Last Updated on 26/10/2021 by Tabibu Fadhili Paulo
Mwanaume mwenye sifa hii anapendwa na wanawake wote.
Leo nitakueleza kwa undani kabisa ni nini hasa wanawake wanapenda kutoka kwa waume zao au wachumba zao.
Wanaume karibu wote kote duniani wamekuwa na swali hili na kutaka KUFAHAMU ni nini hasa kinachowavutia wanawake kwao.
Wanaume wengi wanatafuta KUFAHAMU ni tabia gani au ni kitu gani wakiwa nacho kitawafanya wapendwe na wake zao au wachumba zao
Wapo Wanaume wanaodhani labda wanawake wanapenda wanaume wenye hela au matajiri.
Kama unatumia mtandao basi umeshasoma comment za watu mbalimbali wakihitimisha kwamba wanawake wanapenda hela tu na kwamba mwanaume uwe bize na kutafuta tu hela na wanawake watakupenda.
Hilo la Wanaume kudhani wanawake wanapenda hela tu siyo habari ngeni na hata nijaribu kueleza vipi kupinga mawazo hayo nina uhakika wa asilimia 100 wapo ambao hawatakubali.
Hata hivyo ukweli ni kuwa wanawake hawapendi hela tu kwenye mahusiano kwa sababu ukweli ni kuwa hakuna mtu asiyependa hela awe ni mwanamke au mwanaume hakuna mtu asiyependa hela
Hakuna mtu asiyependa hela.
Utaongea misemo, nahau na ngonjera zako kutaka tukuone kwamba hela siyo kitu mhimu kwako lakini toka moyoni unafahamu kuwa kila kitu kinahitaji hela.
Hela siyo kila kitu ni sawa, lakini kila kitu kinahitaji hela
Hata kanisani hatupewi Biblia bure.
Biblia inauzwa na bado unawajibika kutoa zaka na sadaka.
Ninayo Biblia ya bure kwenye simu yangu lakini nikiifungua na intaneti imewashwa basi ni matangazo kila upande, kwahiyo nayo siyo bure kwa asilimia 100.
Na hata hii Biblia kwenye simu bado sikuipata bure kama bure sababu ilinilazimu kununua kifurushi cha intaneti ndiyo nikaipakua (download).
Hata ikitokea kanisa limejenga hospitali usitegemee utaingia hapo na kupata matibabu bure sababu eti ni hospitali ya kanisa!
Mwanamke mpenda pesa ni yule ambaye anapata mahitaji yote ya mhimu toka kwa mmewe kama malazi, chakula na matibabu lakini bado anachepuka ili tu apate hela ya kununua vitu visivyo na umhimu wowote kama simu, nguo, vilevi nk
Lakini kama mwanamke amekukubali na huoni akiwa bize kudai dai vitu visivyo na ulazima huyo hajakupendea hela na wala hahitaji hela yako.
Ukiacha hayo siku hizi uchumi wa kibepari unamuwezesha mtu yoyote kuwa na hela bila kujali jinsia yake
Miaka ya sasa ni kawaida tu kumkuta mwanamke ana nyumba yake na biashara yake na hela zake
Wapo wadada wengine wamezaliwa kwenye familia tajiri na wala hahitaji hela yoyote ya mwanaume
Ukikutana na 👆mwanamke wa namna hiyo unafikiri hela zako zinaweza kukuongezea mvuto wowote?
Jibu ni hapana.
Ninaweza kuandika maelezo mengi na nitakuchosha bure kukuhakikishia kwamba hela siyo kitu pekee wanawake wanapenda kutoka kwa waume zao au wachumba zao.
Wanawake wanapoonyesha kukupendea hela kwa sehemu kubwa huwa ni hitaji lao la kuwa na usalama kwa maana ana uhakika hatashinda njaa na akiumwa ana uhakika wa kwenda hospitali.
Je wanawake wanapenda mwanaume mwenye sifa ipi?
Ni sifa au tabia gani mwanaume ukiwa nayo una uwezo wa kupendwa na mwanamke yoyote wa kabila lolote na taifa lolote?
Kama ulikuwa unafikiri ni hela umekosa na hata Biblia imeagiza tuishi na wake zetu kwa akili na siyo kwa hela.
7. Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe.
1 Petro 3:7
Unaweza kufikiri labda ni muonekano wako mzuri.
Labda umeenda hewani, ni mwanaume mtanashati (handsome) au labda unakifua kizuri unafanya mazoezi ya kunyanyua vyuma na unafikiri ni kitu mhimu wanawake wanahitaji
Unaweza kujitesa mwili wako na pengine upoteze hadi hela ili uwe na Sixpack tumboni na ukafikiri labda wanawake wanapenda wanaume wenye Sixpack!
Wakati fulani nilikuwa napenda na nawaza muda wote namna ya kuwa na Sixpack tumboni mwangu. Namshukuru Mungu wazo hilo sina tena na wala sina kitambi
Ingawa hata kuwa na kitambi siyo jambo baya na hakuna mwanamke anaweza kukuacha kisa tu una kitambi!
