Uhusiano wa kitambi na upungufu wa nguvu za kiume

Last Updated on 11/02/2024 by Tabibu Fadhili Paulo

Uhusiano wa kitambi na upungufu wa nguvu za kiume

Wanaume wengi wanaopenda kufuatilia afya zao huwa hawapendi kuwa na kitambi na wanafanya kila wawezalo ili kukiepuka.

Lakini wapo baadhi ya wanaume wachache ambao huhangaika kwa kila njia ili wapate kuwa na kitambi ili iwe rahisi waonekane ni mabosi na ni watu wenye hela!

Ndiyo wapo wanaume ambao hupenda sana waonekane wana hela au ni mabosi na namna nzuri ya kutimiza hitaji hilo ni kufuga kitambi!

Lakini kiafya kitambi ni ugonjwa na ni dalili ya magonjwa mengine makubwa zaidi kama kolesto, kisukari, shinikizo la juu la damu, kupungukiwa nguvu za kiume na magonjwa mengine mengi.

Kile wanaume wengi wanashindwa kuelewa ni kudhani kwamba upungufu wa nguvu za kiume ni ugonjwa unaojitegemea kitu ambacho si kweli.

Kupungua kwa nguvu za kiume siyo ugonjwa bali ni dalili au ni matokeo ya uwepo wa ugonjwa au magonjwa mengine ikiwemo kitambi.

Je kitambi kinaweza kupelekea mwanaume kupungukiwa nguvu za kiume?

Jibu la haraka ni NDIYO kitambi kinaweza kuathiri moja kwa moja uwezo wa mwanaume kitandani.

Wakati wanaume wengine wanaweza kupata upungufu wa nguvu za kiume kama matokeo ya mzunguko hafifu wa damu mwilini au kama matokeo ya kuzidi ya kutumia vilevi, wapo Wanaume wengine wanaoishiwa nguvu za kiume kama matokeo ya mafuta kuzidi mwilini na hivyo kuwapelekea kuwa na uzito uliozidi, unene kupita kiasi na kitambi.

Ingawa nimeshakutana na baadhi ya wanaume wanaodai unene wao au vitambi vyao ni vitu vya kurithi kwa maana kwamba baba alikuwa hivyo hata babu alikuwa hivyo, mimi bado nakataa dhana hii, sikubaliani na utetezi wao huo na neno langu kwao ni kuwa waendelee kupambana ili kupunguza uzito na kuondoa kitambi.

Wasiridhike na hiyo hoja kwamba wamerithi unene na kitambi.

Mimi nawataka waendelee kuwa wadadisi zaidi na waendelee kupambana mpaka kitambi kipotee kwani ni jambo linalowezekana kama ukiamua kweli kweli na ukiwa na hasira ya kutosha ya kuondokana na tatizo.

Penye NIA pana NJIA.

Kuwa na uzito, unene na kitambi ni jambo linaloweza kukuletea maradhi mengine yanayosababisha upungufu wa nguvu za kiume kama vile ugonjwa wa kisukari, shinikizo la juu la damu, magonjwa ya moyo, kolesto na msongo wa mawazo.

Bado unajiuliza ikiwa kitambi kinaweza kuleta upungufu wa nguvu za kiume au la?

Unataka kufahamu kama kuondoa kitambi kunasaidia kukurudishia nguvu zako za kiume?

Uhusiano wa kitambi na upungufu wa nguvu za kiume :

1. Kitambi kinasababisha kushuka kwa homoni mhimu kwa nguvu za kiume ijulikanayo kama Testosterone

Ni kawaida sana kwa wanaume wengi wenye vitambi kukutwa pia wana homoni ya testosterone pungufu au ipo chini ya kiwango kinachohitajika.

Kwa kifupi ni kuwa wanaume wenye upungufu wa homoni ya testosterone wengi wao wanakabiliwa pia na tatizo la kuongezeka uzito, unene na kitambi kwa wakati mmoja kama matokeo ya kuongezeka kwa homoni zingine ambazo ni estrogen na cortisol.

