Unaifahamu G-Spot, vipi kuhusu A-Spot?

Unaifahamu G-Spot, vipi kuhusu A-Spot?

Last Updated on 25/03/2022 by Tabibu Fadhili Paulo

Unaifahamu G-Spot, vipi kuhusu A-Spot?

Watu wengi au wanaume wengi wanafahamu kuhusu G-Spot lakini hawaifahamu A-Spot

Ndiyo, nafahamu wapo wengine wengi hata hiyo G-Spot yenyewe hawajui inapatikana wapi kwenye mwili wa mwanamke

Wataalamu wengi wa elimu ya tendo la ndoa wanasema kulisisimua hili eneo la A-Spot kunaweza kumsaidia mwanamke kuondokana na tatizo la kuwa na uke mkavu, kunamfanya mwanamke afurahie zaidi anapoandaliwa kabla ya kumwingilia na pia kunamsaidia mwanamke kufika kileleleni kirahisi zaidi

Kwenye makala hii nitaeleza A-spot ni nini, inapatikana wapi kwenye mwili wa mwanamke na namna ya kuiamsha

A-Spot ni nini?

Ni moja kati ya zile sehemu 5 mhimu kwenye uke au kwenye sehemu za siri za mwanamke ambazo humpa raha sana mwanamke zinaposisimuliwa pole pole na kwa usahihi

Ukiacha A-spot sehemu zingine ni ;

*G-Spot
*O-Spot
*The cervix na
*The pelvic floor muscles

Kwa leo nitakuwa bize na A-Spot, hizo 4 zingine nitazitolea ufafanuzi siku nyingine nikipata muda

Inaposisimuliwa hii A-Spot inaweza kuleta raha sana kwa mwanamke na kitendo hicho humsaidia mwanamke kuwa na unyevunyevu ukeni na hivyo kuondoa tatizo la kuwa na uke mkavu linalowasumbuwa baadhi ya wanawake.

Utafiti mmoja uliowahi kufanywa mwaka 1997 ulihitimisha kuwa wanawake wengi hutokewa na msisimko zaidi na kuloa sehemu zao za siri baada ya dakika 10 mpaka 15 za kuichezea na kuisisimua A-Spot.

Daktari ambaye aliandika kwa mara ya kwanza duniani kuhusu A- Spot anasema kulisisimua eneo hili lenye A-Spot kunaweza kusaidia kutibu baadhi ya matatizo ya wanawake wakati wa tendo la ndoa ikiwemo tatizo la kuwa na uke mkavu na maumivu wakati wa tendo la ndoa.

Unaifahamu G-Spot, vipi kuhusu A-Spot?

Je kila mwanamke anayo A-Spot?

Kinadharia kila mwanamke mwenye uke anaweza pia kuwa na hii A-Spot.

Hata hivyo watafiti bado hawajafanya utafiti wa kutosha kwa idadi kubwa ya wanawake ili kuweza kuhitimisha kwamba eneo hili lipo kwa kila mwanamke.

Baadhi ya watafiti wanasema hakuna uhakika wa kisayansi kuthibitisha kwamba A-Spot ipo kwa kila mwanamke.

Baadhi ya watafiti wanasema wanawake wengi wana miishio mingi ya neva za kusisimua karibu na eneo ilipo A-Spot.

Kwa mfano utafiti mwingine wa mwaka 1985 uligundua kuwa sehemu ya juu ya uke na sehemu ya chini ya nyuma ya ukuta wa uke ndizo sehemu zenye mishipa au neva zenye kusisimua zaidi katika sehemu za siri za mwanamke.

Kwenye utafiti huo wa 1985 asilimia 89 ya wanawake waliokuwa kwenye majaribio hayo walifanikiwa kufika kilelelni kirahisi zaidi kama matokeo ya kusisimuliwa sehemu hizo mbili yaani sehemu ya juu mbele ya uke na sehemu ya chini nyuma ya ukuta wa uke.

Namna ya kuifikia A-Spot :

A-spot inapatikana sehemu ya chini kabisa kwenye uke wa mwanamke.

Chini kabisa na inapaswa kuguswaguswa pole pole sana na uume au kidole chako kirefu.

Wakati G-Spot ipo katikati ya uke wa mwanamke yaani kama inch mbili hivi chini toka juu ya uke (mashavu ya uke) wa mwanamke. G-Spot Ipo upande wa juu kama inch 2 ndani ya uke.

Karibu kila mwanaume au mwanaume yoyote mwenye uume kuanzia inch 4 anaweza kuifikia hii G-Spot na kuweza kumfikisha mwanamke kileleni.

Kumbe hii A-Spot yenyewe ipo chini kabisa na haihitaji fujo wakati wa kuisisimua na uume na ndiyo sehemu inayompa mwanamke raha zaidi na kumuwezesha kufika kileleni kirahisi kuliko G-Spot.

Kama mwanaume ana uume mfupi au mdogo sana chini ya inch 4 au 3 hawezi kuifikia hii sehemu kwa kutumia uume wake. Anaweza kujaribu kuifikia kwa kutumia kidole chake cha mkono kirefu na kisafi.

Ukitumia uume unaweza kuanzia katikati ya uke ukicheza hapo muda mrefu kwa dakika kadhaa huku pole pole bila fujo ukienda chini kuigusagusa hii A-Spot kwa sekunde kadhaa na urudi juu katikati na kurudi chini tena bila fujo.

Hapo mwanamke husikia raha na kupoteza fahamu, ataloa ukeni na kufika kilelelni kirahisi zaidi.

Ukiacha kidole unaweza pia kutumia uume roboti (sex toy) kulifikia eneo hilo. Kuwa makini na njia hii kwani si ya kuitumia kila siku inaweza kuleta madhara kwa mwanamke sawa na madhara ya kujichua au kujipiga punyeto kwa mwanamke.

Kuna uwezekano pia kuna mwanamke unaweza kujitahidi kumsisimua eneo hili la A-Spot na asisikie raha au msisimko wowote kwa haraka au kwa nguvu kama mwanamke mwingine.

Hilo ni kutokana na kuwa kila mwanamke ana kiasi chake cha msisimko na kinatofautiana toka mwanamke mmoja hadi mwingine na ndiyo maana kuna mwanamke ukitaka tu kumwingiza kidole ukeni kwake anakataa na hataki kabisa, wakati kuna mwingine anapenda na anaweza hata kuchukuwa mkono wako na kuuelekezea huko.

Kabla hujaondoka soma na hii pia > Sehemu kuu 8 zenye msisimko zaidi katika mwili wa mwanamke

SHARE POST HII NA WENGINE UWAPENDAO

Unaifahamu G-Spot, vipi kuhusu A-Spot? Share on X

Bonyeza kengele ili uwe unapata kidokezo (notification) kila mara ninapochapisha makala mpya kwenye blog hii.

Imesomwa na watu 1,826
Unaifahamu G-Spot, vipi kuhusu A-Spot?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WhatsApp 0714800175