Kwahiyo kitu pekee kila mwanamke anahitaji kutoka kila kabila au taifa anachopenda na kinachomvutia sana kwa mwanaume siyo hela, siyo utajiri, siyo mali, siyo muonekano hasa wa huyo mwanaume wala siyo cheo wala madaraka.
NDIYO unaweza kuwa na hizo mali na sifa za kidunia na vinaweza kuwasaidia muishi bila kuwa omba omba lakini siyo kitu pekee mwanamke anahitaji kutoka kwa mwanaume
Utanisamehe pia nikikuambia hata siyo tendo la ndoa linalomvutia kwako na kutaka kuolewa na kuishi na wewe.
Unaweza kuwa na nguvu kama simba kitandani na bado mwanamke asione sababu ya kuishi au kuwa na wewe
Je ni sifa gani hiyo ukiwa nayo mwanamke yoyote anaweza kukupenda na kuhitaji kuwa na wewe?
Ukiwauliza wanawake swali hili kote duniani jibu lao la kwanza utasikia wanataka mwanaume mwenye hofu ya Mungu.
Kila mwanamke lazima atakujibu hivyo kwanza.
Hata hivyo kwenye jamii tunashuhudia ndoa zenye amani na zinadumu miaka mingi huku wanandoa wote wakiwa ni wapagani na wanaishi miaka bila kuingia kanisani wala msikitini.
Kumbuka haijalishi unaishi kwa amani kiasi gani bado kuna umhimu wa kwenda kanisani au msikitini
Usichukulie haraka haraka maneno yangu hapo juu
Kwahiyo kuwa na hofu ya Mungu tu bado kunaweza kusitoshe.
Ingawa wanawake wote wanaanza kwa kusema wanahitaji mwanaume mwenye hofu ya Mungu, ukweli wa mambo ni kuwa wanawake wanapenda kuwa au kuishi na mwanaume ambaye ni MKARIMU.
Ukarimu ndiyo kitu pekee kila mwanamke anahitaji kutoka kwa mwanaume.
Kama wewe ni mwanaume na huoni sababu ya kuwa MKARIMU ni ngumu kupendwa na mwanamke yoyote.
Anaweza kukuvumilia labda sababu ya umaskini akaishi na wewe lakini siku isiyojulikana ataachana na wewe bila kujali una hela ngapi.
UKARIMU.
NDIYO sababu unawasikia wanataka mwanaume mwenye hofu ya Mungu kwa sababu ni ngumu mtu awe na hofu ya Mungu halafu asiwe MKARIMU.
Jitahidi tu uwe MKARIMU na mengine yote yatakuwa sawa.
Kila mwanamke kutoka kila kabila au taifa lolote anapenda kuwa na kuishi na mwanaume ambaye ni MKARIMU.
Hela, Mali, uzuri wako ni vitu vya ziada lakini cha kwanza wanaangalia ni UKARIMU.
SASA kwa leo sitaki nikuchoshe sana kwa maelezo mengi bila sababu.
Nimefanikiwa kukufafanulia kitu kimoja mhimu kila mwanamke anapenda mwanaume wa ndoto zake awe nacho.
Natumaini utafanyia kazi na kunipa mrejesho.
Sasa pamoja na hayo siwezi kukuacha hivi hivi tu bila kukupa angalizo.
Angalizo / warning;
Nimesema kwamba UKARIMU ndiyo kitu pekee kila mwanamke anahitaji kutoka kwa mwanaume wa maisha yake, Sasa usikimbie tu mbio mbio kuwa MKARIMU bila kutumia akili.
Usije kunililia huko siku za mbeleni kwamba nilikushauri uwe MKARIMU na mambo yakawa tofauti.
Ni hivi; hata huo ukarimu uwe na kiasi.
Ukizidisha na wenyewe una madhara.
Tena madhara makubwa kuliko hata ukatili.
Wapo baadhi ya wanawake na hata wanaume ukiwa ni MKARIMU sana hawachelewi kukuchukulia poa na pengine hata kukuona wewe ni mdhaifu au ni wa bei rahisi.
Wakati unajifunza na kuanza kuwa MKARIMU fanya kwa kiasi ukipitiliza sana hawakawii kukudharau.
Na unapoona ukarimu wako unachukuliwa poa au hauthaminiwi kwa kipindi kirefu usiogope kusema please stop it, enough is enough.
22. Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,
23. upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.
Wagalatia 5 : 22 – 23
Ni hayo tu kwa leo
Kama wewe ni mwanamke na unaishiwa hamu ya tendo la ndoa yaani husisimki tena kushiriki tendo la ndoa ninayo dawa nzuri sana ya asili kwa ajili ya tatizo lako. Kama utaihitaji niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175
Share post hii kwa ajili ya wengine uwapendao.