Kushuka kwa homoni ya testosterone pia kunahusishwa na matatizo mengine ya kiafya kama vile :

* Msongo wa mawazo
* Kupotea kwa misuli
* Kupoteza hamu ya tendo la ndoa
* Kupoteza nywele kichwani
* Kupungua kwa nguvu za kiume

Tafiti nyingi za kisayansi zimethibitisha kuwa kupungua kwa testosterone kuna uhusiano na kuongezeka kwa unene na uzito.

Tafiti zimethibitisha pasipo na shaka kwamba kupungua uzito kunasaidia kuongeza uzalishwaji wa homoni ya testosterone jambo ambalo linaweza kukusaidia kutibu tatizo la upungufu wa nguvu za kiume na kuwahi kufika kileleni.

Baadhi ya wanaume wanaopambana na kufanikiwa kupunguza uzito na kitambi huona wazi misuli na mishipa yao imerudi na kuongezeka jambo linalowawezesha kufurahia stamina mpya na uwezo mkubwa wa kuhimili tendo la ndoa.

2. Kitambi kinapunguza mtiririko huru wa damu kwenda kwenye uume

Kama unavyojuwa ili mheshimiwa aweze kusimama vizuri na kwa muda mrefu unahitaji damu yako iwe ni ya kutosha na inatiririka vya kutosha na kwa uhuru wote kwenda kwenye mishipa, ogani na viungo vingine ikiwemo uume (mheshimiwa).

Kuna matatizo mengi ya kiafya yanayoweza kuathiri utiririkaji huo huru wa damu ikiwemo shinikizo la juu la damu na kolesto, na haya magonjwa kwa sehemu kubwa ni matokeo ya kuzidi kwa uzito, unene na kitambi.

Magonjwa haya ambayo ni sehemu ya pili ya matokeo ya kuzidi kwa uzito, unene na kitambi huwa yanaleta athari (damage) kwenye mishipa ya damu na kufanya usimamaji mzuri na wa uhakika wa mheshimiwa kuwa jambo gumu au lisilowezekana kabisa.

Wanaume wengi wenye kitambi kwa sababu wana pesa huwa pia na tabia au mazoea mabaya ya kula vyakula feki (visivyo na afya) yaani vyenye mafuta mengi, sukari nyingi na kolesto.

Kula vyakula hivyo visivyo na afya kunapelekea afya mbovu kwenye mfumo wa upumuwaji, pia huleta mishipa kuzibika na kupungua vipenyo vyake (atherosclerosis).

3. Kitambi kinaleta shida kwenye mfumo wa mmeng’enyo wa chakula

Injini ya afya ya mwili wa binadamu ipo tumboni.

Afya yako huanzia tumboni Kisha kwenye ubongo.

Unapokuwa na kitambi mfumo wako wa mmeng’enyo wa chakula unaathiriwa sana kwenye utendaji wake wa kila siku.

Chakula unachokula hakimeng’enywi vizuri na hivyo hakitumiki ipasavyo na mwili ili kukuletea nguvu.

Ni kawaida pia kwa watu wenye kitambi kusumbuliwa na bawasiri, kupata choo kigumu au kukosa choo kwa siku kadhaa mfululizo.

Matatizo yoyote yanayoathiri afya ya mfumo wako wa mmeng’enyo wa chakula yanaathiri moja kwa moja uwezo wa mwanaume kitandani.

4. Kitambi kinafanya mheshimiwa aonekane ni mdogo na kukuondolea kujiamini.

Mara nyingi wanaume wenye kitambi husumbuliwa pia na tatizo la uume kuwa mdogo.

Ukiwa na kitambi automatically utaanza kujihisi uume wako ni mdogo na hali hii itakuondolea uwezo wako wa kujiamini.

