Sababu 6 zinazopelekea kuvunjika kwa ndoa nyingi

Last Updated on 26/09/2022 by Tabibu Fadhili Paulo

Sababu 6 zinazopelekea kuvunjika kwa ndoa nyingi

Wanaume mnafahamu nimekuwa nikiwauzia dawa za asili kwa ajili ya kuimarisha nguvu za kiume na wanawake pia baadhi yenu nimekuwa nikiwauzia dawa za asili kwa ajili ya kuamsha hisia na kuongeza hamu ya tendo la ndoa.

Sasa dawa peke yake bila kuwaeleza na mambo mengine yanayoweza kuboresha mahusiano yenu nje ya tendo la ndoa nitakuwa siwatendei haki.

Asilimia mpaka 40 ya ndoa na mahusiano mengi hufa njiani na leo nimeona niwaandikie sababu kwanini ndoa na mahusiano mengi vinakufa mapema tofauti na matarajio ya wahusika na jamii kwa ujumla.

Sababu 6 zinazopelekea kuvunjika kwa ndoa nyingi

1. Kukosekana kwa uaminifu

Uaminifu ni jambo la mhimu sana ili kujenga na kuendeleza mahusiano yoyote hasa ya mapenzi.

Uaminifu ni kama gundi inayowaweka pamoja watu wawili ili wabaki pamoja.

Bila uaminifu hakuna uhusiano wowote unaweza kufika popote.

Uaminifu ni bidhaa adimu sana na unaweza kutumia miaka mingi sana kuujenga lakini ukaubomoa ndani ya siku 1.

Wenza ni lazima wajijengee tabia ya kuaminiana baina yao na kila mmoja kati yenu ni lazima aishi na kutoonyesha hali yoyote ya kuweza kutiliwa shaka na mwenzake.

Kama mmoja wenu ana tabia za siri kwenye mambo yake mengi, kama mmoja wenu ana mipango yake binafsi ambayo hamshirikishi mwenzake, kama mmoja wenu ana mi – password kila kona bila hata sababu yoyote basi hizo ni ishara uhusiano wenu hauwezi kufika popote.

2. Kuchepuka

Kuchepuka ni hali inayoweza kuvunja uhusiano wowote haraka sana.

Kama wewe ni mwanaume au wewe ni mwanamke na unachepuka basi tambua hiyo ni moja ya sababu zinazoweza kuvunja uhusiano uliopo baina yenu.

Kuna baadhi ya wanaume hata baadhi ya wanawake ni wajinga sana kiasi siwezi kukueleza ukaamini.

Mwanaume au mwanamke mjinga anaweza kuchepuka ndani ya mtaa huo huo mmoja mnaoishi hadi majirani wanajua lakini yeye anaona ni kawaida.

Kama unapenda mahusiano yako yadumu basi epuka kuchepuka.

Kuchepuka ndiyo tabia pekee inaweza kuvunja uhusiano wako wakati wowote pengine bila hata taarifa na pengine ukapatwa na mambo mengine mabaya kama vile ugomvi usioisha na wengine huenda mbali hata kusababisha kifo kwa mwingine.

Kusema ukweli kabisa kama unaipenda ndoa yako basi achana na mambo ya kuchepuka

Ni wanawake wachache sana wanaweza kuvumilia kuishi na mwanaume mchepukaji na hakuna mwanaume hata mmoja anayeweza kuendelea kuvumilia kuishi na mwanamke mchepukaji.

Katika mambo yote yanayoweza kuvunja mahusiano, kuchepuka ndiyo namba 1 na inachukua karibu ya asilimia 80 ya ndoa zote zinazovunjika.

Jambo la mhimu hapa kufahamu ni kuwa unapogundua na kujihakikishia kweli kwamba mwenza wako anachepuka basi tatizo lipo kwa mwenza wako tu na siyo kwa huyo anayechepuka naye na utatakiwa ushughulike na mwenza wako tu na siyo huyo mwingine.

Na pia haijalishi umepokea kwa namna gani taarifa au uthibitisho wa mwenza wako kuchepuka basi unatakiwa kudhibiti nafsi yako usimdhuru yoyote wala usijidhuru mwenyewe binafsi. Hili ni tukio moja baya kwenye maisha yako na haimaanishi ndiyo mwisho wa dunia.

Vyovyote itakavyokuwa fanya kila uwezalo kuepuka kudhuru yoyote na ruhusu maisha mengine yaendelee.

3. Kukosekana kwa mawasiliano

Kwenye maisha ya ndoa au mahusiano yoyote mawasiliano ni mhimu sana.

Kama mmoja wenu anajidai yupo bize sana na hana muda wa kuwasiliana na mwenzake basi ni wazi huo uhusiano hautafika popote.

