Sababu za kupungua kwa nguvu za kiume

Last Updated on 01/11/2024 by Tabibu Fadhili Paulo

Sababu za kupungua kwa nguvu za kiume 

Kuishiwa nguvu za kiume ni jambo la kawaida kwa wanaume wengi.

Ni kushindwa kwa uume kudumu kusimama barabara kwa ajili ya tendo la ndoa, au kuwahi kufika kileleni.

Ni jambo linaloweza kumtokea kila mwanaume bila kujali ni nani.

Linaweza kukutokea mara moja moja kwa mwezi au mara kadhaa kwa mwaka kwani hakuna mwanaume anayeweza kuwa na uwezo wa kuchelewa kufika kileleni kila atakaposhiriki tendo la ndoa mwaka mzima.

Ingawa kama linakutokea kila mara mfulululizo kwa kipindi kirefu basi hapo ni lazima upate msaada wa tiba na ushauri juu ya vyakula na mazoezi.

Tatizo la kupungukiwa nguvu za kiume huongezeka sababu ya umri.

Tafiti mbalimbali zinasema wanaume wa umri kuanzia miaka 61 na kuendelea ndiyo wanapatwa na tatizo hili zaidi kuliko wanaume wenye umri wa miaka 41 Kushuka chini.

Wanaume wenye elimu ndogo juu ya utendaji kazi wa mwili na afya ndio wanaokabiliwa sana na tatizo hili.

Hii ni kutokana na kwamba wengi wao wanakuwa hawaelewi aina ya vyakula vinavyoongeza nguvu za kiume na za mwili kwa ujumla, namna wanavyotakiwa kuishi ili kupunguza janga hilo, wanakunywa pombe na hawajishughulishi na mazoezi ya viungo.

Mazoezi ya viungo hupunguza tatizo la kuishiwa nguvu za kiume kwa asilimia kubwa sana.

Kupungukiwa nguvu za kiume kunaweza pia kuwa kumetokana na mambo ya kihisia (emotional causes).

Vitu vingine vinavyoweza kusababisha kupungua kwa nguvu za kiume ni pamoja na magonjwa kama vile ugonjwa wa Kisukari na Shinikizo la juu la damu.

Asilimia 51 mpaka 61 ya wanaume wanaosumbuliwa na kisukari wanapatwa na tatizo la uume kushindwa kusimama vizuri.

Kadharika wagonjwa wa kiharusi na wale waliotekwa na ulevi nao ni miongoni mwa watu wanaoweza kupatwa kirahisi na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.

Walevi wengi wa pombe kwa mfano wanakabiliwa na tatizo la uzalishaji mchache wa mbegu za kiume (manii).

Wengine wenye hatari ya kupatwa na tatizo la kupungukiwa nguvu za kiume ni pamoja na;

  1. Wanaume wenye shinikizo la juu la damu,
  2. Wenye matatizo ya tezi,
  3. Waliowahi kufanya upasuaji katika viungo vya uzazi wakabaki na majeraha,
  4. Watu wanaotumia dawa zenye kemikali kiholela bila kushauriwa na wataalamu na
  5. Wale wanaougua maradhi yanayodhoofisha msukumo wa damu kwenda katika mishipa ya uume.

Pamoja na hayo, tatizo la upungufu wa nguvu za kiume linaweza kutibika kwa watu wa rika zote.

Kabla daktari hajaanza kukutibu tatizo la kupungukiwa nguvu za kiume, atataka kujuwa:

1. Umri wako
2. Utendaji wa tendo la ndoa kabla na baada ya kuugua
3. Afya yako kwa ujumla
4. Matatizo katika ndoa ikiwa kuna ugomvi wowote n.k
5. Nini sababu ya wewe kutaka kupona

Kuwa na mtaalamu mzuri ni njia ya kwanza katika kupata uponyaji sahihi.

Ni mhimu wewe kujisikia vizuri na kuwa na imani na daktari wako. Kwa kufanya hivi utakuwa umepiga hatua nzuri kelekea kwenye ufumbuzi wa tatizo lako.

Imesomwa na watu 1
Sababu za kupungua kwa nguvu za kiume

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WhatsApp 0714800175