Kujiamini kunapopungua huwezi kushiriki tendo la ndoa kwa hamasa na kwa uwezo mkubwa kama matokeo ya aibu na wapo ambao huamua kutokuwa na mahusiano kabisa kama matokeo ya aibu hii.

Ndiyo ni kweli baadhi ya watu wanaweza kukuona wewe ni boss na una hela ukiwa na kitambi lakini madhara yake kiafya ni mengi ikiwemo kushuka kwa nguvu zako za kiume.

Je kuondoa kitambi kunaweza kukusaidia kurudisha nguvu zako za kiume?

Habari njema ni kuwa ukiamua kupambana kweli kweli na ukafanikiwa kuondoa kitambi nguvu zako lazima zitarudi.

Uwezo wako wa kujiamini kitandani utarudi.

Utajisikia vizuri tena na mwenye afya.

Kumbuka nimetumia neno KUPAMBANA.

Siyo jambo rahisi tu kupunguza uzito au kitambi kama baadhi ya wanaume wanavyofikiri.

Wapo baadhi ya wanaume hupenda kuchukulia poa kila kitu kwenye maisha, wanafikiri kila kitu kinapatikana kirahisi tu na ni bure.

Wao hudhani ili kuondokana na kitambi au uzito ni kitendo tu cha kuagiza dawa na kunywa kisha wanasubiri kupona kama vile wanaumwa malaria.

HAPANA, maisha hayapo hivyo, kuna baadhi ya vitu huwezi kuvipata bila kupambana tena kupambana kwa muda mrefu mfululizo.

Hata mimi nimewahi kuwa na kitambi na kilinisumbua sana kwa miaka mpaka nilipoamua kupambana na kusema liwalo na liwe na hatimaye nilifanikiwa kukiondoa kitambi na mpaka leo huwa siwazi lolote kuhusu kitambi.

Kitambi kilinianza pole pole mwaka 2008 na nikaja kufanikiwa kukiondoa kabisa maishani mwangu mwaka 2011 nikiwa kisiwa cha Mafia mkoa wa Pwani.

Haikuwa rahisi kama wewe unavyodhani.

Nilienda gym mbali mbali, nilijinyima kula, nilitumia dawa, nilifuatilia program mbali mbali mpaka nilipofanikiwa.

Ili kuondoa kitambi unahitaji vitu vifuatavyo kwa pamoja kwa kipindi kirefu ;

1. Kubadili mfumo wako wa vyakula na vinywaji

2. Kufanya mazoezi ya kukimbia pole pole (jogging) dakika 60 mfululizo bila kupumzika (nonstop) kila siku

3. Kuacha kukaa chini au kwenye kiti masaa mengi

4. Kufunga kula mara kwa mara

5. Kuondoa msongo wa mawazo

6. Kutumia dawa ya asili sahihi inayoweza kukusaidia kupunguza mafuta, kuchoma mafuta mwilini na kukupunguzia hamu ya kula.

Mpaka hapo ni matumaini yangu umenilewa vema juu ya uhusiano wa kitambi na upungufu wa nguvu za kiume

Ikiwa utahitaji dawa nzuri ya asili isiyo na madhara ya kukusaidia kuondoa kitambi niachie tu ujumbe kwenye WhatsApp na nitakuwa bega kwa bega na wewe kila mara KUKUELEKEZA kuhusu vyakula, vinywaji, mazoezi na MAMBO MENGINE YASIYOHUSU dawa au chakula au mazoezi yanayoweza kukusaidia kuondoa kitambi na uzito kwa ujumla.

Tafadhali SHARE post hii kwa ajili ya wengine uwapendao.

Imesomwa na watu 342
Uhusiano wa kitambi na upungufu wa nguvu za kiume

2 thoughts on “Uhusiano wa kitambi na upungufu wa nguvu za kiume

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WhatsApp 0714800175