Last Updated on 12/02/2024 by Tabibu Fadhili Paulo
Namna kitunguu swaumu kinavyoongeza nguvu za kiume
Kitunguu swaumu na nguvu za kiume
Kama umekuwa ukijiuliza iwapo kitunguu swaumu kinaongeza nguvu za kiume na namna gani kinafanya kazi hiyo leo ndiyo mwisho wa wewe kuendelea kujiuliza swali hilo sababu naeleza kila kitu namna kitunguu swaumu kinavyoongeza nguvu za kiume kupitia makala hii.
Endelea kusoma…
Jina langu ni Fadhili Paulo ni tabibu wa tiba asili nipo Kibugumo Mji Mwema Kigamboni Dar Es Salaam.
Namna kitunguu swaumu kinavyoongeza nguvu za kiume :
1. Kinaongeza msukumo wa damu mwilini
Moja ya sababu ya kitunguu swaumu kusemwa kinaimarisha nguvu za kiume ni uwezo wake wa asili wa kuboresha msukumo wa damu mwilini.
Msukumo mzuri wa damu ndiyo kitu cha lazima ili kuwa na nguvu za kiume, kitu chochote kinachoweza kuathiri mtiririko huru wa damu kwenye mishipa ya damu mwilini kinaweza kushusha nguvu za kiume.
Kitunguu swaumu kina kitu ndani yake kijulikanacho kwa kitaalamu kama ‘allicin‘ ambacho tafiti mbalimbali zinasema kinahusika na kuboresha mzunguko na mtiririko wa damu mwilini.
Utafiti mmoja wa mwaka 2014 unasema kitunguu swaumu ni msaada mkubwa pia kwa wanaume wanaokaribia kuzeeka au walio tayari ni wazee kuwa na afya nzuri kitandani
2. Kinaimarisha homoni ya testosterone
Namna nyingine kitunguu swaumu kinaimarisha nguvu za kiume ni uwezo wake wa kuiongezea ubora homoni mhimu kwa mwanaume ijulikanayo kama testosterone.
Kitunguu swaumu kinaamsha na kuongeza usawa wa homoni mhimu kwa afya ya nguvu za kiume testosterone.
Testosterone ni mhimu katika afya ya mwanaume, ndiyo homoni inayohusika moja kwa moja na tendo la ndoa kwa wanaume.
Ukiacha huo uwezo wa kuongeza usawa wa homoni ya testosterone, kitunguu swaumu kinatajwa kama chakula cha asili kinachoweza kuboresha na kuimarisha mbegu za kiume na hivyo kuwa msaada kwa upande wa afya ya uzazi kwa mwanaume.
3. Kinaimarisha Kinga ya mwili
Mara nyingi nimeandika kwamba Kinga ya mwili ni mhimu sana linapokuja suala la nguvu za kiume.
Ni vigumu mwanaume kuwa na nguvu za kiume kama Kinga yake ya mwili ipo chini.
Kitunguu swaumu kinaongeza Kinga ya mwili mara dufu na kwa haraka sana hasa kama utakichanganya na mtindi.
Kitunguu swaumu kina viambata vinavyosaidia kuondoa sumu na Kusafisha damu na mwili.
Wote tunafahamu kuwa moja ya vitu vinavyoharibu nguvu za kiume ni sumu kuzidi mwilini.
Sumu ikishazidi mwilini ni vigumu damu kutiririka vizuri na pia kinga ya mwili lazima itashuka.
Kitunguu swaumu kimebarikiwa kuwa na viondoa sumu (antioxidants) na hivyo kuwa na uwezo wa kudhibiti bakteria na virusi mbalimbali vinavyoweza kuleta magonjwa mwilini.
4. Kinaweka sawa shinikizo la juu la damu
Moja ya magonjwa yanayoweza kuharibu nguvu za kiume ni shinikizo la juu la damu (BP).
Ni vigumu mwanaume kuwa na nguvu za kiume kama anasumbuliwa na shinikizo la juu la damu.