Wanandoa wengi wanashindwa kuwasiliana mara kwa mara kwenye mahusiano yao kwa visingizio kwamba wanaongea lugha tofauti (kemia yao haiendani).

Lakini kukosekana kwa mawasiliano mazuri baina yenu kunaweza kuanza kuweka ukuta na umbali baina yenu na mkaanza kuishi kama wapangaji wa nyumba moja badala ya kuwa mwili mmoja.

Kwenye vitu vinavyoweza kuvunja uhusiano kukosekana kwa mawasiliano kunaweza kuchukuwa mpaka asilimia 70 ya mahusiano yote yanayovunjika njiani.

Sasa mawasiliano hapa haina maana ya kutumiana sms au kumpigia mtu simu kila baada ya nusu saa!

Walau usimalize masaa 6 hujamjulia hali mwenzako.

Toa taarifa wakati wowote unahisi utachelewa kurudi nyumbani na useme wazi upo wapi na simu yako ibaki hewani wakati wote mpaka utakapofika nyumbani.

Sasa unakutana na mwanamke mmoja mjinga anarudi nyumbani saa tano usiku na hakukujulisha anaenda wapi na atarudi saa ngapi na mahusiano yake yakivunjika anaanza kulaumu wachawi kumbe ni upumbavu wake mwenyewe.

4. Kutofahamu umhimu wa mwenza wako

Hili linaweza kukushangaza lakini ni kweli lipo kwenye baadhi ya ndoa na mahusiano.

Unakuta mwanaume au mwanamke haoni umhimu wowote wa mwenzake.

Anamuona ni wa kawaida tu na anamchukulia poa.

Kuna mwanamke anaweza kumsikiliza sana mchungaji wa kanisani kuliko hata anavyomsikiliza mmewe.

Kuna mwanamke anaweza kuwasikiliza sana ndugu, marafiki na jamaa wengine kuliko hata anavyomsikiliza mme wake.

Unakuta mtu anaishi na mwenzake lakini haoni umhimu wala mchango wowote wa mwenzake.

Hana shukrani kwa lolote analotendewa na mwenzake.

Na tafiti nyingi zinasema ndoa nyingi huvunjika kwa sababu tu ya wanandoa kuacha kutumia neno AHSANTE mara nyingi kwenye maisha yao baada ya miaka kadhaa ya kuoana.

Kila mtu hujituma zaidi pale anapogundua mchango wake unathaminiwa na anaambiwa AHSANTE.

Hata kama mwenzio amekuletea zawadi ya pipi ya shilingi 200 onyesha kushangazwa na hali hiyo, jifanye unalia kwa furaha na umwambie AHSANTE mme wangu au AHSANTE mke wangu.

Usiache kuendelea kutumia neno AHSANTE mara nyingi kwenye maisha yenu hata kama mmeishi tayari miaka mingi.

Kuna wanandoa wanaishiishi tu hata haoni umhimu wa mwenza wake, anamchukulia poa tu mwenzake.

Tambua huyo uliyenaye ni mpango wa Mungu na kwamba kama unamchukulia poa basi unaweza kumpoteza wakati wowote.

5. Ukatili

Zamani tulizoea kuona ukatili wa wanaume kwa wake zao lakini miaka ya sasa tunashuhudia pia ukatili wa wanawake kwa waume zao ukizidi kuongezeka.

Tabia ya kuwa mkali kupita kiasi, kufoka bila sababu, kelele, kumpiga mwenza wako ni tabia za kikatili zinazoweza kuvunja uhusiano baina yenu.

Mwanaume mkatili ni mpumbavu kabisa.

Huhitaji ukali sana au vitisho ili kuishi na mwingine.

Kwanza ukiona kwenye ndoa au kwenye mahusiano yenu mmeanza kupigana basi tambua hakuna mwisho mwema kati yenu.

Hata kama mwenzio atakukosea kwa kiasi gani bado hakuna sababu ya kumpiga.

Unaweza kumfokea kidogo hasa mkiwa wawili tu chumbani na mtu mwingine yoyote asisikie lakini siyo KUMPIGA.

Ukiona kila mara mkikosana mwenza wako anakimbilia kukupiga tambua hakutakuwa na mwisho mwema kati yenu.

Kama mwenzio kakukosea mweleweshe tu kwa maneno siyo kwa kipigo.

Kama hakuelewi kwa maneno achana naye kwa amani siyo lazima kupigana.

Ukatili upo wa aina nyingi na siyo lazima iwe ni kupiga tu.

Hata baba kushindwa kutoa hela ya chakula ni ukatili pia.

Hata mwanamke kumnyima mme wake tendo la ndoa bila sababu inayoeleweka ni ukatili pia.

Imesomwa na watu 245
Sababu 6 zinazopelekea kuvunjika kwa ndoa nyingi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WhatsApp 0714800175