni mkatembee huko na huko na rafiki yako mpya.

Wakati huu mkiwa marafiki ndiyo unaweza kumsoma na kumwelewa vizuri kwamba ni mtu anayeweza kukubali awe mchumba wako au atakataa, unaweza kumsoma nyakati hizi.

Na wapo wanawake wengi tu kwenye hii hii hatua ya kuwa marafiki anaweza kukupa hadi unachohitaji bila kutumia nguvu yoyote, yaani kimasihara tu ushapewa ulichokuwa unakihitaji ambacho siyo urafiki tena bali ni ….

Wakati huo huo uwe bize na kazi na shughuli za kukupatia kipato kwa sababu wanawake hawapendi kuwa na mwanaume mvivu au asiye na shughuli au kazi yoyote.

Na pia mbinu hii  unaweza kuitumia hata kwenye biashara zako zingine, wateja wa siku hizi wanapenda kwanza muwe marafiki kabla ya kumuuzia bidhaa yako. Tafuta marafiki, usitafute wateja, na utaona biashara yako inavyokuwa kwa kasi.

Ukipata muda soma na hii > Jinsi ya kuacha punyeto

Ikiwa unatafuta dawa ya kutibu madhara yatokanayo na punyeto, niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175, Maelezo yake zaidi unaweza kusoma kwa kubonyeza hapa.

Share post hii na wengine uwapendao.

Mtongoze mwanamke yoyote kwa kutumia mbinu hii Share on X
Imesomwa na watu 2,435
Mtongoze mwanamke yoyote kwa kutumia mbinu hii

One thought on “Mtongoze mwanamke yoyote kwa kutumia mbinu hii

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WhatsApp 0714800175