Kitunguu swaumu kinadhibiti shinikizo la juu la damu kwanza kama matokeo yake ya kuongeza na kuboresha msukumo na mtiririko wa damu mwilini, pili kama matokeo ya kuwa na kiambata kijulikanacho kama ‘sulfur‘ ambacho chenyewe kinahusika na kuweka sawa shinikizo la damu mwilini.
Ni mhimu kukujulisha pia kitunguu swaumu si salama kutumika na mtu mwenye shinikizo la chini la damu.
Kama hiyo haitoshi Kitunguu swaumu hakitibu shinikizo la juu la damu pekee bali pia ni dawa mjarabu kwa magonjwa mengine yanayoweza kuleta upungufu wa nguvu za kiume ambayo ni kolesto, magonjwa ya mifupa, ugonjwa wa moyo, saratani na matatizo kwenye mfumo wa mmeng’enyo wa chakula.
Namna ya kutumia kitunguu swaumu ili kuongeza nguvu za kiume :
Kitunguu swaumu ni kiungo cha jikoni, ni chakula kama vilivyo vyakula vingine kama vile nyanya au bamia, hivyo unaweza kukiongeza karibu kwenye kila mboga au chakula unachopika.
Kama utapenda kukiongeza kwenye vyakula unavyopika ni vema kiongezwe mwishoni kabisa wakati chakula kinakaribia kuiva na kutolewa jikoni.
Lakini ili upate faida kamili za kitunguu swaumu na kiweze kukuongezea nguvu za kiume utatakiwa kukitumia kikiwa kibichi bila kukipitisha kwenye moto kwa kufuata hatua zifuatazo;
- Chukuwa kitunguu swaumu kimoja
- Kigawanyishe katika punje punje
- Chukua punje 6
- Menya punje moja baada ya nyingine
- Kisha vikatekate (chop) vipande vidogo vidogo sana na kisu na uache hivyo katika hewa kwa dakika 10, kama hautaacha kwa dakika 10 kabla ya kukitumia “allicin” ambayo ni kemikali mhimu sana ambayo ndiyo inakifanya kitunguu swaumu kuwa dawa kubwa haitajiunda kwenye hicho kitunguu swaumu
- Meza kama unavyomeza dawa na maji nusu lita kila unapoenda kulala.
Namna nyingine nzuri zaidi ni kuviweka ndani ya kikombe kimoja (robo lita) cha mtindi freshi koroga vizuri na unywe na hii itakusaidia kupunguza harufu mbaya ya kitunguu swaumu huku ukipata faida nyingine mhimu zilizomo kwenye mtindi.
Fanya hivi kila baada ya siku 1 unapoenda kulala kwa wiki 3 mpaka 4.
Unaweza pia kuendelea kukitumia hata kama umepona tatizo lako.
Ukiona kichwa kizito au kinauma pumzika kutumia kitunguu swaumu kwa siku 3 hivi kisha endelea tena, mhimu usitumie kila siku bali ni kila baada ya siku 1.
Kitunguu swaumu kinachoweza kutumika hivi kama dawa ni kile kinacholimwa Tanzania pekee! vile vidogo vidogo ukitafuna ni vikali sana ndiyo hivyo tu vina dawa ndani yake, tofauti na hivyo au kama havijalimwa Tanzania vitumie kwa kazi nyingine lakini siyo hii ya kuimarisha nguvu za kiume.
Pia ni mhimu kufahamu kuwa kitunguu swaumu hakiwezi kutumika kama dawa kwa kila mwanaume.
Kama unasumbuliwa na shinikizo la chini la damu usitumie, kama una aleji na kitunguu swaumu usitumie pia kama kuna dawa yoyote ya hospitali unakunywa usitumie kitunguu swaumu kwa namna hii niliyoeleza hapa mpaka umewasiliana kwanza na Daktari aliyekupa hizo dawa unazotumia sasa.
Tafadhari Share makala hii kwa ajili ya wengine uwapendao